Kwenye sherehe zilizohudhuliwa na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, askofu Shayo kwenye salamu zake kwa Rais wa Zanzibar amezungumzia mambo mbalimbali likiwemo la tatizo la wabara kumiliki ardhi Zanzibar.
ameongelea kuhusu aridhi ambapo ni tatizo kubwa Zanzibar, yaani mkristo kupata aridhi ni haiwezekani, hasa ukifahamika kutoka bara kama ni mkristo upewi.
Aliongeza kuwa "katiba inatoa nafasi kwa raia kuwa na usawa,haiwezekani ukienda bara unachukua aridhi ila ukija zanzibar upewi, ifike mahari tuangalia usawa, ukipenda kula vya mwenzako na wewe kubali kuliwa vyako".
Maoni ya ziada
Achilia mbali taasisi za Znzibar, yani hata kwa raia wa kawaida wa kizanzibar, ukienda dsm, kigamboni, kuna wazanzibar wanamiliki ardhi wapendavyo, ukienda mikoani kuna wazanzibar wananunua maeneo wapendavyo. ila sisi tukienda kule mhhhh, .......,
kwenye kuoa hapa napo huwa pana ubaguzi, yani ukifahamika ni mtu wa bara tu hapo sahau kupata binti, ila huku bara haya mambo hayapo.
kingine ni kila ramadan ikifika wakristo inabidi tujifungie vyumbani kupika na kula lasivyo utachapwa viboko kama mtoto mdogo ama kufungwa jela kwenye mateso makali mno....ni jambo ambalo linaumiza sana maana katiba ina uhuru wa imani ila nchi inaendeshwa utadhani ina katiba ya kidini.
kingine pia ni udhalilishaji wa wazi wazi, ni kawaida sana kusikia ukiitwa "kichogo" kisa tu ni mtu wa Tanganyika na kichwa chako hakipo flat kama wazanzibar wengi, nadhani hiki si kitu kigeni hata cheme kwa wale ambao awmejiunga ama wamewai kupiga chabo kwenye magrup ya kizanzibari ya fb na whatsapp.