Tetesi: SUA: Prof Mstaafu afariki kwa tatizo la kushindwa kupumua! Ni Prof wa tatu kufariki ndani ya miezi miwili kwa tatizo kama hilo

Tetesi: SUA: Prof Mstaafu afariki kwa tatizo la kushindwa kupumua! Ni Prof wa tatu kufariki ndani ya miezi miwili kwa tatizo kama hilo

Taarifa hizi nimezipata kwa rafiki wa karibu aliyeko SUA.

Sijawa na uhakika wa kutosha kuhusu chanzo hiki cha habari . Imenitia Uchungu kwa vile hawa walikuwa watu maarufu kitaaluma na waliotoa mchango kwa maendeleo ya uchumi nchini. Iweje taarifa zao zisisikike au kutangazwa na vyombo vikuu vya habari?
Huu uzi ufungwe na mleta hii post aonywe
 
Nasikia na Meneja wa Banki ya NMB Geita,nae amefariki usiku wa leo kwa changamoto ya kupumua.
 
Wewe hujawa na uhakika na chanzo chako cha habari.

Huna hata jina la hao marehemu.

Wote unasema mwenyewe kwamba ni wastaafu,ina maana ya uzee.
Wapi unapata nguvu ya kukimbilia JF kuleta ulojo badala ya habari ambayo ni CONTENT.

Kwa nini hukujiridhisha kwa kupata habari kamili kwanza?

HUU NDIO UMBEYA!
Nimeleta habari ambayo ni tetesi. Wenye habari kamili watatuhabarisha. Hii ni JF,tetesi nayo ni habari na inaruhusiwa.
 
Taarifa hizi nimezipata kwa rafiki wa karibu aliyeko SUA.

Sijawa na uhakika wa kutosha kuhusu chanzo hiki cha habari . Imenitia Uchungu kwa vile hawa walikuwa watu maarufu kitaaluma na waliotoa mchango kwa maendeleo ya uchumi nchini. Iweje taarifa zao zisisikike au kutangazwa na vyombo vikuu vya habari?

Ukishafariki hata kama ulikua na sifa gani, u sawa na mbuzi aliekufa porini tu.

Kwani akitangazwa ndio atafufuka, nashangaa sana watu wanaoweka ufahari makaburini kwenye mwili unaooza
 
Hii changamoto ya kupumua itakuwa inaendelea kutafuna taratibu hasa kwa wenye umri mkubwa, over 60 yrs...
 
Kama tunavyoshindwa kuchagua siku ya kuzaliwa, hatuwezi kuchagua siku ya kufa.
 
Ukishafariki hata kama ulikua na sifa gani, u sawa na mbuzi aliekufa porini tu.

Kwani akitangazwa ndio atafufuka, nashangaa sana watu wanaoweka ufahari makaburini kwenye mwili unaooza
Ni desturi yetu. Endapo Mangwea na Kanumba hadi Ikulu ilishiriki kuwaaga na hukutoa hoja kama hiyo ila kwa Profesa unaona kawaida! Ni nini kimetupata sisi Watz?
 
Inatamkwa imepungua sana haisemwi imekwisha na ndio sababu tunasisitizwa tuendelee kuchukua tahadhari
Korona ipo usidanganywe na wanasiasa kwamba imekwisha fuatilia taarifa za kimataifa ndio utajua kuwa Kumi na Kenda anazidi kupuyanga China wenyewe wameshapata maambukizi tena yaani FUTA limerudi CHINA.
 
Inatamkwa imepungua sana haisemwi imekwisha na ndio sababu tunasisitizwa tuendelee kuchukua tahadhari
Imepungua kutoka ngapi hadi ngapi? Watu hawapimwi lakini wanasema imepungua mara imekwisha mara tuna wagonjwa 66 yaani hawaeleweki.
 
Back
Top Bottom