Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Hapo issue sio ushabiki mwenzetu yupo hapo kimaslahi zaidi ...hana mapenzi na ccm kiasi hicho mpaka kujitoa akili
 
Kichaa Dotto Magari aliwahi kutuambia, maskini hana kiapo. Sasa nimekubali msemo wake.

Nini hasa kimemtokea msanii AY ?
View attachment 3247946
Mkuu unachuma dhambi kijinga mno. Ulimpima Dotto ukajua ni kichaa? Halafu kuna sheria ya jamhuri au ya Mungu imevunjwa na AY kushabikia CCM? Haki mnazopigania ndo mnatakiwa mziheshimu na sio kuwanyooshea vidole wengine walioamua kuwa tofauti na nyie.
 
Hapo issue sio ushabiki mwenzetu yupo hapo kimaslahi zaidi ...hana mapenzi na ccm kiasi hicho mpaka kujitoa akili
Kwanza suala la maslahi linahitaji ushahidi. Hata kama ni kweli, ushahidi unahitajika ili tujue ni kweli.

Unajuaje kikichopo kwenye kichwa cha AY kuweza kusema hana mapenzi na CCM hivyo?

Pili, mwanachama au mshabiki wa chama kushabikia kwa maslahi si ajabu. Kila mtu ana haki ya kuwa mwanachama au mshabiki wa chama kwa kuangalia maslahi yake.

Hata unapopigia kura chama unatakiwa kuangalia chama gani kitaboresha maisha yako. Hayo ni maslahi pia.

Tatizo liko wapi?

Mpaka sasa hujanionesha tatizo la AY kuishabikia CCM au kumshabikia Samia liko wapi.

Naelewa kunaweza kuwa na tofauti za kisiasa, lakini hilo halifanyi AY kuwa kakosea. Kwa sababu, kifalsafa, AY kushabikia CCM au kumshabikia Samia ni haki yake ya kiraia, ya kikatiba, ya kibinadamu.

Kosa la AY kushabikia CCM au kumshabikia Samia (ukiondoa mambo ya tofauti za kisiasa, hizo hazina mashiko kwenye hoja yangu, kwa sababu zinakubakiwa
Jata mimi mwenyewe siikubali CCM, simkubali Samia )

Kosa la AY ni lipi hasa?
 
Nitoke vipi sasa AY nani anamjua kwa kizazi hiki cha genz,asipouza sura atajulikanaje asife njaa
 
Mkuu he has the family to feed and not the society to impress.

Usifanye masikhara na njaa ,kama inakupa hela pita nayo...yupo kazini hapo.
 
Maisha magumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…