Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Jitu unaliheshimu Toka zamani halafu unakuja kuona linatuma post ya kikuda kama hili li KirangaKwanza kabisa hilo la kumnafikia mtu kwa sababu ya njaa ni vigumu kuliprove.
This is a contentious, argumentative and controversial claim.
Unaposema njaa una maana gani? Unaweza kuthibitisha AY ana njaa hivyo?
Pia, kumuita mtu mnafiki ni judgement call. Unafiki wa AY uko wapi? Kuna siku AY aliwahi kujitambulisha kuwa yeye ni msanii activist wa upinzani useme sasa kawageuka wapinzani kinafiki? AY mbona hata kwenye muziki amejitambulisha yeye ni "Mzee wa Commercial"?
Na hata kama kageuka, utajuaje kwamba kageuka kinafiki na si kwa kuona kweli kuwa matumaini ya maendeleo ya Tanzania yapo CCM?
Unaposema huyu chawa mnafiki, unahakikishaje huyu ni chawa mnafiki na si mtu tu ambaye kaona CCM, pengine pamoja na mapungufu yake yote, bado ndiyo chama sahihi kwake kuongoza nchi?
Mimi si mwanachama wala shabiki wa CCM au Samia, lakini naona kama mnaingilia uhuru wa watu kuamua wanataka ku support chama na mwanasiasa gani.
Hii ni haki yao ya msingi ya kiraia, kikatiba na kibinadamu. Na kwa kuwa ni haki ya msingi hivyo, hamna haki kuwaingilia watu katika haki hiyo.