Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Napata wasiwasi kama hili jipu la Lugumi litaweza kutumbuliwa kwa kawaida ya Mh Rais Magufuli hili lilikuwa ndicho kipa umbele cha kwanza ila naona kakaa kimya sasa sijui nini ukiona hata Mh Supika kanawa ujue iko namna ogopa.
 
Mh Magufuli kaz anayo'Hii nchi labda malaika ndio ataiweza watu hawana wema
 
Rais Magufuli hawezi kutumbua jipu la Lugumi linalomgusa Charles Kitwanga kipenzi chake. Mind U, Kitwanga wakati wa kampeni za CCM 2015 alikuwa akisema wazi bila kuficha kuwa yeye ndiye Waziri wa Mambo ya Ndani wa Magufuli na ikaja kuwa hivyo baada ya Patrick yule bosi wa Tanroad naye kipenzi chake kukataa uteuzi wa ubunge then waziri, wizara ya Kitwanga.
 
Waigizaji wazuri wa kuigizia kwa wengine,lilipokuja halisi linalowahusu na sii igizo wote wakaingia mitini kuanzia na mganga mkuu wa opereshini tumbua jipu.
 
Kama ilivyokawaida yetu() kupewa matumaini hewa naamini hapa wanatumia saikolojia ya kwamba wananchi tutaachana nalo tukiona halipewi airtime na media, na halipewi attention yoyote na viongozi wakuu wa serikali iliyopo madarakani. . Kama ilivyoisha ESCROW, NA RICHMOND hili nalo litaisha tuu.
 
Kipimo nambari moja ni Lugumi akiweza basi ataweza IPTL na Escrow!! Kisu mfupani! Hana ujanja! Urais wake una ubia na Kitwanga!!
 
jipu liko makalioni mwa mtu,mpaka aanze kumchunguza,amuinamishe aliandae aliguse guse lilainike mwenyewe abaki anamwangalia tu? mjomba haiwezekaniki hiyo
 
Sitaki kuamini kama Mh Rais hadi leo jipu lililo wazi la Lugumi kinekushinda kulitumbua maana naona hata wabunge wameufyata haligusiki nasikia usaha wake ni mwingi sana unahitaji maandalizi kabla ya kulitumbua maana utachafua hali ya hewa.

Sasa najiuliza kama hili jipu la hivi karibuni je yale majipu ndugu utayaweza maana yale IPTL na ESCROW naona umeamua kuyapa dawa za kuyafifisha sasa ni sukari sukari sukari.
Huu mchezo hautaki hasira!!!!
 
Noma sana haligusiki
 
Buku 7 FC kuña mada ya kuongeza posho huku jamani mada hii ata wale mlioombewa kufikiriwa Na mwenyekiti inawahusu mkiitetea mtafikiriwa
 
Siyo rahisi utawala kumaliza ufisadi wote. Kwa kuwa ufisadi ulikuwa umekithiri, yahitajika akili katika utumbuaji, waweza kukata tawi ulilolikalia.
 
Back
Top Bottom