1. Bajeti ya SMZ ni Trillioni 2.5. Bajeti ya JMT ambayo ni Tanganyika ni Trilioni 41
Hivi Wazanzibar wanataka account ya pamoja ya nini? kujadli nini?
2. Makusanyo ya ZRB ni Bilioni 500, TRA ni Bilioni 400. Wazanzibar wanaosema TRA inakusanya na kuleta Bara, ni kiasi gani hicho? Bilioni 400 hazijafika hata nusu Trilioni. Bajeti inaonyesha pesa zote zinabaki Zanzibar
3. Bajeti ya SMZ haina Wizara ya Ulinzi, mambo ya ndani , nje au taasisi za muungano
Gharama hizo zipo katika bajeti ya JMT ambayo ni bajeti ya Tanganyika
4. Kuna eneo linaeleza pesa za mfumo wa elimu ya juu (HEET) ambapo JMT itagharamia Zanzibar Marine institute
Hivi Zanzibar si wana mfumo wao wa elimu ya juu na wizara zao kwanini pesa zitoke Tanganyika?
5. Bajeti ya SMZ haionyeshi wale Wabunge wa Zanzibar wanaokuja Dodoma kusikiliza habari za Tanganyika wanalipwaje. Maana yake gharama za Taasisi ya Bunge kwa Wabunge kutoka Zanzibar zinalipwa na Watanganyika
Ukisoma bajeti ya Zanzibar sehemu kubwa ni elimu , afya na kununua maboti na utalii
Bajeti haina vyanzo vingi vya kodi kwasababu maeneo yenye gharama kama kuendesha wizara na taasisi za muungano zinabebwa na Watanganyika.
Katika kuhakikisha Watanganyika hawabebeshwi kodi na tozo na katika kuongeza vyanzo vya mapato, njia moja ni kupunguza matumizi hapo ndipo Zanzibar inatakiwa ibebe gharama kama za taasisi kama Wabunge wao, ichangie taasisi za muungano na wizara husika.
Kwa kuwa na taasisi za JMT zenye mbadala kule Zanzibar, je, hiyo siyo duplication inayombebesha mlipa kodi gharama?
JokaKuu Pascal Mayalla