Pre GE2025 Suala la maslahi ya Tanganyika tunataka liwe addressed kampeni 2025!

Pre GE2025 Suala la maslahi ya Tanganyika tunataka liwe addressed kampeni 2025!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hayo nayajuwa vyema kabisa, pamoja na kwamba ni nadharia tu, hakuna mwenye uhakika nayo (hayo ya magharibi/mashariki); kwani pia wakati huo palikuwepo na msukumo sana wa nchi kuungana maeneo mbalimbali duniani kwa sababu tofauti na hiyo ya magharibi/mashariki.
Lakini pamoja na hayo yote, hakuna sababu ya kuendelea kuwepo na ubaguzi huu ndani ya taifa moja. Hili sasa limekuwa jambo la kuumiza muungano.
Inasemekana Mwalimu Nyerere alipokwenda kule Marekani mwaka 1963 akaonana na Rais Kennedy alipewa masharti na CIA ya kuhakikisha Russia hawaichukui Zanzibar kama walivyotishia kuichukua Cuba.

Nguvu ya wakubwa ilikuwepo katika kuhakikisha tunaungana mapema iwezekanavyo. Miaka ya karibuni kumekuwepo na vikao vya pamoja kati ya serikali ya mapinduzi na ya muungano katika kutatua kero zinazojitokeza..

Zinapoendelea kuwepo mtu makini anayo haki ya kuhoji kipi kinajadiliwa kwenye vikao hivyo tukizingatia kero bado ni nyingi.
 
Habari za akina Babu hizo za enzi hizo. Kama nilivyo eleza hapo juu, hizi ni nadharia tu zilizo buniwa sababu za uwepo wa muungano.
Wengine wanaeleza hofu ya viongozi wa Mapinduzi kwa wakati huo kugeuziwa kibao na hao walio wapindua; ikbidi haraka watafute mwamvuli wa Tanganyika.

Hizo habari za vikao juu ya "kero", hujui kuwa kero zote zilikuwa ni kutoka upande mmoja tu wa muungano? Na bila shaka utasema utatuzi wa kero hizo ndiko kumeimarisha muungano?
Kushughulikia kero za upande mmoja ndiko sasa kumezaa "KERO" kubwa upande wa pili; na CCM haioni sababu ya kutatua hizo kero za upande huo!
 
inaonyesha nyerere ndio alikuwa anajibembeleza, sawa na unatafuta mwanamke halafu unakubali kuandika viwanja na nyumba zote majina yake alimradi akukubali wakati yeye hana chochote anachooffer.
Umeingiza mfano wa mwanamke ulio hai, mada nzima imesisimka hii.
 
a.

Hizo habari za vikao juu ya "kero", hujui kuwa kero zote zilikuwa ni kutoka upande mmoja tu wa muungano?
Kero ni kutoka upande mmoja, Zanzibar. Kwavile hakuna Tanganyika, nani anawakilisha hoja za Tanganyika! Mleta mada ana hoja nzito kwa kuzingatia hilo, kwamba, lazima kuwepo na Tanganyika ili iilinde masilahi yake. Rais wa JMT si wa Tanganyika ni wa JMT ambayo Zanzibar imo.

Kwa mfano, kuna ujenzi wa 'cable' ya umeme kwenda Zanzibar inalipiwa na JMT.
Nishati si suala la Muungano, lakini, Rais wa JMT anaweza kuamua hivyo kwasababu ni Rais wa JMT.
Swali, Watanganyika wanaolipia cable hiyo wanatendewa haki?

Pili, kuna mikopo ya Wanafunzi HESLB. Wazanzibar wana ZHELSB. Mzanzibar ana haki ya kuchukua HESB kwasababu ni Mtanzania na hapo hapo ZHESLB kwasababu ni Mzanzibar. Mtanganyika hana fursa ya kuchukua ZHESLB. Huyu Mtoto wa Tanganyika aliyekosa mkopoHESLB unamwambiaje!

Tatu, kodi za Tanganyika ndizo za Tanzania. Mchango wa Zanzibar upo wapi? Kama hauonekani, tunapata wapi formula ya kugawa ajira kwa 20% Zanzibar yenye watu milioni 1 na 80 kwa watu milioni 60? Wapi tunapata formula ya kuendesha shughuli za JMT
Na bila shaka utasema utatuzi wa kero hizo ndiko kumeimarisha muungano?
Utatuzi wa kero umezua tatizo kubwa sana kwasababu imekuwa si utatuzi ni ''favor' kwa Wazanzibar.
Zanzibar haijawahi kuonewa hata siku moja kwasababu nyingi ikiwemo kauchumi kadogo, eneo na Watu
Kwahiyo chochote wanachodai si haki ni fadhila kwa gharama za Tanganyika
Kushughulikia kero za upande mmoja ndiko sasa kumezaa "KERO" kubwa upande wa pili; na CCM haioni sababu ya kutatua hizo kero za upande huo!
CCM hawaoni sababu, lakini siku ikifika hawataweza kuzuia tatizo na utakuwa mwisho
Hata ndani ya CCM kuna kutoridhishwa!

JokaKuu
 
CCM hawaoni sababu, lakini siku ikifika hawataweza kuzuia tatizo na utakuwa mwisho
Hata ndani ya CCM kuna kutoridhishwa!
Muda tokea sasa hadi Oktoba ni mchache, lakini hii haizuii hata mara moja kuwa ajenda muhimu kwenye kampeni.
Lakini ni kama kuna uoga fulani juu ya jambo hili la Muungano ndani ya vyama vya siasa kulizungumzia vyema lieleweke kwa wapiga kura. Sabau za uoga huo, bila shaka ni kuogopa 'lebo' ya kuvunja muungano inayo wekwa mbele na CCM.
Naona safari hii CHADEMA wakilipangia muda na kulifafanua vizuri, litakuwa jambo litakalo eleweka kirahisi kwa wapiga kura, badala ya kuwa na hofu ya kuwapotezea kura.
Sioni jinsi gani CCM inavyoweza kujihami juu yake kwa sababu tu za kuhofia kuvunja muungano.

Hii ni ajenda isiyo epukika tena.
 
Utatuzi wa kero umezua tatizo kubwa sana kwasababu imekuwa si utatuzi ni ''favor' kwa Wazanzibar.
Zanzibar haijawahi kuonewa hata siku moja kwasababu nyingi ikiwemo kauchumi kadogo, eneo na Watu
Kwahiyo chochote wanachodai si haki ni fadhila kwa gharama za Tanganyika
"Utatuzi wa kero" kwa Zanzibar kujitambulisha kuwa nchi iliyo huru ndani ya muungano ni utatuzi gani huo?
 
Gentleman,
wananchi wa Tanzania hawana haja ya kubabaika na utapeli wa kisiasa, wala muda wa kutumia kuskiza vibaka wa kisiasa 🐒
Ha ha haa. Nilikua Wazenji lazima muivamie hii hoja.

Mtoa mada anataka kuwatilia mchanga kitumbua. Ha ha haaaaaa
 
Kwa sheria za Zanzibar wanaoishi bara si Wazanzibari hata kama wana asili ya huko.
 
Muda tokea sasa hadi Oktoba ni mchache, lakini hii haizuii hata mara moja kuwa ajenda muhimu kwenye kampeni.
Lakini ni kama kuna uoga fulani juu ya jambo hili la Muungano ndani ya vyama vya siasa kulizungumzia vyema lieleweke kwa wapiga kura. Sabau za uoga huo, bila shaka ni kuogopa 'lebo' ya kuvunja muungano inayo wekwa mbele na CCM.
Naona safari hii CHADEMA wakilipangia muda na kulifafanua vizuri, litakuwa jambo litakalo eleweka kirahisi kwa wapiga kura, badala ya kuwa na hofu ya kuwapotezea kura.
Sioni jinsi gani CCM inavyoweza kujihami juu yake kwa sababu tu za kuhofia kuvunja muungano.

Hii ni ajenda isiyo epukika tena.
Exactly! Ni agenda isiyoepukika kutokana na wakati na population iliyopo. Hapa ndipo CCM wanatatizo.
Laiti tungaalikuwa na chaguzi huru na za haki hii ingalikuwa hoja tosha ya kuiweka CCM mguu sawa.

CCM hawana hoja kilichobaki ni kutishia tu fulani anataka kuvunja Muungano. Kinyume chake,
wanapotishia kuvunja Muungano wanajenga hoja nyingine! Kuna tatizo gani ukivunjika! yaani kizazi cha sasa kinahoji .

Habari ya Muungano kuwa ''taboo' imepitwa na Wakati. Tundu Lissu ameongelea Muungano kwa hoja kali sana zingine zina ukakasi. Jambo la kushangaza na CCM hawalioni ni jinsi Tundu Lissu anavyokubaliwa na pande zote kwa hoja. Dawa anayotoa ni chungu, watu wanakubali ni matibabu.

CHADEMA waichukue hoja hii iwe sehemu ya no reform no election! kwa maana kwamba kunahitajika marekebisho makubwa, wata ''win' sana nyoyo za Watu tena wakiwemo CCM
 
"Utatuzi wa kero" kwa Zanzibar kujitambulisha kuwa nchi iliyo huru ndani ya muungano ni utatuzi gani huo?
Na hili CCM waldhani wana solve tatizo kwa kukaa kimya! bila kujua wametengeneza tatizo kubwa zaidi.
Uwepo wa Zanzibar na Taasisi zote unaifanya JMT kubaki kama Tanganyika na Taasisi zote.

Watanganyika wanahoji , hatuna sababu za kujificha kwa kuita JMT wakati ni Tanganyika. Zanzibar tayari ni Nchi na Rais wake anafanya ziara kwa niaba ya Zanzibar.
Rais wa JMT hana mamlaka Zanzibar, kwa manaa ni Rais wa Tanganyika.

Kama ni Rais wa Tanganyika kwa jina la Tanzania kwanini apatikane kutoka Zanzibar. Ndio maana mamuzi mengi anayofanya hata kwa nia njema, kwa mfano Bandari, yanaangaliwa kw ajicho la ni Mzanzibar badala ya huyu ni Mtanzania.

CCM wanatafuta njia za mkato , wameanza kufuta sherehe za Uhuru wa Tanganyika ili kuzuia hoja ya Utanganyika , ili kupoteza Utanganyika. Kinyume chake watu wanahoji kwanini iwe Dec 09 na siyo January 12. Tena January 12 zinatumika pesa nyingi za Tanganyika kwa kuzindua miradi Zanzibar !
 
Umeichambua vizuri sana hoja yako.
Tunazidi kupata elimu dhidi ya huu muungano.
 
Haya mambo yoote lawama zinaanzia kwa Mwl Nyerere

kwa sasa huu muungano uvunjwe hauna faida yoyote kwa Mtanganyika!
 
Naona wadau mnataka kuvunja muungano?

Hivi haiwezekani wazanzibari wenyewe wakaamua kuivunja serikali yao na kuifanya nchi yao kuwa mkoa. Tukawa Taifa moja completely au ndio hatupendani na hatuaminiani. Kwanza hii mipaka ilichorwa na wakoloni na wazanzibar wengi wanasema asili yao ni unyamwezini.
 
Laiti tungaalikuwa na chaguzi huru na za haki hii ingalikuwa hoja tosha ya kuiweka CCM mguu sawa.
Naamini kuwa pamoja na ufinyu wa muda uliopo, pengine na rabsha nyingi watakazofanya CCM kuwavuruga CHADEMA, 'No Reform, No Election' itawafikia wananchi vyema na kuielewa inalenga nini. Wananchi pekee ndio wenye mamlaka yote ya kuamua hili. Ndiyo maana CHADEMA ni muhimu wawafikishie wananchi maana sahihi ya hili jambo.
Kuchagua viongozi wa nchi hii ni HAKI ya wananchi, siyo fadhila inayotolewa na CCM na vyombo vyake serikalini.

CCM hawana uwezo wa kuzuia wanachotaka wananchi kifanyike.
 
Habari za akina Babu hizo za enzi hizo. Kama nilivyo eleza hapo juu, hizi ni nadharia tu zilizo buniwa sababu za uwepo wa muungano.
Wengine wanaeleza hofu ya viongozi wa Mapinduzi kwa wakati huo kugeuziwa kibao na hao walio wapindua; ikbidi haraka watafute mwamvuli wa Tanganyika.

Hizo habari za vikao juu ya "kero", hujui kuwa kero zote zilikuwa ni kutoka upande mmoja tu wa muungano? Na bila shaka utasema utatuzi wa kero hizo ndiko kumeimarisha muungano?
Kushughulikia kero za upande mmoja ndiko sasa kumezaa "KERO" kubwa upande wa pili; na CCM haioni sababu ya kutatua hizo kero za upande huo!
Mume na Mke wanaishi nyumba moja kwa miaka 40 na hawakosi kutofautiana sembuse nchi mbili?.

Kuungana kuna faida kuliko kutengana na mpaka leo heri wanaoungana kuliko wanaotafuta sababu za kutengana.
 
Naamini hapa ndipo mahali pa kuwa wazi na kueleza kilichopo mtaani ili viongozi wetu kama sio kujirekebisha basi watafute solution ya kudumu kwenye mambo mbalimbali.

1. Raia wengi, wanaamini mtu mwenye courage pekee kuongelea suala la muungano, ni TL.

2. eneo dogo kama zanzibar, lenye watu hada 2m hawafiki, kuwa sawa na eneo kubwa lenye watu zaidi ya 55m, watu hawaridhiki.

3. suala la ardhi, zanzibar wanamiliki bara wapendavyo, ila bara marufuku kumiliki zanzibar?

4. kazi, asilimia 20% kazi bara wanapata wazanzibar, ila marufuku mtanganyika kuajiriwa zenji.

5. raia wa zanzibar waliowengi hasa wasio na makazi bara, hawawapendi watanganyika wala muungano. hata wale waliofaidika na tanganyika na kuishi bara, chuki wanazo nyingi sana na ipo wazi.

6. viongozi wa kuteuliwa kama mawaziri, wakurugenzi n.k, hatuwezi kuwa sawa, not fair.

7. Rais anatoka zanzibar, anaweza kuwa Rais zanzibar na akawa rais bara, ruksa, nasemani rais bar akwa sababu hata akiitwa rais wa muungano akienda zanzibar anakuwa chini ya rais wa zanzibar.

8. wengi pamoja na kwamba wapo tayari hata uvunjike, lakini kwa sababu tumeshaishi pamoja miaka mingi, wanasema hata usipovunjika itakuwa safi, ila kipengele cha rais wa zanzibar kiondoke, issue ya umiliki wa ardhi iondoke, na issue za ajira ziwe fair mtu aajiriwe pande zote mbili.

9. haiji kichwani, wewe unasema unapenda muungano, ila hautaki tuungane. kama tungemiliki ardhi kwa pamoja, wabara wata assimilate zanzibar na wazanzibari wataassimilate bara, na hapatakuwa na Tanganyika wala Zanzibar, itakuwapo TANZANIA. sasa kama wewe haupendi tuassimilate to each other, muungano upo wapi sasa na ni wa nini? si utakuwa muungano wa upande mmoja? yaani leo hii zanziba anaamini anapenda muungano ila akiruhusu ardhi ya zanzibar imilikiwe watanganyika wataimiliki yote na wazanzibar watakosa au zanzibar haitakuwepo tena, sasa kama unataka iwepo, unataka muungano upi na kivipi?

TL akija na gia hii kwenye kampeni, ndipo ajajua nini hasa kilichopo kwenye mioyo ya watanganyika, hata kitendo cha kutawaliwa na mzanzibari ambaye hatujui maslahi yake yapo bara au zenji, na hatujui pesa zetu kama zinapelekwa kujenga zenji au la. ni hayo tu. TL nishakupa password ya kuteka mioyo ya wabara tayari, kuichukua au kuiacha ni juu yako.
Sasa Mhuni Lissu atalielezeaje kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 wakati yeye hautaki huo uchaguzi?
 
Naamini kuwa pamoja na ufinyu wa muda uliopo, pengine na rabsha nyingi watakazofanya CCM kuwavuruga CHADEMA, 'No Reform, No Election' itawafikia wananchi vyema na kuielewa inalenga nini. Wananchi pekee ndio wenye mamlaka yote ya kuamua hili. Ndiyo maana CHADEMA ni muhimu wawafikishie wananchi maana sahihi ya hili jambo.
Kuchagua viongozi wa nchi hii ni HAKI ya wananchi, siyo fadhila inayotolewa na CCM na vyombo vyake serikalini.

CCM hawana uwezo wa kuzuia wanachotaka wananchi kifanyike.
No reform no election ni kauli mbiu nyingine inayokuja na kupita, ni sawa na zile za Mbowe alizobuni kila kukicha na kupiga pesa kutoka kwa wazungu.

Sugu kaenda Marekani na kaishia kupiga picha na watu wa state department hakuna cha maana alichopewa, Trump hatoi tena pesa za bure bure na CDM ilistawishwa kwa kupewa hizo pesa enzi za miaka ya nyuma.

Lissu analo tatizo la ukosefu wa pesa kuelekea uchaguzi mkuu, huwezi kuwasikia chawa wake humu kina Erythrocyte wakiuongea huo ukweli watakuja na mada za kuwajaza ujinga vijana wa upinzani lakini ukweli ni kwamba Mbowe aliweza kuiendesha Chama kwa nguvu ya pesa, na Lissu kwa sasa yupo chali hana kitu. Hapo sijaongelea namna yeye mwenyewe alivyo tofauti na Mbowe.
 
Mume na Mke wanaishi nyumba moja kwa miaka 40 na hawakosi kutofautiana sembuse nchi mbili?.

Kuungana kuna faida kuliko kutengana na mpaka leo heri wanaoungana kuliko wanaotafuta sababu za kutengana.
Mkuu 'Steve' usidhani sikuelewi, na juwa tu ni kiasi gani tulivyo upenda muungano wetu huu pamoja na kasoro zake nyingi. Muungano toka mwanzo haukuwa 'perfect', lakini matarajio yalikuwa kwamba hapo tutakapo zoeana na kuona faida za kuungana, muungano wetu unge imarika zaidi. Lengo lilikuwa hilo tokea mwanzo, licha ya mapungufu yaliyo kuwepo toka mwanzo.
Badala ya matarajio hayo ya mwanzo kuwa kama ilivyo tegemewa, kero zikashika kasi mwaka hadi mwaka!

Umetumia mfano wa ndoa. Ni wazi unajuwa ni ndoa ngapi huishia njiani kwa sababu mbalimbali, au siyo?

Hii ndoa yetu ya muungano sasa hivi katika inashikiliwa na wachache sana wanao nufaika nayo moja kwa moja. Siyo ndoa inayo nufaisha taifa tena. Ni CCM pekee ndio wanao ona faida kwa kuendelea kuwaweka madarakani.
 
Back
Top Bottom