kwamwewe
JF-Expert Member
- Jul 15, 2010
- 1,908
- 604
Amewagonga ndipo mumeingia Kama hamna akili vizuri , mumechanganyikiwa😝😝😝😝Hekaya za Mohamed Said
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amewagonga ndipo mumeingia Kama hamna akili vizuri , mumechanganyikiwa😝😝😝😝Hekaya za Mohamed Said
Yuko obsessed sana na udini mpaka aibu, maana hata busara za kawaida tu zinazotakiwa kwa mtu mwenye umri wake, hakuna, ni upumbavu mtupu😂😂ila hili lizee linapitia kipindi kigumu sana....yaan jambo la kawaida kabisa atalitafutia mtazamo wa kidini lionekane kama Kuna competition flan hv ya waislamu na wakristo...
Watu wanalumbana vipengele vya kimkataba yeye anaangalia how to "dinilise"😂Yuko obsessed sana na udini mpaka aibu, maana hata busara za kawaida tu zinazotakiwa kwa mtu mwenye umri wake, hakuna, ni upumbavu mtupu
Kimsingi ilitakiwa iwe hivyo, lakini kwa bahati mbaya historia nyingi zimeandikwa kimaslahi. Nitakupa mifano michache tu.Ni kweli unayosema na kwa kuongezea tu Historia haiandikwi bali inawasilishwa. Historia hujiandika yenyewe sisi wanadamu tunainukuu nakuiwakilisha kama ilivyotokea na si kama tunavyodhani
Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa bahati mbaya wachangiaji ndio wamevutika huko. Pengine ungemshauri abadili kichwa cha habari. Kwa sababu kwa ajenda 1,2 na 3 ni pana sana na ni vigumu kwa wachangiaji kuelewa wajikite kwa Chadema/uislam/ukatoliki au Uarabu na DP N.K.Pili, mada si Historia bali yatokanayo na video ya Ansbert Ngurumo ambayo Mohamed ameiweka mwenyewe
Badala ya kujenga hoja, kutetea hoja au kubomoa hoja kwa kutumia Video katika haya hapa chini ameingia kwingine. Hoja ni hizi
1. Ziara ya Rais Vatcan
2. Uarabu na DP
3 Chadema na Ukatoliki, Waislam na CCM
Kinachoshangaza ni kusikia Nyerere, Mtikila , Mwinyi, Mabucha ya Nguruwe, Abdul Sykes n.k. vikitawala mjadala bada ya hoja alizoleta mwenyewe. Sijui kwa wengine mlisoma , kwasisi wenye elimu ya kubabaisha hili linatupoteza, tunashindwa kujua mjadala unahusu nini
HahahahahahaChifu...
Ahsante sana ndugu yangu.
Nimeweka makala hiyo hapo juu labda huenda ndugu zetu wakakaa kitako na kutafakari.
Kuna watu hapa wananitukana na wanapandisha hamaki na kuropoka ovyo wenyewe huandika 'hovyo.''
Angalia picha hii ambayo nayo sitaweka maelezo:
View attachment 2881687
1955/56
Ngumu kupona hilo tatizoDah huyu mzee nadhani anasumbuliwa na tatizo lilelile... ni vizuri akawaona madaktari bingwa pale hospitali karibu na gereza kuu dodoma wakamsaidia tatizo lake
Nan...Hekaya za Mohamed Said
Tresor...Ngumu kupona hilo tatizo
Ndio maana ni ngumu hii kitu kukutoka kichwani kila uonapo au kusikia hayo we unaghadhibika kw ulaghai huoTresor...
Kila miaka inaposonga mbele katika kujadili suala la historia ya uhuru wa Tanganyika yanakuja mambo mapya.
Binafsi mambo haya yananifurahisha sana.
Kwanza siamini kama kwa dhati ya nafsi zao wanaamini wanachosema.
Nikifika hapa najiuliza sasa ikiwa hivi kwa nini wameona waseme kuwa nina tatizo la upungufu wa akili?
Nikiwa hapa akili yangu sasa inaniambia mimi hawa wenye fikra hii ya kuniona mimi nina tatizo la akili wao bongo zao ziko sawa?
Wanaweza kusimama na mimi, ''toe to toe'' katika uwezo wa matumizi ya akili zetu zao na zangu?
Nani ataibuka mshindi?
Au ni yale ya akutukanae akuchagulii tusi na mdomo haumkatai bwana wake?
Zawadi...Kimsingi ilitakiwa iwe hivyo, lakini kwa bahati mbaya historia nyingi zimeandikwa kimaslahi. Nitakupa mifano michache tu.
Hivi unaamini kuwa katika historia tulikuwa tunasoma kuwa ZIWA VIKTORIA, TANGANYIKA nk yaligunduliwa na wazungu...... Licha ya kukuta watu katika maeneo hayo wakiishi na kuvua samaki. Hali kadhalika mlima Kilimanjaro...na ....na...na.
Unajua kuwa katika vitabu vya historia vya Afrika Kusini wakati wa utawala wa wazungu kabla ya Mandela kuingia madarakani: Viliandika kuwa Watu wote Afrika ya kusini ni wahamiaji.......(sasa imefutwa)- Hii iliwekwa kwa lengo maalum, kuwa Afrika kusini hakuna wazawa (native). Hali kadhalika huko Australia.....
Ndugu yangu, Historia ndio mahali pekee kwa watawala husika kuelekeza matakwa yao na kuyarudia mara milioni mpaka mkaamini hivyo. Sijasema ya ziwa Nyasa au Ziwa Malawi. Niishie hapo.
Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa bahati mbaya wachangiaji ndio wamevutika huko. Pengine ungemshauri abadili kichwa cha habari. Kwa sababu kwa ajenda 1,2 na 3 ni pana sana na ni vigumu kwa wachangiaji kuelewa wajikite kwa Chadema/uislam/ukatoliki au Uarabu na DP N.K.
Binafsi sikuona busara kumshauri afute bandiko. Haya ni maoni yangu.
Tresor...Ndio maana ni ngumu hii kitu kukutoka kichwani kila uonapo au kusikia hayo we unaghadhibika kw ulaghai huo
Uzuri nimekua nakusoma kila bandiko nani mpz wa hizi history zako ILA KUJA KUWA UNAVYOTAKA NDIO KUGUMU
Sawa Mzee wangu..endelea kutupatia history ya TanganyikaTrevor...
Sijapatapo kughadhibika.
Pitia post zote tazama nani anatukana na nani anakejeli na nani anaweka vitisho.
Tresor...Sawa Mzee wangu..endelea kutupatia history ya Tanganyika
Jaribu kuwaza nje ya box. Muungano uliasisiwa na watu kwa hiari yao. Na jambo likishakubaliwa na wengi kiimani ni mpango wa Mungu. Je, wewe ulitaka Askofu Pengo achochee watu kanisani wapinge muungano? Kuutaka muungano au kutoutaka ni jambo la kisiasa na si jambo linaloshughulikiwa na Kanisa.Kwani kwenye Biblia imeandikwa mungu aliwaambia wakristo walinde muungano ?? Huu muungano si wa hiari ?? Wazanzibari wakati wote wanasema hawautaki muungano , kwa nini yeye atake kuulinda tena na kumhusisha Mungu ??
Mohammed, unajitahidi sana kuandika, hakuna anaekataa hao akina mama kumsindikiza Nyerere uwanja wa ndege siku anaenda UNO kwa mara ya kwanza. Ndiyo walimsindiki so what? Kipi cha kujifunza ktk usindikizaji wao huo? Swala hapa je, hao akina mama walimsindikiza kwasababu ya uanchama wao ndani ya TANU au kwasababu ya Uislam wao? Ukitofautisha haya mambo mawili Sheikh utakuwa kwenye mstari.Nan...
Hakika ni Hekaya za Abunwas.
Nakuelewa kwa nini akili yako inakataa kuamini kama hii ni kweli.
Hata picha unaziona lakini huamini.
Wale walioamini historia hii kwangu walikuja na maswali mengi ya kutaka kujua zaidi historia hii.
Wananiuliza imekuwaje hao akina mama wanne na mabaibui na huyo msichana wakamsindikiza Mwalimu Nyerere Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Mwalimu UNO?
Dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Picha hiyo yuko Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed,
Nawaeleza kuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mke wa Shariff Abdallah Omar Attas na huyu Shariff Attas kajuana na Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwani wote wakifanya kazi Kariakoo Market.
Abdul akiwa Market Master na Shariff Attas Mkusanyaji wa Ushuru wa Nafaka hapo sokoni.
Hawa walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU na Bi. Chiku yeye ndiye alikuwa akiwakusanya na kuwahamasisha wanawake kujiunga na TANU na kuhudhuria mikutano ya TANU Mnazi Mmoja kuujaza uwanja na kutia nderemo.
Watoto wawili wa Bi. Chiku, Sakina na Fatina bint Arab walikuwa walimu wakifundisha Al Jamiatul Islamiyya Muslim School.
Hawa mimi ni shangazi zangu si kwa nasaba bali kwa ujamaa kwani kaka yao Mustafa alikuwa rafiki wa baba yangu.
Huyu Mustafa alimuoa mtoto wa Max Mbwana ambae yuko kwenye picha ya tatu na Nyerere pamoja na Mwinjuma Mwinyikambi na Mshume Kiyate.
Bi. Tatu bint Mzee yeye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU Mwenyekiti akiwa Clement Mohamed Mtamila.
Siku hizo TANU katiba yake ilikuwa na nafasi ya Mwenyekiti na Rais.
Bi. Tatu bint Mzee alihudhuria kikao cha kujadili barua ya Mwalimu Nyerere alioandikiwa na Wamishionari wakimtaka achague moja katika mawili, ualimu au siasa.
Hii ilikuwa baada ya kurejea kutoka UNO.
Prof. Haroub Othman alikutana na Mwalimu baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes na akamsihi aandike historia yake kwani historia ambayo ndiyo hii hapa naieleza imegeuza si historia ya uhuru wa Tanganyika bali hata historia yake Mwalimu.
Ndugu yangu unaghadhibishwa na historia hii ya wazee wangu ambao wewe huwajui mimi ndiyo nawajua na Mwalimu anawajua na ushahidi ni hizo picha unaiita historia hii hekaya.
Hivi ndivyo inavyokuwa ninapoisomesha historia hii kwa wanafunzi wengine wao wanakuwa na maswali ya kutaka kujua zaidi.
Nyinyi historia hii inawaudhi mnatamani kama nisingeiandika Tanganyika ikabaki kuwa nchi isiyo na historia yake ya wapigania uhuru.
Mwanzoni nilikuwa napinga watu walivyokuwa wanakusema wewe ni mdini ... Haunaga mada Wala Chochote zaidi ya udini ... pathetic
Anachojaribu kukifanya huyu msemaji ni kutaka wasiokuwa Wakatoliki waamini kuwa Kanisa Katoliki bado lina nguvu ile ile iliyokuwanayo kabla ya sakata la "Waarabu" na Bandari ya Dar-es-Salaam.
Kanisa Katoliki katika sakata hili halikupata kile ambacho wamezoea kupata kuanzia wakati wa ukoloni hadi kufikia hili la bandari kupewa "Waarabu," katika Tanganyika huru.
TEC imefedheheka na hili limewaumiza na kwa mara ya kwanza wameshindwa kupata walichotaka kama ilivyokuwa mazoea.
Hawa walikuwa wakikataa kitu basi hakipiti.
Hawakuitaka EAMWS.
Hawakuitaka OIC.
Hawakuitaka Mahakama ya Kadhi.
Hili la bandari hawakulitaka kama ilivyo kawaida.
Wameshindwa safari hii kwa mara ya kwanza.
"Waarabu" wamekabidhiwa bandari.
Imekuwaje kwa TEC kushindwa?
Imeshindwa kwa sababu kuu moja ingawa zipo nyingi.
Hapa nitaeleza hii sababu moja kuu.
Waislam katika sakata la bandari walijikusanya pamoja na kujiweka mbali sana na wale ambao kila wamuonapo "Mwarabu" wao wanauona Uislam ambao lazima upigwe vita kwa hali yoyote ile.
Lakini kulikuwa na kitu kilichoongeza ladha katika kachumbari iliyokuwa ikitengenezwa na TEC.
Waliokuwa wanapinga Waarabu kuendesha bandari walikuwa wa imani moja na pamoja na CHADEMA.
Mifano iko mingi lakini hapana haja kueleza yote hapa.
Waislam kimya kimya wakaiunganisha CHADEMA katika orodha yao.
Chama hiki kikawekwa kundi moja na TEC na hii haikuwa kazi kubwa ya kumtoa mtu jasho la kwapa.
Ndani ya serikali na CCM kuna watu waliona mapema kabisa asubuhi kuwa nchi imeshagawanyika mapande mawili katika misingi ya imani.
Walio ndani ya serikali na CCM iliwadhihirikia kuwa Waislam wamejitenga wako mbali na wanaowapiga vita "Waarabu" na kwa mara ya kwanza kwa namna ya ajabu kabisa Waislam wakawa wanasubiri muda uwadie wapambane na TEC na mwenza wake CHADEMA.
Zikavuja taarifa kuwa Waislam nje ya BAKWATA wanajiandaa kwenda mahakamani kuhoji mengi yanayowasibu ndani ya serikali.
Waliokuwa serikalini na CCM walitambua watuhumiwa watakuwa nani.
Wenye akili zilizotimia ndani ya serikali na CCM haraka wakajiuliza tumefikaje hapa?
Hawa Waswahili si ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana?
Wenye akili timamu wakatambua vipi wamefika hapo.
Waingereza wana msemo, "You do it once too often."
Wakatoliki wamejidekeza kupita kiasi kwa kuhodhi kila kitu kuanzia serikali yenyewe, bunge, vyama vya siasa na kila kitu bila ya kukutana na kizingiti chochote.
Waislam wako nje na katika hili la "Waarabu," na bandari wamejiweka pembeni makusudi ili Ukristo ndani ya Tanzania ujivue nguo wenyewe hadharani.
Wametishika na wakarudi nyuma.
Hatari iliyokuwa inawakabili waliitambua.
Serikali ikatimiza maamuzi yake.
Taifa likabakia limetulia.
Kanisa likabakia limefedheheka.
Ile nguvu waliyodhani bado TEC inayo kumbe haipo tena.
TEC bila shaka imejiuliza baada ya haya nini kitafuatia?
Sababu ya kushindwa kwao wanaijua fika.
Sasa msemaji anasema Vatican siyo iliyomwalika Rais wa Tanzania bali serikali imeombwa ialikwe Vatican.
Nani mwenye kawaida ya kuongopa?
Kinachotafutwa hapa ni kujaribu kujifuta tope baada ya kuanguka.
Inataka ieleweke kuwa Rais wa Tanzania ana hofu na amejisalimisha Vatican.
Msemaji ananadi kuwa Kanisa Katoliki lina nguvu si watu wa kupuuzwa.
Ukweli ni kuwa hakika Kanisa limehodhi serikali kwa uwiano wa 80% kwa 20%.
Hali hii leo si mtaji tena kwao kwa sababu zilizo wazi kwani mengi yasiyopendeza yanaelezwa dhidi ya Kanisa na hatari yake ishajitokeza.
TEC imedhoofika bila yenyewe kutambua.
Hii ndiyo sababu ya TEC na CHADEMA kujikuta wako peke yao katika sakata la bandari na vita yao dhidi ya "Waarabu."
Iwe iwavyo hali ya siasa imebadilika.
Hizi propaganda kuwa Rais wa Tanzania ana hofu hazitasaidia kitu.
Zinaweza zikaamsha makubwa ambayo hawayategemei.
Zinaweza hizi propaganda pengine zikazua makubwa kuliko ule ukimya walioonesha Waislam wakati wa sakata la bandari.
Wasisahau ukimya mwingi una kishindo.
Sasa naamini hata wapumbavu mnazeeka ..... Sio kila Mzee ana hekima ...wewe ni mpumbavu ....kila Andiko lako ni udiniudini udini ....Petrol,
Misingi ya umoja iliwekwa tokea mapema wakati wazee wetu hapa Dar es Salaam mwaka wa 1929 wanaunda African Association.
Waasisi walikuwa hawa: Cecil Matola (President), Kleist Abdallah Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Rawkes Kusi na Rawson Watts.
AA ikawa imetawaliwa na Waislam na wakawa wanapitisha baadhi ya matatizo yao katika AA.
Wazee wetu wakaona hii haifai kwani walataka AA kiwe chama kisichofungamana na imani za wanachama wao.
Wakaamua mwaka wa 1933 kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) President akiwa Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Abdallah Sykes ili mashauri ya Waislam yapitishwe huko.
Sasa mwaka wa 1950 harakati za kutaka kuunda chama cha siasa.
Msimamo wa Hamza Mwapachu ulikuwa nafasi ya President wa chama hicho awe Mkristo ili chama kichukue sura ya umoja wa Watanganyika wote.
Wakati ule TAA ili ilikuwa imeshikwa na Waislam na Wengine walikuwa wachache sana katika siasa kwa kuwa Kanisa lilijiweka mbali sana na harakati za ukombozi wa Tanganyika.
Historia hii nimeieleza mara nyingi sana hapa.
Hivi ndivyo Julius Nyerere alivyochaguliwa kuwa President wa TAA mwaka wa 1953 katika uchaguzi ulifanyika Arnautoglo Hall Julius Nyerere na Abdul Sykes wakigombea nafasi hiyo.
Hii ni katika historia muhimu ya TANU ambayo Nyerere hakupata kuieleza na matokeo yake ikawa haifahamiki hadi pale kilipochapwa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes (1997).
TANU ikaingia kupigania uhuru wa Tanganyika Nyerere akiwa kiongozi wa harakati hizi na nchi ikawa imeshikamana.
Ushahidi ni picha za kupigania uhuru.
Picha zote Nyerere kazungukwa na Waislam wake kwa waume.
Uhuru ukapatikana mwaka wa 1961 nchi ikiwa na umoja.
Nani aliyekuja kutugawa na kuuvunja umoja huu?
Ndugu yangu Petrol,
Unalo jibu?
Unamjua adui huyu?
Angalia picha hizo hapo chini na kwa makusudi sitaweka maelezo ila mwaka wa picha kwani picha zinajieleza zenyewe:
Mbussi,Mohammed, unajitahidi sana kuandika, hakuna anaekataa hao akina mama kumsindikiza Nyerere uwanja wa ndege siku anaenda UNO kwa mara ya kwanza. Ndiyo walimsindiki so what? Kipi cha kujifunza ktk usindikizaji wao huo? Swala hapa je, hao akina mama walimsindikiza kwasababu ya uanchama wao ndani ya TANU au kwasababu ya Uislam wao? Ukitofautisha haya mambo mawili Sheikh utakuwa kwenye mstari.
Mtoto...Mwanzoni nilikuwa napinga watu walivyokuwa wanakusema wewe ni mdini ... Haunaga mada Wala Chochote zaidi ya udini ... pathetic