Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Huyu jamaa alijijengea heshima kubwa sana katika bongo fleva na kuonekana ni mmoja ya wasanii wa bongo wanaopush mziki huo kimataifa.

Kuna kipindi akawa yupo mamtoni huko anapiga mitkasi yake!

Sasa hivi tunae hapahapa kwa Nyerere, amegeuka chawa mwandamizi wa mama Samia.

Kichaa Dotto Magari aliwahi kutuambia, maskini hana kiapo. Sasa nimekubali msemo wake.

Nini hasa kimemtokea msanii AY ?
View attachment 3247946
Noma sana
 
Kwa kweli inasikitisha kuona watu wanawaingilia wenzao katika haki zao za kikatiba na kibinadamu.

Kwani msanii hatakiwi kushabikia CCM?

Mimi si mpenzi, mwanachama wala mshabiki wa CCM.

Lakini, kifalsafa, kila mtu ana haki ya kushabikia chama anachokitaka.

Tuwapinge watu kwa hoja, sio kwa sababu wameamua kushabikia chama fulani.

Kushabikia chama chochote anachoamua mtu, au mwanasiasa yeyote, ni haki ya uraia, ni haki ya kikatiba, ni haki ya kibinadamu.

Kwa nini watu wanaodai demokrasia wao wenyewe wanashindwa kuheshimu uamuzi wa watu wengine kushabikia vyama fulani au wanasiasa fulani, kitu ambacho ni sehemu ya demokrasia?
Kuna tofauti ya kuwa shabiki au mwanacha chama fulani na kuwa chawa, japo ni mstari mwembamba sana unaotenganisha haya mambo.
 
Kuna tofauti ya kuwa shabiki au mwanacha chama fulani na kuwa chawa, japo ni mstari mwembamba sana unaotenganisha haya mambo.
Hata kuwa chawa ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Mtu akiamua kuwa chawa wa Samia, unaweza kumpinga kwa point kwamba hapa ka support ujinga, unapinga hoja yake, lakini ile kuwa chawa tu, hiyo ni haki yake na hutakiwi kumpinga mtu kwa sababu kaamua kuwa chawa wa fulani.

Kuwa chawa ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Hapo kuna haki za self determination, haki za political assembly, kuna haki nyingi sana za kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Kwa nini watu mnaotaka demokrasia mnataka kuwavunjia hawa wasanii haki zao?
 
Kwa kweli inasikitisha kuona watu wanawaingilia wenzao katika haki zao za kikatiba na kibinadamu.

Kwani msanii hatakiwi kushabikia CCM?

Mimi si mpenzi, mwanachama wala mshabiki wa CCM.

Lakini, kifalsafa, kila mtu ana haki ya kushabikia chama anachokitaka.

Tuwapinge watu kwa hoja, sio kwa sababu wameamua kushabikia chama fulani.

Kushabikia chama chochote anachoamua mtu, au mwanasiasa yeyote, ni haki ya uraia, ni haki ya kikatiba, ni haki ya kibinadamu.

Kwa nini watu wanaodai demokrasia wao wenyewe wanashindwa kuheshimu uamuzi wa watu wengine kushabikia vyama fulani au wanasiasa fulani, kitu ambacho ni sehemu ya demokrasia?
IMG_5414.jpeg

Mkuu tofautisha kuunga mkono na uchawa. Uchawa ni kumnafikia mtu kwa sababu ya njaa. Hiyo ndio tunayoikataa
 
View attachment 3248046
Mkuu tofautisha kuunga mkono na uchawa. Uchawa ni kumnafikia mtu kwa sababu ya njaa. Hiyo ndio tunayoikataa
Kwanza kabisa hilo la kumnafikia mtu kwa sababu ya njaa ni vigumu kuliprove.

This is a contentious, argumentative and controversial claim.

Unaposema njaa una maana gani? Unaweza kuthibitisha AY ana njaa hivyo?

Pia, kumuita mtu mnafiki ni judgement call. Unafiki wa AY uko wapi? Kuna siku AY aliwahi kujitambulisha kuwa yeye ni msanii activist wa upinzani useme sasa kawageuka wapinzani kinafiki? AY mbona hata kwenye muziki amejitambulisha yeye ni "Mzee wa Commercial"?

Na hata kama kageuka, utajuaje kwamba kageuka kinafiki na si kwa kuona kweli kuwa matumaini ya maendeleo ya Tanzania yapo CCM?

Unaposema huyu chawa mnafiki, unahakikishaje huyu ni chawa mnafiki na si mtu tu ambaye kaona CCM, pengine pamoja na mapungufu yake yote, bado ndiyo chama sahihi kwake kuongoza nchi?

Mimi si mwanachama wala shabiki wa CCM au Samia, lakini naona kama mnaingilia uhuru wa watu kuamua wanataka ku support chama na mwanasiasa gani.

Hii ni haki yao ya msingi ya kiraia, kikatiba na kibinadamu. Na kwa kuwa ni haki ya msingi hivyo, hamna haki kuwaingilia watu katika haki hiyo.
 
$400,000 Marekani unanunua nyumba ya maana, sema watu ambao hamjawahi kusafiri kila kitu mnaona hatari
Hata mimi nilishangaa sana nilipokuwa naangali kipindi cha House Hunters ,unakuta nyumba fresh tu tena beach front inauzwa $600,000.
 
Siasa zetu kwa kipindi hiki zimekuja kutugawa sana na kama hali itaendelea hivi sijui itakuwaje. Siku hizi mijadala ya kina baina ya mtu na mtu bila kukoseana heshima au bila matusi ni ya nadra sana.

Ninaweza kuichukia CHADEMA bila kumuingilia mtu haki yake ya kikatiba na kibinadamu ya kuipenda CHADEMA, vile vile ninaweza kuichukia CCM bila kumuingilia mtu vitu ambavyo havunji sheria na ni haki yake kama kuchagua chama chochote cha siasa anachokipenda. Hivyo hivyo kwa vyama vyote vya siasa nchini.

Siasa za upendeleo pia ni tatizo linalopelekea haya, sasa hivi wakijitokeza wasanii wakapiga picha kama hiyo wakashikilia bendera ya CHADEMA mkuu Kiranga unafikiri kwenye career yao itakuwaje kuanzia deals, shows mpaka stahiki zao BASATA?

Pia AY miaka yote kama nitakuwa sahihi hajawahi kuonekana akifanya vitu vya namna hii, alionekana ni key kwenye kuuvusha muziki huu kuwa international zaidi. Alijiweka kando kidogo na siasa, hii ndio nadhani sababu ya wengi kushangaa.

Back
Top Bottom