Suala la malezi kwa watoto limekuwa janga la Taifa. Wazazi mnapohangahikia pesa msisahau watoto wenu

Suala la malezi kwa watoto limekuwa janga la Taifa. Wazazi mnapohangahikia pesa msisahau watoto wenu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kuna mtoto wa jirani mbali kidogo na nyumbani ila kwakuwa nyumba zetu ziko scattered tunaishi kama majirani.

Mtoto huyu huwa anapenda kuja nyumbani hushinda nyumbani mara nyingi. Kwa siku hutumia masaa 4 mpaka 8 nyumbani kwangu hasa kipindi hichi cha likizo.

Nimewahi kumtimua mara 2 kutokana na kuvunja Sheria za nyumbani kwangu. Mara ya kwanza kumtimua alitetewa na mwanangu mkubwa nikamsamehe. Mara ya pili nikamtimua baada ya siku tatu hivi akaja tena.
Inasadikika nyumba nyingi mtaani kwetu katimuliwa kwa tabia zake.

Leo akiwa anacheza na mwanangu wa mwisho wa miaka 2 kasoro huku kaka zake wakifanya vishughuli vidogo vidogo nikiwa chumbani nasikia sauti ya mshituko " G njoo nikuue" mwanangu mkubwa(11 yrs old) akamwambia kuwa baba akisikia shauri yako. Mwanangu wa pili (7 yrs old) akamjibu kwa mshituko unasemaje wewe?

Nikatoka chumbani nikaenda jikoni walipokuwa wameketi nikamuuliza umemwambia nini huyu mtoto?
Akasema nisamehe.

Huyu dogo mtoto wa jirani ana miaka kati ya 10-11. Ndiye amwambie mwanangu mdogo wa miaka 2 kasoro aje amuue kama namna ya kucheza.

Nimemtimua kwa hasira na nimemwambia asije tena. Awamu hii akija nitampiga makofi.

Wazazi wako busy sana , watoto wanadhurula hawana habari.
Hivi mtoto kama huyu anayeweza kuondoka nyumbani na kupotea zaidi ya masaa 4 huku wazazi wakiwa busy au comfortable atanusurika vipi na tabia chafu za ulimwengu?
 
Ni sahihi kabisa.
Mtoto anaweza kushinda kwa jirani asubuhi mpaka jioni, mzazi wala hata hana habari kuhusu kula wala kuoga ya mtoto wake.
 
Ni sahihi kabisa.
Mtoto anaweza kushinda kwa jirani asubuhi mpaka jioni, mzazi wala hata hana habari kuhusu kula wala kuoga ya mtoto wake.
Nachelea kusema mzazi wa namna hiyo hajitambui, mtoto aende kwa jirani siku nzima na upo comfortable kweli?
 
Duuh huyo sio mtoto wa kucheza na wanao kwanza umri umeenda, pili kwa maelezo yako inaokena ana shida mentally. Wakataze wanao wasichangamane nae, hata kama itaonekana una nia mbaya. Ila ni jambo zuri kulinda watoto wako, kinga ni bora kuliko tiba.
 
Aiseee nilisisimka.
Yaani amwite mtoto mdogo amwambie njoo nikuue.
 
Back
Top Bottom