Pre GE2025 Suala la maslahi ya Tanganyika tunataka liwe addressed kampeni 2025!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna anayenyonywa kwa wingi wa kodi inayokusanywa na TRA ya matrilioni ya pesa na miradi mingi tu imeajiri mpaka Waingereza achilia mbali wazenji wawili watatu.

Napoiongelea US natumia mfano wa umuhimu wa mataifa kuungana na kuweza kufanya vizuri. Ulaya kwa sasa wanakaa na Zelensky baada ya kuona ananyanyaswa na Trump, kwa umoja wao wanafikiria ni namna gani wamsaidie akiwa anapitia katika kipindi kigumu.

Ndio akili aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere mwaka 1964 kwamba tunaanza sisi kuungana halafu wazo linasambaa kwa mataifa mengine.

Taifa zima linaneemeka na rasilimali tulizonazo, ndege zinatumiwa na wote, mito na maziwa zinatumiwa na wote, madini yanawafaa wote kwa ujumla wao.

Jiografia yetu ndio imezaa huu muungano, tuwe wapole tu hizi fitina na chokochoko hazina mwisho mzuri. Kujitenga kwetu kunaweza kuzaa ili roho ya kujitenga zaidi na zaidi.
 
Hakuna anayenyonywa kwa wingi wa kodi inayokusanywa na TRA ya matrilioni ya pesa na miradi mingi tu imeajiri mpaka Waingereza achilia mbali wazenji wawili watatu.
Kwanini kuna nafasi maalumu za ajira kwa Uzanzibar! 21%.
Katika hayo matrilioni ya TRA Zanzibar inachangia kiasi gani
Ndio akili aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere mwaka 1964 kwamba tunaanza sisi kuungana halafu wazo linasambaa kwa mataifa mengine.
Wazo limefeli, tuendelee kushikilia tu!
Taifa zima linaneemeka na rasilimali tulizonazo, ndege zinatumiwa na wote, mito na maziwa zinatumiwa na wote, madini yanawafaa wote kwa ujumla wao.
Bandari ya Zanzibar inatumiwa na wote? Bahari ya Zanzibar inatumiwa na wote?
Hizo ndege SMZ imetoa kiasi gani kuzinunua?
Jiografia yetu ndio imezaa huu muungano, tuwe wapole tu hizi fitina na chokochoko hazina mwisho mzuri. Kujitenga kwetu kunaweza kuzaa ili roho ya kujitenga zaidi na zaidi.
Wazanzibar wanasema hapana! Wao ni Wazanzibar na wanataka Zanzibar yao. Wao si Watanzania
Wanakuwa Watanzania wanapohitaji kufaidika tu!

Walioanza wazo la kujitenga ni Wazanzibar. Miaka nenda rudi wanasema MAMLAKA KAMILI
Katiba ya 1984 iliyofanyiwa marekebisho 2010 ''imevunja' muungano, kwavile waliofanya ni Wazanzibar hilo lipo chini ya kapeti. Mbowe aliposema neno kuhusu Bandari alishambuliwa kwa chuki

Wakati Wazanzibar wanaeneza chuki na kujitenga, ninyi milikuwa kimya
Watanganyika, wanataka Wazanzibar waheshimiwe maoni yao mnasema ni chuki

Kwani kuna Tatizo gani Tanganyika ikiwepo? halafu tukachagua mambo ya kuwasaidia?
Katiba ya Warioba ilisema ni 7 tu!
 
Hili suala la muungano ni la kuweka sawa kabisa. Ni either huu muundo uliopo urekebishwe na uwe Muungano wa kweli na usawa pande zote mbili au usiwepo kabisa. Na Tanganyika tukiona tuna maslahi mapana na Zanzibar alafu wao hawataki usawa, basi tunaibadilisha Zanzibar kuwa mkoa na tunaitawala kimabavu.
 
umesema kweli
 
Marais wawili wote wa zanzibari mwinyi samia wanahamisha mno mali za bara kupeleka zanzibar usalama ipo ipo tu ka mazuzu
 
Marais wawili wote wa zanzibari mwinyi samia wanahamisha mno mali za bara kupeleka zanzibar usalama ipo ipo tu ka mazuzu
KAMA unataka kuamini hilo, ona sasaivi hawalalamiki wala nini, kwa sababu wanajua ndio muda wao wa kula.
 
Hoja zako ni za msingi lakini jambo moja watanganyika mnalofeli ni suala la ardhi. ZANZIBAR ni eneo dogo sana ukilinganisha na tanganyika. Eneo la tanganyika ni km za mraba karibia million 1, zanzibar hazifiki hata elfu 3, watanganyika mko million 55 , mkisema mnakuja kununua ardhi sisi tutaishi wapi muwe na huruma
 
Uchoyo mmebarikiwa. Huku bara mme jaa na mnanunua ardhi mno shida ikwapi
 
Ardhi yenu ni kubwa sana sisi hata tukinunua sote haimaliziki, lakini ardhi ya zanzibar ni ndogo sana,
ahahah we jamaa mchoyo mchoyo.....isije kuwa kama Rwanda na Kongo huko baadae...mkajiimarisha zaidi huku bara kwa manufaa ya zanzibar
 
mtaishi wapi? si tutaishi wote humohumo? kwa hiyo mnaona bora muwape wataliano kuliko wabongo? na bado kuna visiwa na ardhi kibao imebaki, ila uchoyo na ujinga umewajaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…