Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Yes mkuu mpira watu wengi hatuujui ndio maana huwa tunaishia kutoa lawama tu.

Mpira una mambo mengi sana kwa jicho la kawaida la mashabiki hawawezi kuona na kuelewa kinachoendelea wao wanajua tu goli ndio mpira.
 
Uliposema mugalu anabebwa na matokeo mazuri ya simba kama kuna mtu hajakuelewa atakuwa ni mcha mbuzi. Hata siku ya prison aliyesabisha droo ile ni mugalu
Kosa nafasi nyingi za wazi jumlisha na penati. Simba ingepata strike mzuri kombe hili la caf wangechukua maana idara zote wako vyema tatizo mugalu
 
Kaka hyo ni app gan ?
 
Wapenzi wa Mugalu wanasema eti Mugalu kasajiriwa kama.
"Mshambuliaji mkabaji"
Na sio mshambuliaji mfungaji.

Hivi unafika Fainali ya CAF na una mshambuliaji Mugalu.
Anakosa nafasi nne za wazi. Wapinzani wanapata moja wanachukua ubingwa.

Kati ya washambuliaji wabovu waliowahi kusajiriwa Simba Mugalu anaongoza.
Mugalu yeye na goli mita tatu anapiga mpira nje kwenye kibendela cha kona.
Anapiga mpira huku amefumba macho yeye na goli.
Kinacho mmbeba Mugalu ni wachezaji wazuri wa Simba

Poleni mnaopoteza muda kumsifia Mugalu.
 
Mbali na Mugalu na Mkude mwingine ambaye haeleweki ni Dilunga anapoanza au kuingia hana impact yoyote ila mara nyingi anapewa nafasi
 
Mugalu tumepigwa jamani....anaingia kwenye kikosi kwa sababu mwalimu hana chaguo lingine... Kagere hafai...Bocco uwezo umeshuka....Simba ingekuwa na angalau Kama yule mcongo alikuwa kwa wapinzani zetu...."Makambo"....timu ingekuwa hatari zaidi kuliko hii ya Mshabuliaji Mugalu....Benchi la ufundi wajipange kutafuta mshabuliaji wa uhakika... nafasi tatu goli mbili.
 
Mbali na Mugalu kukosa nafasi za wazi pia ni majeruhi mara kwa mara kama Boko Simba wawe makini tunahitaji mshambuliaji makini timu inatengeneza nafasi nyingi lakini hazitendewi haki
 
Nimekuelewa sana mtoa mada..shida sasa kwa sasa Simba hatuna strijer wa maana kule mbele..hata huyo kagere amebaki kuwa mviziaji tu.
 
Mkuu utamaliza mate yako bure ...we mpotaezee ila tuliona mpira na kuufuatlia bila ushabiki tunaelewa ulichosema.
 
Mbali na Mugalu kukosa nafasi za wazi pia ni majeruhi mara kwa mara kama Boko Simba wawe makini tunahitaji mshambuliaji makini timu inatengeneza nafasi nyingi lakini hazitendewi haki
Na nadhani tatizo kubwa ni majeruhi....anacheza kwa tahadhari....wasiguse pacha yake....hata Bocco tatizo kubwa ni majeruhi....Kagere control ndogo.... kwa kifupi Simba bado inahitaji Mshabuliaji wa uhakika....wa kiwango cha kina Luis na Chama....kosa moja goli moja.
 
Mbali na Mugalu na Mkude mwingine ambaye haeleweki ni Dilunga anapoanza au kuingia hana impact yoyote ila mara nyingi anapewa nafasi
Dilunga ni mmoja wa wachezaji wa kawaida sana sana sana wanaocheza timu kubwa...sionagi kipaji chochote kwa yule jamaa
 
Duuu!!! Tumheshimu mchezaji aliyetupa furaha kwa miaka 2 mfululizo. Kagere amecheza match ngapi full time za ligi hadi afikishe goli 9.

Binafsi,Kagere ni mchezaji mzuri,anayeliona lango vyema,asiyekata tamaa na kuna magoli magumu anayoweza kufunga.

Simba imuache aende Yanga then tutajua habari yake.
 
Kagere anaathiriwa na mfumo na kuwekwa benchi na Kishingo kwa kifupi kishingo kaua morali ya wachezaji wengi kwa kuwaweka benchi bila sababu akiwemo Kahata
 
Kwa level ya ligi yetu ya ndani Kagere ni mchezaji mzuri sana tu.... Na ni kweli amekuwa mfungaji Bora wa ligi kwa misimu miwili........ni mzuri akiwa kwenye sita....nje ya sita.....hana madhara....uwezo wa kukaa na mpira pia hatuko vizuri....aendelee kubaki Simba kwa ligi ya ndani....kimataifa tutafute mshabuliaji wa uhakika.
 
Hata kimataifa tulipoingia robo fainali ni yeye aliyetubeba tatizo ni namna ya kumchezesha
 
Hata kimataifa tulipoingia robo fainali ni yeye aliyetubeba tatizo ni namna ya kumchezesha
Kipindi cha Uchebe- alikuwa anaweka washambualiaji wawili...na ndio mfumo Kagere anafiti......ni mfumo mzuri Kama timu inashambulia....mkiwa mnashambuliwa unasumbua....maana kuwa na washambuaji wawili...Ina maana viungo wamepungua.
 
Kipindi cha Uchebe- alikuwa anaweka washambualiaji wawili...na ndio mfumo Kagere anafiti......ni mfumo mzuri Kama timu inashambulia....mkiwa mnashambuliwa unasumbua....maana kuwa na washambuaji wawili...Ina maana viungo wamepungua.
Mfumo huohuo tulishinda mechi zote Dar tatizo wakati wa Uchebe viungi wakabaji uwezo wao ulikuwa mdogo ndio maana Kotei aliachwa, Mkude alibakizwa kwa kigezo cha uzawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…