Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Hakuna anayenyonywa kwa wingi wa kodi inayokusanywa na TRA ya matrilioni ya pesa na miradi mingi tu imeajiri mpaka Waingereza achilia mbali wazenji wawili watatu.Kwa kweli watu wengine sijui huwa mnafikiria kwa kutumia viungo gani?United States of America ni nchi moja yenye bendera moja.United States of Africa isingwezekana kwa sababu kuna viinchi vimejaa roho mbaya kama vile Rwanda,Libya yenyewe ya Gadafi,Burundi,Democratic Republic of Congo,Malawi,Zanzibar,Somalia,Sudani na Eritria.Na ndio maana mpaka leo Wazanzibar hawaukubali Utanzania bali Uzanzibar kwao ndiyo jambo la msingi.Kama Tanzania ni nchi moja kwa maoni yangu naona siyo sawa maana kuna bendera za mataifa mawili(Tanzania na zanzibar),kuna marais wawili (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar),kuna Katiba mbili (Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Jamhuri ya Zanzibar ya 1984).
Labda huu Muungano ni wa chama na si Watanzania wote kwa maana taifa moja linaneemeka na rasilimaliza nchi zote lakini taifa lingine linanyonywa kila uchao.
Napoiongelea US natumia mfano wa umuhimu wa mataifa kuungana na kuweza kufanya vizuri. Ulaya kwa sasa wanakaa na Zelensky baada ya kuona ananyanyaswa na Trump, kwa umoja wao wanafikiria ni namna gani wamsaidie akiwa anapitia katika kipindi kigumu.
Ndio akili aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere mwaka 1964 kwamba tunaanza sisi kuungana halafu wazo linasambaa kwa mataifa mengine.
Taifa zima linaneemeka na rasilimali tulizonazo, ndege zinatumiwa na wote, mito na maziwa zinatumiwa na wote, madini yanawafaa wote kwa ujumla wao.
Jiografia yetu ndio imezaa huu muungano, tuwe wapole tu hizi fitina na chokochoko hazina mwisho mzuri. Kujitenga kwetu kunaweza kuzaa ili roho ya kujitenga zaidi na zaidi.