Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Hakuna anayepoteza katika muungano. Kwame Nkrumah mpaka kesho ni shujaa miongoni mwa wanazuoni kwa wazo lake la kutaka kuiunganisha afrika nzima iwe ni muunganiko wa majimbo United States of Africa,.Nchi zinaungana kwasababu mahususi. Nchi zilizojaribu kuungana kwa maelezo yako hapo juu zimeishia pabaya. Tatizo si kuungana bali muundo wa Muungano unaofanya Zanzibar kuwa 'special''
Ni eneo linalowabebesha Watanganyika mzigo.
Mfano, Pesa za maendeleo kwa mkoa wa Dar es Salaam unaochangia 86% ya GDP ni ndogo kuliko zile zinazopelekwa Zanzibar! Kwanini Simiyu, Njombe au Geita ambayo ni mikoa michanga sana isipewe kipaumbele kama Zanzibar licha ya kuchangia Uchumi, Zanzibar ikichangia 0%.
Kuna Waha wameoa Wamanyema wa DRC
Kuna Watanzania wameoa Wakikuyu
Kuna Wakurya wameoa Wamakonde
Nguvu kazi haipatikani kwa kuoleana. Wazanzibar ni 1.5M , Watanganyika ni milioni 60. Ni upuuzi kudhani Muungano unasimamishwa na ndoa. Tumeoa Kenya, Musmbiji, na akina JUX wameoa Nigeria!
Hakuna chuki! itoke wapi? Wazanzibar hawataki Muungano! waachwe warudi kuijenga Nchi yao kama ile ya Wakati wa Sultani. Wanataka iwe kama Dubai, wapewe fursa
Swali langu linabaki pale pale! Nje ya Muungano, Mtanganyika anapoteza nini! Ni swali tu
Muamar Ghadhafi alikuwa na wazo lenye kuunganisha afrika iwe nchi moja, wote wawili hao hawakuwa wajinga, hawakuongozwa na hulka za kibinafsi zenye kujali nyimbo za taifa na bendera waliangalia mbali zaidi ya utukufu wa kibinadamu.
Nyerere hakuwa mjinga kuutetea muungano kwa udi na uvumba. Tatizo letu ni lile lile la kutaka kuwaonyesha wazenji kwamba na sisi tunaweza kufanya huo upuuzi mnaoufanya.
Ni akili za visasi na kukomoana zilizo nyuma ya hizi hoja za kuidai Tanganyika.