Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Hata kuwa chawa ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Mtu akiamua kuwa chawa wa Samia, unaweza kumpinga kwa point kwamba hapa ka support ujinga, unapinga hoja yake, lakini ile kuwa chawa tu, hiyo ni haki yake na hutakiwi kumpinga mtu kwa sababu kaamua kuwa chawa wa fulani.

Kuwa chawa ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Hapo kuna haki za self determination, haki za political assembly, kuna haki nyingi sana za kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Kwa nini watu mnaotaka demokrasia mnataka kuwavunjia hawa wasanii haki zao?
Sycophancy/uchawa ni tatizo kubwa sana kwenye demokrasia au utawala wowote, hata demokrasia ya Marekani imezidi kuvuja kwa sababu ya sycophancy.
Kwa sababu wewe ni mpenzi wa vitabu nakushauri usome kitabu cha Sucking Up cha Deborah Parker.
 
Siasa zetu kwa kipindi hiki zimekuja kutugawa sana na kama hali itaendelea hivi sijui itakuwaje. Siku hizi mijadala ya kina baina ya mtu na mtu bila kukoseana heshima au bila matusi ni ya nadra sana.

Ninaweza kuichukia CHADEMA bila kumuingilia mtu haki yake ya kikatiba na kibinadamu ya kuipenda CHADEMA, vile vile ninaweza kuichukia CCM bila kumuingilia mtu vitu ambavyo havunji sheria na ni haki yake kama kuchagua chama chochote cha siasa anachokipenda. Hivyo hivyo kwa vyama vyote vya siasa nchini.

Siasa za upendeleo pia ni tatizo linalopelekea haya, sasa hivi wakijitokeza wasanii wakapiga picha kama hiyo wakashikilia bendera ya CHADEMA mkuu Kiranga unafikiri kwenye career yao itakuwaje kuanzia deals, shows mpaka stahiki zao BASATA?

Pia AY miaka yote kama nitakuwa sahihi hajawahi kuonekana akifanya vitu vya namna hii, alionekana ni key kwenye kuuvusha muziki huu kuwa international zaidi. Alijiweka kando kidogo na siasa, hii ndio nadhani sababu ya wengi kushangaa.
Naam,

Umesema mengi ya msingi.

Tuwaachie wasanii haki zao za kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Ukweli kwamba AY hakuwahi kujihusisha na siasa haumuondolei haki zake za kuanza kufanya hivyo leo.

Unaweza kumpinga AY kwenye vitu specific. Kwa mfano, AY akisema hela za Samia ndiyo z8natengeneza barabara na kujenga shuke, hapi unaweza kumkosoa na kusema hizo ni hela za walipakodi.

Huo ni mjadala wa hoja, una nuance. Hapo unaweza kumpinga mtu kwa point.

Lakini hizi habari za kumpinga mtu kwa sababu kaamua kuishabikia CCM na Samia wakati wewe unayepinga hivyo unadai demokrasia zaidi ni contradiction.

Kwa sababu hata AY kuishabikia CCM na kumshabikia Samia ni demojrasia pia.

Sasa unawezaje kutaka haki za kidemokrasia zaidi wewe wakati mwenzako AY unaiminya haki yake ya kidemokrasia?

This is a contradiction.

Labda tuwe nuanced zaidi, tunapowapinga hawa wasanii, tunapinga nini?

Tunaponga uhuru wa watu kujiamukia wanataka kushabikia chama gani na mwanasiasa gani?

Kwa sababu kama tunapinga uhuru huu, hata na sisi tunaweza kuingia kwwnye mtego wa kupangiwa tu support chama na mwanasiasa gani kwa hoja hiyo hiyo.
 
This is a contradiction.

Labda tuwe nuanced zaidi, tunapowapinga hawa wasanii, tunapinga nini?

Tunapopinga uhuru wa watu kujiamukia wanataka kushabikia chama gani na mwanasiasa gani?

Kwa sababu kama tunapinga uhuru huu, hata na sisi tunaweza kuingia kwwnye mtego wa kupangiwa tu support chama na mwanasiasa gani kwa hoja hiyo hiyo.
Kwani kupinga au kukosoa sycophancy sio sehemu ya uhuru wa kidemokrasia?
 
Sycophancy/uchawa ni tatizo kubwa sana kwenye demokrasia au utawala wowote, hata demokrasia ya Marekani imezidi kuvuja kwa sababu ya sycophancy.
Kwa sababu wewe ni mpenzi wa vitabu nakushauri usome kitabu cha Sucking Up cha Deborah Parker.
Unahakikishaje huu ni uchawa na si mapenzi ya mtu tu au msimamo wake wa kifalsafa tu?

Na zaidi, kitu kikishakuwa haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu kwa mtu, akikitumia kwa sababu yoyote, huna haki ya kumsimanga.

Yani ni hivi, kama kupigia kura chama au mwanasiasa unayemtaka ni haki yako ya kiraia, kikatiba na kibinadamu, haijalishi umepiga kura kwa sababu gani, hiyo itabaki kuwa ni haki yako tu na haki hiyo haitakiwi kuhojiwa. Kwa sababu ni haki yako.

Pia, ni vigumu sana kutenganisha uchawa na msimamo wa kifalsafa. Pengine hata kwa AY mwenyewe kujua wapi msimamo wa kifalsafa unaishia na wapi uchawa unaanzia si rahisi.

AY anaweza kukuambia kuwa anaona kabisa kuwa hakuna chama ambacho kina uwezo wa kuipeleka Tanzania kwenye maendeleo zaidi ya CCM. Huo ukawa ni msimamo wake wa kisiasa na kifalsalsafa anaouamini kabisa. Akaona kuwa wapinzani wote ni waduanzi. Na CCM, licha ya matatizo yake yote, kinarekebishika na ndiyo chama sahihi.

Kuna watu wengi tu sio wasanii wana msimamo huu.

Na AY labda kaona yeye ana uwezo wa kukisaidia CCM kifanye vizuri zaidi.

Kwa nini unalazimisha mtu anayeweza kuwa na maoni hayo iwe lazima yeye anakifagilia CCM kwa sababu ya uchawa tu?

Zaidi ya yote, hata uchawa nao ni sehemu ya haki ya kibinadamu, kiraia na kikatiba ya mtu kujiamulia mambo yake. Mtu yeyote anatakiwa kuangalia maslahi yake ili kukikubali chama. Sasa msanii akiangalia maslahi yake akatumia haki zake hizo kuwa chawa wa chama anachokitaka mwenyewe, tatizo liko wapi?

Natafuta tatizo la AY kuamua kuishabikia CCM na Samia, kisiasa, kifalsafa, kichawa, bado silioni.

Naona watu wanamlazimisha mtu aliyechagua upande anaoutaka yeye asichague upande huo tu.
 
Kwani kupinga au kukosoa sycophancy sio sehemu ya uhuru wa kidemokrasia?
Hujaweza hata kuthibitisha kuwa hiyo ni sycopanthy.

Umefanya judgement call kirahisi kwenye jambo lililo complex.

Na hata hiyo sycopanthy ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.

Ni sehemu ya self determination.

Ukimshambulia mtu kwa sababu kaamua kuwa chawa ni kama vile unasema huna hoja ya kumpinga.

Kwa sababu kila mtu ana haki ya kuwa chawa wa mtu yeyote anayemtaka.

Hiyo ndiyo demokrasia. Kumshambulia mtu kwa sababu katumia haki hii ni kuiminya haki yake ya kidemokrasia.

Kwa hiyo uchawa si kosa.

Labda kuna jambo lingine mnashindwa kulieleza vizuri tu.
 
Damn right.

Sasa kwa nini wabongo wengi wanao support upinzani wanaona kila msanii ni lazima awe mpinzani, na asipokuwa mpinzani basi ni chawa mshenzi shetani mganga njaa?
Ni kwamba huelewi uhalisia wa mazingira ya siasa za Tanzania? Katika common senses tu katika mazingira ambayo upinzani umekuwa unakandamiziwa na kufanyiwa rafu nyingi sana zilizo mbaya bado unategemea hao watu watakuwa waungawana na wastaarabu kama zilivyo siasa za UK, Germany, Japan n.k?!
 
Mimi nakubali kabisa sycophancy ni haki ya kidemokrasia ya mtu lakini hiyo haiondoi ukweli pia kwamba Sycophancy ni tatizo katika demokrasia au utawala wowote, haiondoi ukweli pia kwamba ni haki ya kideomkrasia watu kukosoa au kuwakataa sycophants.
 
Ongeleeni hayo matatizo specifically sasa.

Msiwapangie wasanii vyama na wanasiasa wa ku support.

Wana haki ya kuchagua mwanasiasa wa kuwa support.

Mimi ningewaona, mna hoja sana kama, kwa mfano, mngeleta habari specific kuwa kuna corruption kubwa sana kati ya wasanii na CCM, corruption hii inatumia pesa za walipa kodi kuwalipa wasanii wanao i support CCM. AY kapiga milioni kadhaa za serikali, pesa za walipa kodi, kwa kumshabikia Samia na CCM.

Hapo sasa una hoja kubwa, hoja nzito, hoja specific, preferably yenye detail.

Hoja si AY kuwa chawa wa Samia tu.

Hoja AY kapiga hela za rushwa kwa gharama ya wapigakodi kwenye uchawa wake kwa Samia.

Hapo sasa ungekuwa na hoja, kwa sababu umeenda far and above simple uchawa tu, umeonesha corruption, uneonesha matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.

That's what you guys need to do.

Hizi habari za AY chawa wa Samia tu hazina mashiko. Kama AY chawa wa Samia wewe unaruhusiwa kuwa chawa wa Lissu, what's the big deal?

That is democracy.
 
Mimi nakubali kabisa sycophancy ni haki ya kidemokrasia ya mtu lakini hiyo haiondoi ukweli pia kwamba Sycophancy ni tatizo katika demokrasia au utawala wowote, haiondoi ukweli pia kwamba ni haki ya kideomkrasia watu kukosoa au kuwakataa sycophants.
Sasa unatenganishaje sycopanthy ya ushabiki tu ambayo ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu isiyo tatizo na sycopanthy yenye tatizo?
 
Damn right.

Sasa kwa nini wabongo wengi wanao support upinzani wanaona kila msanii ni lazima awe mpinzani, na asipokuwa mpinzani basi ni chawa mshenzi shetani mganga njaa?
Ndio wasanii wote wawe ccm? Ndio ujue huko ccm wapo kimaslahi ...yaan wasanii almost 300 wote wawe kwenye chama kimoja? Kwenye nchi yenye vyama vingi? Kwa vyovyote vile huko ccm wanafata pesa
 
Ongeleeni hayo matatizo specifically sasa.

Msiwapangie wasanii vyama na wanasiasa wa ku support.

Wana haki ya kuchagua mwanasiasa wa kum support.

Mimi ningewaona, mna hoja sana kama, kwa mfano, mngeleta habari specific kuwa kuna corruption kubwa sana kati ya wasanii na CCM, corruption hii inatumia pesa za walipa kodi kuwalipa wasanii wanao i support CCM. AY kapiga milioni kadhaa za serikali, pesa za walipa kodi, kwa kumshabikia Samia na CCM.

Hapo sasa una hoja kubwa, hoja nzito, hoja specific, preferably yenye detail.

Hoja si AY kuwa chawa wa Samia tu.

Hoja AY kapiga hela za rushwa kwa gharama ya wapigakodi kwenye uchawa wake kwa Samia.

Hapo sasa ungekuwa na hoja, kwa sababu umeenda far and above simple uchawa tu, umeonesha corruption, uneonesha matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.

That's what you guys need to do.

Hizi habari za AY chawa wa Samia tu hazina mashiko. Kama AY chawa wa Samia wewe unaruhusiwa kuwa chawa wa Lissu, what's the big deal?

That is democracy.
Wewe unaona sycophancy sio tatizo kwenye demokrasia au utawala wowote?

Pia sycophancy/uchawa unahusishwa na fursa ndio maana sio rahisi sana kusema kuna chawa wa Lissu.
 
Ndio wasanii wote wawe ccm? Ndio ujue huko ccm wapo kimaslahi ...yaan wasanii almost 300 wote wawe kwenye chama kimoja? Kwenye nchi yenye vyama vingi? Kwa vyovyote vile huko ccm wanafata pesa
Mkuu mbona wasanii kibao wameenda CHADEMA wengine mpaka wakapata ubunge, kina Sugu, kina Prof. Jay.

Tena Prof. Jay alianzia CCM akahamia CHADEMA.

Na hata wasanii wote wakienda CCM, tatizo liko wapi? Si haki yao ya kiraia, kikatiba na kibinadamu?

Unataka kuwapangia waende wapi?
 
Sasa unatenganishaje sycopanthy ya ushabiki tu ambayo ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu isiyo tatizo na sycopanthy yenye tatizo?
Huu ni mjadala mwingine, ila kwa kuanzia tu sycophancy sio nzuri kwa ujumla wake na zaidi sycophancy mbaya ni ile inayohusishwa na fursa au maslahi binafsi. Mtu akiwa chawa wa Lissu ambaye anasema tunahitaji katiba mpya na tume huru hii haiwezi kuwa tatizo sana ila unapkuwa chawa unayesema hatuhitaji tume huru au katiba bora zaidi hili ni tatizo.
 
Wewe unaona sycophancy sio tatizo kwenye demokrasia au utawala wowote?

Pia sycophancy/uchawa unahusishwa na fursa ndio maana sio rahisi sana kusema kuna chawa wa Lissu.
Nimekuuliza unatofautishaje hii ni sycopanthy ya fursa na hapa mtu anafanya uchawa kwa mapenzi yake tu?

Hujajibu.

Nimekupa mfano wenye specificity jinsi gani unaweza ku raise a legitimate concern kuhusu uchawa wa watu kama AY kwenye rushwa huko. Muweke specific claims zilizopita hoja banal ya "huyu chawa wa Samia" (hoja ambayo haina mashiko kwa sababu uchawa ni haki ya kidemokrasia, hata wewe unaruhusiwa kuwa chawa wa mtu unayemtaka).

Wekeni hoja jamani hii habari ya "AY chawa wa Samia" si hoja.

Uchawa ni haki ya kidemokrasia, kiraia, kisiasa, kikatiba na kibinadamu.
 
Back
Top Bottom