Sycophancy/uchawa ni tatizo kubwa sana kwenye demokrasia au utawala wowote, hata demokrasia ya Marekani imezidi kuvuja kwa sababu ya sycophancy.
Kwa sababu wewe ni mpenzi wa vitabu nakushauri usome kitabu cha Sucking Up cha Deborah Parker.
Unahakikishaje huu ni uchawa na si mapenzi ya mtu tu au msimamo wake wa kifalsafa tu?
Na zaidi, kitu kikishakuwa haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu kwa mtu, akikitumia kwa sababu yoyote, huna haki ya kumsimanga.
Yani ni hivi, kama kupigia kura chama au mwanasiasa unayemtaka ni haki yako ya kiraia, kikatiba na kibinadamu, haijalishi umepiga kura kwa sababu gani, hiyo itabaki kuwa ni haki yako tu na haki hiyo haitakiwi kuhojiwa. Kwa sababu ni haki yako.
Pia, ni vigumu sana kutenganisha uchawa na msimamo wa kifalsafa. Pengine hata kwa AY mwenyewe kujua wapi msimamo wa kifalsafa unaishia na wapi uchawa unaanzia si rahisi.
AY anaweza kukuambia kuwa anaona kabisa kuwa hakuna chama ambacho kina uwezo wa kuipeleka Tanzania kwenye maendeleo zaidi ya CCM. Huo ukawa ni msimamo wake wa kisiasa na kifalsalsafa anaouamini kabisa. Akaona kuwa wapinzani wote ni waduanzi. Na CCM, licha ya matatizo yake yote, kinarekebishika na ndiyo chama sahihi.
Kuna watu wengi tu sio wasanii wana msimamo huu.
Na AY labda kaona yeye ana uwezo wa kukisaidia CCM kifanye vizuri zaidi.
Kwa nini unalazimisha mtu anayeweza kuwa na maoni hayo iwe lazima yeye anakifagilia CCM kwa sababu ya uchawa tu?
Zaidi ya yote, hata uchawa nao ni sehemu ya haki ya kibinadamu, kiraia na kikatiba ya mtu kujiamulia mambo yake. Mtu yeyote anatakiwa kuangalia maslahi yake ili kukikubali chama. Sasa msanii akiangalia maslahi yake akatumia haki zake hizo kuwa chawa wa chama anachokitaka mwenyewe, tatizo liko wapi?
Natafuta tatizo la AY kuamua kuishabikia CCM na Samia, kisiasa, kifalsafa, kichawa, bado silioni.
Naona watu wanamlazimisha mtu aliyechagua upande anaoutaka yeye asichague upande huo tu.