James Comey
JF-Expert Member
- May 14, 2017
- 8,759
- 14,831
Hujui jinsi udokta unavyopatikana?Huyo Dr Kachumbari alipata wapi Huo u dk , Kivukoni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujui jinsi udokta unavyopatikana?Huyo Dr Kachumbari alipata wapi Huo u dk , Kivukoni?
Hujui jinsi udokta unavyopatikana?
Basi nasi huku Bara tuwawekee sheria hiyo hiyoHawakatai kutoa mkuu, tatizo lililopo ni jinsi wanavyoitoa, yaani mashariti kwa Mtanganyika ni magumu sawa na muwekezaji.
Kwa kifupi ukija Zanzibar hata kujenga nyumba unahesabika kuwa muwekezaji, -Hii ni kutoka kwa Dr. Hussein Mwingi.
But huko Tanganyika wao wananunua hata bila kuulizwa kitambulisho cha kupigia kura!.
mtaacha kutokujiamini hadi lini? mbona siku zote hamjiamini?mkoa wenyewe huo sijui wilaya, imejaa machoko tu.Huna unachojua kazi kuwaongopea machogo wenzako wa dot.com
Hiyo inayoitwa passport iliondolewa mwaka 1993 baada ya mtifuano wa kadhia ya OIC.
Rais wa Zanzibar wa wakati huo Dr.Salmin Amour alisema wazi kwenye hutoba yake kwamba wamekubali kuondoa hiyo kero ya Muungano pamoja na kujitoa kwenye OIC na kabla ya hapo kukubali kuanzisha vyama vingi kwa sababu ya kulinda Muungano.
Kero moja aliikataa wazi na hadharani ya kutakiwa kukubali Muungano wa Serikali 2 kuelekea 1 alisema hiyo labda waje watawale miti.
OIC ilijitoa kwa makubaliano kwamba Tanzania ndio ijiunge kwa sababu kikatiba Zanzibar haikuwa na sifa.
Hiyo kusema ukienda Zanzibar ilikuwa ni lazima kwa passport ila ukija Bara silazima ni uzushi uliotungwa sijui kwa maslahi ya nani.
Ukweli ni kwamba ilikuwa ukienda Zanzibar huku Bara huulizwi chochote, ukifika kule Zanzibar unaulizwa hati/kibali cha kusafiria ( hakukuwa na ulazima wa passport hata barua ya mjumbe wa nyumba kumi inatosha na ndio walio wengi walikuwa wanatumia hizi kwa huku Bara, kule Zanzibar walikuwa wanatoka Uhamiaji Ni karatasi ya ukurasa mmoja yenye heading ya "HATI YA KUSAFIRIA" ilikuwa ina muda wa matumizi ya miezi kati ya 6 na mwaka (wenye kukumbuka vizuri wanaweza kunisahihisha) wenye kujiweza na passport ndio walikuwa wanatumia hizo passport). Na ukitoka Zanzibar unaulizwa tena ukifika Bara huulizwi. Na hii ilikuwa inawahusu wote uwe Mzanzibari, Mzanzibara au Mtanganyika. Aliekuwa kwenye ulazima wa passport ni mgeni ambae si Mtanzania na walikuwa wanashangaa sana inakuwaje nchi moja lakini ukifika Zanzibar unadaiwa tena passport.
wala sio sheria, kuna siku mwendawazimu mmoja atakuja kuchukua nchi, watafurumushwa na kutembea kwa mguu hadi nungwi. ndio maana tunasemam tunahitaji muungano wa kuheshimiwana na wenye usawa kwenye kila kitu, ama la....,wao wanashangilia na kuita nchi ya upande mmoja ya kidini, kwingine wanakuja kuinjoi tu, wengine wapate ardhi na wengine wasipate, wengine waitwe chogo wengine wasiitwe. ni dhambi ya ubaguzi itawadhuru siku moja.Ni muda tanganyika itungwe sheria wale watu wa visiwani wairejeshe ardhi wanaomiliki bara na asiruhusiwe mtu wa visiwani kumiliki ardhi
Kwa kweli askofu Shao amekuwa jasiri sana, muwazi na amewafungua watu macho na akili, hongera sana askofu!MHASHAMU ASKOFU SHAO ANATAKA KUITEKA ZANZIBAR KWA JINA LA USAWA (RECIPROCITY) WA KUMIlIKI ARDHI.
Sasa hii ni hatari tena kubwa tena ilioekwa hadharani. Ni dalili ilio wazi ya kutapatapa na kumtisha hadharani Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi aridhie kile ambacho hakikuridhiwa na Maraisi wote wa Zanzibar waliopita.
Askofu Shao anaingiza hisia za kiroho ndani ya siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Zanzibar. Maudhui ya suala la ardhi ni suala la kisiasa na la Mamlaka Kamili ya Zanzibar na kwa hiyo lipo nje ya dini ya Ukristo na Uislamu.
Vipi utakuwepo usawa wa umiliki wa ardhi baina ya Wazanzibari milioni moja (1) na Watanganyika milioni arubaini na tano (45)?
Hii fitna mpya ya hadharani ya Askofu Shao imekusudiwa kujenga mifarakano ya kidini na ujinga wa kiitikadi baina ya dini mbili na pande mbili za Muungano ili Wazanzibari pamoja na Watanganyika wanaoidai Tanganyika yao, wapoteze Umoja wao katika kudai haki zao ndani ya Muungano.
Viongozi wa kidini na wa kisiasa wa Zanzibar na wa Tanganyika wanapaswa kuwa waangalifu imara na waangalifu SANA na kumshauri vizuri Rais wa Zanzibar. Dokta Hussein Ali Mwinyi, anatakiwa achukue tahadhari za makusudi za kuuona mtego wa Askofu Shai wa kujaribu kudhililishwa hadharani na mbele ya Wazanzibari ma Watanganyika, na kuiepusha Zanzibar na Tanganyika na mbegu za sumu mpya alizozimwaga Askofu Shao mchana kweupe kwenye uwanja wa Amani na mbele yako Rais Dokta Hussein Ali Mwinyi.
Watakaoumia katika jaribio la kupandisha mbegu za fujo za kisiasa kupitia udini wa Askofu Shao na jimbo la Katoliki la Zanzibar ni Wakristo na Waislam kwa pamoja.
Ni dhahir Askofu Shao na jimbo la Katoliki la Zanzibar anataka Watanganyika Wakristo (hakuwatetea Watanganyika Waislam) waruhusiwe kununua ardhi na nyumba Zanzibar kinyume na sheria za Zanzibar.
Askofu Shao katuamsha hadharani kwa kututangazia mkakati wa hatari mpya na mchafu. Sisi Wazanzibari, na zaidi Watanganyika wenye kuuona uovu wa Uongozi wa watu wachache wa Tanganyika juu ya Zanzibar, tutaendelea kufa kupona kudai Mamlaka Kamili (sovereignty) ya Zanzibar na Mamlaka Kamili ya Tanganyika (sovereignty) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ukipenda kula vya mwenzako na wewe kubali kuliwa vyako
Ikisha c watanunua uku baraWatanganyika wakiruhusiwa kununua ardhi Zanzibar si itaisha!!..Kuna ardhi kubwa bara,kimekushinda nini kununua mpaka uvuke maji!!?
Malizeni bara kwanzaIkisha c watanunua uku bara
Ikisha c watanunua uku bara
So wewe unaona sawa kwao kutupa ardhi kwa masharti wakati wakija hapa bara wanapewa tu ardhi kwa kuwa ni watanzania?Wee chogo ni simple kwa utashi wako lakini ktk makabrashi ya muungano ni pamoto.[emoji23][emoji23][emoji23]
Walipishwe tozo/kodi kama wawekezaji......wataachia tu na kurudi kwao kunywa kahawa na kashataMKuu wao wanamiliki ardhi kisheria, kuwanyang'anganya kwa nguvu ni kujitafutia matatizo.
Walipishwe tozo/kodi kama wawekezaji......wataachia tu na kurudi kwao kunywa kahawa na kashata
Fafanua.mtaacha kutokujiamini hadi lini? mbona siku zote hamjiamini?mkoa wenyewe huo sijui wilaya, imejaa machoko tu.
kwasababu huna akiliSioni motive ya kumiliki ardhi zanzibar