Mbussi,
Kuna picha maarufu ya Nyerere na Baraza la Wazee wa TANU.
Picha hii haikuwapo popote.
Picha hii aliipata kwangu na akaipenda na ndiyo sababu ya yeye kuniomba nimtafutie picha ya Nyerere na Maaskofu.
Mimi humtania namwambia labda nikupe ya kuchora.
Najua anajua hii picha ya Nyerere na Maaskofu haipo lakini hupenda kunicheza shere.
Wala si suala la unafiki bali maskhara kati ya marafiki wawili.
Ukweli ni kuwa Waislam mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika ni wa pekee sana.
Hii ndiyo sababu iliyonisukuma mimi kuandika historia hii.
Huu si udini.
Mchango wa Wakikuyu na Mau Mau katika kupigania uhuru wa Kenya ni wa pekee.
Kuandika historia ya Wakikuyu na mchango wao katika uhuru wa Kenya si ukabila.
View attachment 2888466