Suala la dini litanikosesha ndoa. Naombeni ushauri

Ndugu msikilize, mama yako, unaweza kulazimisha kuoa vyovyote, na mama yako hasifike kwako utajisikiaje?Usifanye ligi na mama yako, we ongea naye kiupole tu, tutakushauri sisi wanazengo we funga ndoa upendavyo baadaye yatakayotokea sisi hatupo.
 
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM.
Ulivyosema tu mwanachama wa CCM sikuendelea hata kusoma. Sinaga Utaratibu wa kuwasaidia chochote watu wa hiki chama japo hata ushauri tu.

Sana sana nikiweza sana basi ushauri wa kuwaingiza mkenge
 
Punguza chuki
 
Ila miccm bwana ni janga kwa hili taifa. No wonder!!!!
 
Ulivyosema tu mwanachama wa CCM sikuendelea hata kusoma. Sinaga Utaratibu wa kuwasaidia chochote watu wa hiki chama japo hata ushauri tu.

Sana sana nikiweza sana basi ushauri wa kuwaingiza mkenge
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.

Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.

Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.

Nishaurini wakuu.
Duuuu 37 uko mbali sana
Nimeoa nikiwa na 10 years ago mkuu

And bado anasema wewe ni mdogo

Duuu

Nashaurii usigombane na wazazi hata siku moja ongea na mpenzi wako mfunge ndoa SDA

Baada ya hapo mpeleke familia yenu mnakotakaa kiroho

Umri uliofika sio wa kusema nisubiri watoto wako unatakiwa uwalee ukiwa kijana mwenye nguvuu Nguvu Zako zinaenda kukataa mkuu.
 
Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.

Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.

Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.

Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.

Nishaurini wakuu.
Ongea na mzee...mbona Mimi naona easy wote nyinyi ni wakristo...Mimi sioni shida...
 
Back
Top Bottom