Suala la Bandari TEC hawakupata kama walivyozoea

Still bado jf mnampa credit huyu kichaa,lengo lake kubwa ni kutafuta mpasuko wa kidini nchini,yupo katika siku zake za mwisho hana cha kupoteza kazi yake ni kuona nchi hii inaingie katika mgogoro wa kivita baina ya waislam na wakristo.

Serikali iwe makini naye sana ikiwezekana hatua za msingi zichukuliwe dhidi ya huyu mfia dini gaidi.
 
Sina tatizo na Historia aliyoandika Mohamed, tungependa wengi wawasilishe ili tupate upana wa kuelewa.

Nina tatizo anapodai 'yakwake ni ya kweli haihitaji kuhojiwa. Nina tatizo anapofanya makosa yale yale ya Wandishi wa awali ya kuwa biased'' na hata kupotosha kwa makusudi au bahati mbaya.

Hapana Wachangiaji hawana tatizo, shida imeanza Mohamed kuwaondoa katika mada na kujadili yasiyokuwepo. Mfano, bandiko 56, nimejaribu kumrudisha katika mada lakini kwa makusudi au kutojua akaingiza mambo yasiyohusiana na mada. Nyerere na Mtikila wanaingiaji kwa Video aliyotuma Ansber Ngurumo? Pili, kwanini hamjibu mleta Video anamshambulia kama Taasisi. Je, naye kwa maoni yake ni ya Taasisi? Ni ipi hiyo.


Rudi usome kwa utulivu utagundua Mohamed amechangia kuwapoteza Wasomaji na Wachangiaji kwa kuwaondoa katika Mada aliyoleta.

Hili si jambo geni kwa baadhi yetu, Mo anaposhindwa kukabiliana na hoja hiyo ni staili yake, mapicha n.k.
Mwenyewe anaita mkando kando ya mjadala bila kujua ni kuwapoteza Wasomaji

Zawadi Ngoda , nimemuuliza Mohamed kwa wema , kwamba, amefanya kazi Bandari ingalikuwa jambo jema angeonyesha wanaopinga Mkataba wa DP wanakosea wapi au Uzuri wa Mkataba upo wapi. Mohamed hakufanya bali kutupa lawama zisizo na msingi kwasababu hoja inajengwa juu ya 'facts'. Hana!

Pili, amedai Chadema walishirikiana na TEC kupinga Mkataba. Nilimuuliza Vipi ACT Wazalendo na CUF ya Prof Lipumba? Mbona nao walipinga, je waliungana na TEC? Hakujibu akaamua kumfuata Mtikila Kaburini.

Tatu, akasema Waislam waligundua hila hawakuungana nao ! Nimemuuliza, si waliungana na CCM! ni kwa mahaba gani na ya lini Waislam hawa hawa wenye malalamiko mengine hayajajibiwa na serikali ya CCM, leo waungane na Watesi wao wa miaka 60! Kulikoni. Mohamed hakujibu akaamua kumfuata Nyerere Kaburini.

Mo akaingiza Uarabu na DP. nikamuuliza kwani Uarabu ni Tusi? Mbona tuna Wazungu!

Kwa hayo machache nilijaribu kumrudisha katika madaasimamie anachoamini , haikufanikiwa kwasababu ku-focus si utamaduni wa majadiliano wa Mohamed, ata 'dance' kila mahali na kila 'tune'

Binafsi sikuona busara kumshauri afute bandiko. Haya ni maoni yangu.
Nilimshauri afute bandiko kwa kuchelea kwamba hoja ni nyepesi na hata kama ni nzito hazina mashiko na hataweza kuzitetea au kuzijadili. Nilimshauri, lakini pia nikakiri kwamba ana uhuru wa kutoa maoni.
Ushauri si shurti ni hisani tu, kuukubali au kuukataa si tatizo
 
Ndivyo ilivyoandika biblia ?
 
Wewe tunakuelewa ulitaka lisifiwe kanisa tu
 
Nguruvi3,
Sijapata kulazimisha kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika niliyoandika mimi kila mtu aikubali.

Uwezo huu mimi nitautoa wapi?

Nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes na nimeeleza vipi African Association ilivyoundwa na nimeweka majina ya waasisi wake.

Nikaeleza historia nzima.

Sina haja ya kurudia yale ambayo hakuna aliyekuwa akiyajua hadi nilipoyaeleza.

Wasomaji wamepokea kitabu hiki vizuri kupita mategemeo yangu.

Mfano ndiyo huu hapa JF tunakijadili kitabu hiki toka 2008 na nikapewa tuzo mara mbili ya Mwandishi Bora wa Historia.

Halikadhalika Waislam wamenipa tuzo mara mbili pia.

Wanahistoria bobezi wa African History wakafanya pitio mara tatu na kuchapwa katika Cambridge Journalists of African History.

Nikatiwa katika miradi minne ya kuandika historia, mradi wa Harvard na Oxford University Press New York, Mradi wa Oxford University Press Nairobi, mradi wa kuandika historia ya Julius Nyerere na mradi wa historia mpya ya Tanganyika ulioletwa na Rais Magufuli.

Miradi yote hiyo utanisoma ila wa Magufuli huu haukuchapwa.

Sijawalazimisha hawa wote kuniingiza katika miradi yao.

Huu ndiyo ukweli.
La haukupendezi hakuna tatizo.
 
Sasa naamini hata wapumbavu mnazeeka ..... Sio kila Mzee ana hekima ...wewe ni mpumbavu ....kila Andiko lako ni udiniudini udini ....
Uzuri MO hata ukimkejeli, yeye anakurudisha ktk hoja. Huu ndio uungwana. Ni shule kubwa sana hii, sote tujifunze toka kwake.
Shauri wa bure kwako Mtoto wa Inzi: kutukana kunakupunguzia hekima yako, ni busarna kutumia lugha mbadala hata kama hukubaliani kabisa na hoja mwenzako.
 
Zawadi..
Mimi nimesomeshwa mlango wa mnakasha yaani mjadala katika madrasa na mwalimu wangu Sheikh Haruna.

Kanifunza saikolojia na adabu ya mjadala.

Akisisitiza kuwa ingia katika mjadala kwa heshima na adabu na kwa nia ya kufundisha na wewe kujifunza kutoka kwa wenzako.

Akitufunza mwalimu wetu kuwa tusijibu matusi na kejeli kwani atukanae na kukejeli tayari keshashindwa.

Mwenyewe akipenda kusema usimpige mijeledi punda aliyeanguka chini.
 
Naam, mie ni mfuasi wa ilmu yako ya history ya Tanganyika
Tresor...
Ndugu yangu sote hapa tunajifunza.
Mimi ilm hii si kwa kuwa labda nimesoma sana la hasha.

Nimeijua historia hii kwa kuwa ni historia ya wazee wangu.

Wao ndiyo walioasisi harakati hizi za kupigania uhuru wa Tanganyika wakianza na African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, TAA na TANU.

Wao ndiyo waliompokea Mwalimu Nyerere Dar es Salaam wakawa na yeye hadi uhuru umepatikana.

Sababu ni hii tu.

Mimi nina mengi pia ya kujifunza kwa wengine kwani huko kwao walikuwapo wazee wao na huenda na wao waliwaona katika harakati mfano wa hizi.
 
Mzee wangu nikukumbushe ila sijui kama utanikumbuka niliwahi kufika kwako pale magomeni tukafanya maongezi nilipata 'ilmu' kubwa sana.. nakumbuka moja ya story ulitupatia ni ya Mzee wangu Kitwana Kondo kuwa alienda Nje kusomea "strategic " hahahaha hivyo mie ni kijana wako kabisa niko hapa kujifunza ilmu ya history ya Tanganyika na huwa naitumia ktk maongezi yangu na kukutolea mifano .
 
Tresor...
Hapana sikumbuki.
Ulikuja kunirekodi au tulizungumza tu kama mgeni wa kawada?


2012

 

Muungano uliasisiwa kwa hiari , Msikilize mkristo mwenzako anavyokuambia



View: https://www.youtube.com/watch?v=hsNMiqFLPVU


View: https://www.youtube.com/watch?v=kvN0jG_1QJc
 
Mohamed, sijasema umelazimisha. Nilichosema ni kauli yako ya '' Historia ya Kweli'' uliyoandika. Kumbu kumbu zipo
Sikubaliani na hilo kwamba wewe una 'monopoly' ya ukweli hasa nikiangalia matundu katika historia yako.
Hayo mengine uliyoandika hayanishwishi lakini tunashukuru tumeelewa unakubalika wapi.

Turudi kwenye mada
1. Kwani uarabu ni tusi?
2. Hawa wanaopinga Mkataba wa DP wanakosea wapi? Ukiwa mstaafu wa Bandari ni wapi uzuri wa mkataba wa DP
3. ACT Wazalendo na CUF walipinga mkataba , je nao ni 'washirika wa TEC' kama ulivyosema kuhusu Chadema?
4. Lini CCM imekuwa na uzuri na Waislam, na je hoja zimejibiwa na Serikali ya CCM? Madhila ya miaka 60 yameisha?
5. Huyo mleta mada umemhusisha na TEC kwa maoni yake, wewe unahusishwa na Waislam. Hili ni sawa?
 
Aisee... Nilikuona kupitia tv kumbe wewe ni ntu mzima vizuri tu tatizo una utoto mwingi uliojificha kwenye chuki za kiimani. Wewe mzee ni mdini waziwazi. Shida sana
🚮🚮🚮
 
Nguruvi3,
Huwa wakati mwingine nasali misikiti ya pembezoni sana na huamini hakuna anaenifahamu hapo.

Ghafla mwisho wa sala Imam anatangaza, "Ndugu zangu Waislam ndugu yetu Mohamed Said tunae humu ndani namuomba asimame awasalimu nduguze."

Machozi hunilenga.
Hii ndiyo nafasi yangu kwa Waislam.
 
Aisee... Nilikuona kupitia tv kumbe wewe ni ntu mzima vizuri tu tatizo una utoto mwingi uliojificha kwenye chuki za kiimani. Wewe mzee ni mdini waziwazi. Shida sana
🚮🚮🚮
Raia...
Umechelewa kuniona.

Mimi mwezi huu nafikisha miaka 72.

Mimi ni mzee.

Niko JF toka 2008 kwa jina langu halisi na kwa picha.

Nashangaa hujaniona.

Ningekuwa na chuki singeweza kuwagusa wachapaji vitabu, media, vyuo vikuu na watu wa kawaida.

Nimeandika mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika kama "field of enquiry."

Kitabu kimevutia wengi sana na mazungumzo yangu katika historia hii yamekuwa mashuhuri.

Hakuna udini hapo.
 
Kinj...
Tatizo la bandari kupewa Waarabu TEC na CHADEMA walisimama upande mmoja.

Sasa si mimi ndiye niliowaunganisha.

Hili la udini angalia wewe mwenyewe na fanya utafiti utajua.
Yaani unataka CHADEMA waruhusu tu bandari apewe Muarabu kirahisi hivyo ata kama mikataba ni ya ovyo,kisa Kuna maslahi ya Mwarabu ambaye ndie mwenye uislam wake ili kuwavutia Waislamu waipende Chadema??.......Hicho kitakuwa sio Chama cha siasa,bali ni taasisi ya dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…