Ni kama useme watu wanaogopa kufa. Si kweli ila wanahofu ya namna watakufa na wakifa watakwenda wapi ila sio kufa. Sababu kufa ni process ya maisha.
Tukirudi kwenye mada yako. Si kweli kuwa wanaume wanaogopa au tutumie neno hawapo intimidated na wanawake waliokwenda shule. Hiyo si kweli.
Wanaume huwa wanachukua tahadhari dhidi ya matokeo ya kuwa na mwanamke aliyekwenda shule sababu wengi wao ni uhakika wakishaingia kimahusiano huwa na mushkeli wa kimaadili au tabia.
Yaani mwanamke ambaye amekwenda shule tayari anakuwa hana ukamilifu wa tabia za kike ambazo mwanaume anahitaji na hii itapelekea uhakika wa uhusiano kuwa wa mashaka au kufeli siku za baadae huko mbeleni.
Mwanamke aliyesoma huwa ametumia miaka mingi darasani na mashuleni kuandaliwa kuwa mtaalamu au mweledi wa taaluma na kazi fulani ila anakuwa na muda mchache sana wa kujifunza majukumu ya mke na pia kujiandaa kumtumikia, kuishi, kushirikiana, kumsapiti na kujitoa kwa mwanaume wake wa ndoa.
Pia katika hizi safari za kitaaluma mazingira anayopitia hayamruhusu kuwa mwaminifu kwasababu anakuwa hana tena ile female Innocence sababu ya kukaa na jinsia ya kiume na kuzoeana nayo so ni ngumu kumheshimu mume wake kama mwanaume pekee.
Mwanamke aliyesoma akimaliza shule akili yake inakuwa programmed kutafuta ajira na kuwa chini ya kampuni au taasisi na kutii amri na sheria anazopangiwa jambo ambalo litamuwia vigumu kumudu kutii maelekezo, ushauri, maagizo na amri kutoka kwa mume wake wa ndoa. Ni ngumu kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati m'moja lazima m'moja atadharauliwa na mwingine kuwekwa juu.
Though wapo mabinti wa kike ambao ni wasomi, wameajiriwa, na wameolewa na kuweza kumudu ndoa, kutii mume na kutekeleza majukumu na kumuweka mume mbele kabla ya ajira na kujua kubalance attention. Hawa wapo ila very rare. Majority hawawezi kujigawa hata kidogo akiweka akili kazini ni kazini tu mume wake akilalamika anaona kama anaonewa au kulazimishwa mambo ambayo yapo nje ya iwezo wake.
So kama mwanaume unajua cha kufanya na kama mtoto wa kike chagua lililobora kwako.
Sent using
Jamii Forums mobile app