Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,021
- 79,710
Yes mkuu mpira watu wengi hatuujui ndio maana huwa tunaishia kutoa lawama tu.Simkubali mugalu hata kidogo kufunga magoli.
Umegusa maeneo yote muhimu kiufundi. Makocha kama mourinho wanatumia mfumo wa build from the back and safety first.. yaani move inanzia kutoka kwa beki-kati-forward-striker-goli, namfananisha mugalu na jesse lingard hawa muda wote wanachase mpira ndani ya final third na hivyo kusababisha mabeki wasiwe na utulivu muda wote na kuwa na hali ya Kuondoa hatari golini haraka na kupeleka kwenye usalama, kwahiyo move ya kutengeneza goli inaharibika na hivyo timu kushambuliwa mara chache sana.
Mkishambuliwa move ikiharibika mpira unarudishwa kwa mabeki ili wahold na wachezaji warudi kwenye position zao then move inaanza upya, sasa kama mbele kuna mkabaji mzuri anayewin mipira inakuwa ngumu kurudisha mpira na hivyo timu pinzani inacheza ikiwa na presha na disorganized muda wote. Tumeona vita hawakuwa na utulivu muda wote na baada ya mugalu na mkude kutoka vita walipata utulivu na kuwa organized kuliko kipindi cha kwanza
Kikingine wanawazuia mabeki kupanda mbele kuongeza mashambulizi. Simba imefanikiwa sana hapa.
Kuna vitu vingi vinatokea uwanjani lakini huwezi kujua sababu ni nani
Mpira una mambo mengi sana kwa jicho la kawaida la mashabiki hawawezi kuona na kuelewa kinachoendelea wao wanajua tu goli ndio mpira.