Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Zanzibar ametimiza Jubilei ya miaka 25 katika utumishi wa kanisa la Roman Catholic huko Zanzibar.
Kwenye sherehe zilizohudhuliwa na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, askofu Shao kwenye salamu zake kwa Rais wa Zanzibar, amezungumzia mambo mbalimbali aliyokumbana nayo akiwa katika utumishi wa kanisa, moja au baadhi ni Usafirishaji haramu wa watu kwenda nje ya nchi na uhamiaji wanatumika kutoa pasipoti pasipo utaratibu.
Amesema watu wanasafirishwa nje kwa kuhadaiwa kazi nzuri lakini mbele wanabadilishiwa kile walichoahidiwa na kwenda kufuga nguruwe au kazi za hatari.
Kwa upande mwingine ameongelea kuhusu ardhi ambapo ni tatizo kubwa Zanzibar, yaani mkristo kupata ardhi ni haiwezekani, hasa ukifahamika kutoka bara kama Yohana hupewi.
"Siyo kila mkristo anakuja kujenga kanisa, kanisa halijengwi na familia bali na taasisi kama madhehebu", alisema askofu Shao.
Aliiomba Serikali ifikirie wanapopima viwanja waweke kipaumbele pia kwa mashirika na taasisi za kidini, sababu kanisa linatizama mbele na si kuwapa kiwanja size ya 20x20.
Aliongeza kuwa "Katiba inatoa nafasi kwa raia kuwa na usawa, haiwezekani ukienda bara unachukua ardhi ila ukija Zanzibar hupewi, ifike mahali tuangalie usawa, ukipenda kula vya mwenzako na wewe kubali kuliwa vyako".
MHASHAMU ASKOFU SHAO ANATAKA KUITEKA ZANZIBAR KWA JINA LA USAWA (RECIPROCITY) WA KUMIlIKI ARDHI.
Sasa hii ni hatari tena kubwa tena ilioekwa hadharani. Ni dalili ilio wazi ya kutapatapa na kumtisha hadharani Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi aridhie kile ambacho hakikuridhiwa na Maraisi wote wa Zanzibar waliopita.
Askofu Shao anaingiza hisia za kiroho ndani ya siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Zanzibar. Maudhui ya suala la ardhi ni suala la kisiasa na la Mamlaka Kamili ya Zanzibar na kwa hiyo lipo nje ya dini ya Ukristo na Uislamu.
Vipi utakuwepo usawa wa umiliki wa ardhi baina ya Wazanzibari milioni moja (1) na Watanganyika milioni arubaini na tano (45)?
Hii fitna mpya ya hadharani ya Askofu Shao imekusudiwa kujenga mifarakano ya kidini na ujinga wa kiitikadi baina ya dini mbili na pande mbili za Muungano ili Wazanzibari pamoja na Watanganyika wanaoidai Tanganyika yao, wapoteze Umoja wao katika kudai haki zao ndani ya Muungano.
Viongozi wa kidini na wa kisiasa wa Zanzibar na wa Tanganyika wanapaswa kuwa waangalifu imara na waangalifu SANA na kumshauri vizuri Rais wa Zanzibar. Dokta Hussein Ali Mwinyi, anatakiwa achukue tahadhari za makusudi za kuuona mtego wa Askofu Shai wa kujaribu kudhililishwa hadharani na mbele ya Wazanzibari ma Watanganyika, na kuiepusha Zanzibar na Tanganyika na mbegu za sumu mpya alizozimwaga Askofu Shao mchana kweupe kwenye uwanja wa Amani na mbele yako Rais Dokta Hussein Ali Mwinyi.
Watakaoumia katika jaribio la kupandisha mbegu za fujo za kisiasa kupitia udini wa Askofu Shao na jimbo la Katoliki la Zanzibar ni Wakristo na Waislam kwa pamoja.
Ni dhahir Askofu Shao na jimbo la Katoliki la Zanzibar anataka Watanganyika Wakristo (hakuwatetea Watanganyika Waislam) waruhusiwe kununua ardhi na nyumba Zanzibar kinyume na sheria za Zanzibar.
Askofu Shao katuamsha hadharani kwa kututangazia mkakati wa hatari mpya na mchafu. Sisi Wazanzibari, na zaidi Watanganyika wenye kuuona uovu wa Uongozi wa watu wachache wa Tanganyika juu ya Zanzibar, tutaendelea kufa kupona kudai Mamlaka Kamili (sovereignty) ya Zanzibar na Mamlaka Kamili ya Tanganyika (sovereignty) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.