Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Umenikumbusha kipindi cha Alex Ferguson wakati akimtumia Shaba Ranks Danny Welbeck.
Welbeck alikuwa anakosa magoli sana yaani kama Mugalu hivi. Lakini alikuwa anatimiza majukumu yote kama ulivyoelezea hapo juu. Nakumbuka Fergie aliulizwa kuwa kwasasa ni mchezaji gani ambae anacheza kama unavyoaagiza bila kusita alisema Danny Welbeck.
 

Mkuu una msimamo thabiti ila argument zako sio za kiutu uzima.

1. Umesema kwenye mfumo wako utamtumia Kagere over Mugalu, wakati huo huo unasema Gomez anamtumia Mugalu kwa sababu Kagere amejiishia (kaisha). Maana yake wewe ungemtumia mshambuliaji aliyejiishia.

2. Unaposema Simba haina mshambuliaji mahiri kwa sasa. Unaweza kuwa sawa au si sawa. Lakini hii sio hoja mezani, hoja iliyopo ni kati ya washambuliaji WALIOPO ni nani ana tija zaidi.

3. Dube na Azam yake wameshacheza mechi 25 za ligi. Simba na akina Bocco, Kagere na Mugalu wana mechi 20 tu za ligi.
Litakua ni jambo la ajabu sana kushangaa watu wenye mechi tano mkononi kuzidiwa magoli mawili au moja na mtu aliyewatangulia mechi tano (dakika 450).
Tena hawa wenye mechi tano mkononi Wako kwenye ''timu yenye safu kali zaidi ya ushambuliaji'' katika ligi husika.

4. Kwa maneno mengine ni kwamba wewe unahoji credibility ya Gomes, mtu ambaye yuko mazoezini na wachezaji. Yeye na benchi la ufundi wanapokuja na kikosi kitakachokwenda kutekeleza mpangokazi uwanjani, Mugalu anaoangwa ''on merit'' sio kwa rushwa, uzuri wa sura, kujuana n.k.

NB: Naheshimu sana maoni yako, sifurahishwi na mshambuliaji (yeyote) kukosa magoli. Ila ninachoweza kukuhakikoshia ni kwamba Gomez atakukera sana msimu huu (Kama unakereka na chaguo lake kwenye eneo la mshambuliaji). Na ndio maana nikasema wewe na ''kocha mwenzio'' Gomez, mnatofautiana kwenye misingi (principles). Wewe uko sahihi, yeye yuko sahihi.
 
hasira za nini bwasheee??
tuliza mihemko

mimi kwa maoni yangu kwa mfumo wa Da Rosa chaguo la kwanza ni Mugalu alafu Bocco ndo huyo Kagere wako ambaye ni mtu wa kuvizia vizia uwanjani na kukimbia kimbia hovyo.

Kunywa chai
Sio Ditram Nshimbi? Maana nimegundua hii maada inachangiwa pia na utopolo walioamua kujifanya mashabiki wa Simba.Shabiki wa Simba anaeitakia mafanikio,hawezi kutaka timu yake iridhike na mchezaji wa aina ya Mugalu.

Yani kwamba Mugalu anazuia mabeki kupanda kushambulia? Umesahau kazi ya Djuma kule Congo, ilivyosababisha Miqiusone arudi nyuma kumsaidia Zimbwe,huyo Mugalu alikuwa wapi?? Mshambukiaji akiwa sharp magoli lazima yapatikane kulingana na nafasi zinazotengenezwa . Nakumbuka ile Yanga ya Zahera iliyokuwa na viungo wabovu, ila kazi ya Makambo ilionekana, na ndie aliachangia wao kumaliza katika nafasi ya pili.

Hebu fikiria yule Makambo wa kipindi kile,ndo angekuwa kwenye timu inayotengeneza nafasi nyingi kama simba.

NB;Kiufupi Mugalu ni striker butu,acheni kumpamba ovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wewe jamaa kabla ya kuangalia pass acculacy angalia zone ambayo mchezaji anacheza, kuna asilimia 3% hadi 5% ya kupoteza pasi ukiwa upande wako (zone yako). Pia mpaka 40% ukiwa kati kati ya uwanja. Mpaka 70%ya kupiteza mpila ukiwa kwenye zone ya adui, simply ni rahisi kufanikisha pass, drible, hata kupokonya mpila ukiwa kwenye zone yako hadi katikati ya uwanja. Yaani ni uchizi kutaka statistic za mugalu na thadeo. Ndio maana timu inaproduce offtaget nyingi kuliko on target. Inafikia hadi 13(2) haushangai? Nenda na fact basi kidogo. Yaani mugalu anacheza kwenye zone ya mpinzani unategemea awe na acculate pass ya 80-90% kama thadeo?
 
Sina hasira yoyote.
Nilielewa mshambuliji jukumu lake ni kufunga magoli.
Hayo mambo mengine sikuwa nayaelewa.
Asante kwa kunifahamisha.
Hata tukimpima kwa takwimu za kufunga huyo Mugalu, sidhani takwimu zake ni mbaya sana. Leading scorer kwenye mashindano ya CAF ana magoli matatu, yeye anayo magoli mawili (pungufu ya goli moja). Sidhani kama hizi ni ''takwimu mbaya sana'' kama ambavyo unataka umma uamini.
 
Mpira sio mpila. Unatatizo la R
 
Gomez anafanya hivyo kwakuwa hana jinsi.
Nakuhakikishia, Mugalu ukiisha mkataba wake kama uchezaji wake utabaki huohuo wa kukaba badala ya kufunga magoli, basi utumishi wake Simba utaishia hapo.
Namaanisha jinsi Mugalu anavyocheza sasa hawezi kuongezewa mkataba hapa Simba.

Simba kwa sasa haihitaji sababu, au Mkabaji wapo wakabaji na Fraga anakuja kusaidia, Sumba inamhitaji mshambuliaji mahiri wa kufunga magoli.

Katika Mechi za Clab Bingwa nafasi moja ni muhimu sana.
Simba inahitaji mtumiaji sahihi wa nafasi hiyo moja, ambaye hayupo.

Kama Mugalu Mkabaji mzuri sawa tu kwakuwa Simba inahitaji mtu kama yeye pia.

Ila bado Simba kuna pengo la mfungaji mahiri, ndiye ninayemzungumzia hapa na sio Mugalu.
 
Gomez anafanya hivyo kwakuwa hana jinsi.
Nakuhakikishia, Mugalu ukiisha mkataba wake kama uchezaji wake utabaki huohuo wa kukaba badala ya kufunga magoli, basi utumishi wake Simba utaishia hapo.
Namaanisha jinsi Mugalu anavyocheza sasa hawezi kuongezewa mkataba hapa Simba.

Simba kwa sasa haihitaji sababu, au Mkabaji wapo wakabaji na Fraga anakuja kusaidia, Sumba inamhitaji mshambuliaji mahiri wa kufunga magoli.

Katika Mechi za Clab Bingwa nafasi moja ni muhimu sana.
Simba inahitaji mtumiaji sahihi wa nafasi hiyo moja, ambaye hayupo.

Kama Mugalu Mkabaji mzuri sawa tu kwakuwa Simba inahitaji mtu kama yeye pia.

Ila bado Simba kuna pengo la mfungaji mahiri, ndiye ninayemzungumzia hapa na sio Mugalu.
 
Yaani huyo mwenye 3 angepata nafasi za Mugalu angekuwa na goli 8 sasa hivi.
 
Mkuu walio wengi mpira wanaangalia au kuuongelea Kwa mihemko Tu na sio uhalisia au inavotakiwa kuwa. Utajikuta unachoma calories za kutosha kujaribu kumuelewesha mtu kumbe mwenzako anabishana, maana kuna tofauti ya kueleweshana na kubishana, so watu wa kubishana sio watu wa kuchoma calories zako ata kama ni Kwa nia njema, Achana nae atakuja kuelewa mbele ya safari
 
Asante sana Mkuu.
Hapa tunazungumzia mshambuliaji mahiri, nafasi ambayo bado Simba haijapata mtu sahihi.
Mi nashindwa kuwaelewa kwamba wanampa sifa gani Mugalu.

Sifa ya mfungaji mahiri au ya Mkabaji mahiri.
Kama anapewa nafasi ya Mkabaji basi wakubali kwamba sio mshambuliaji.

Mi nazungumzia mshambiliaji stadi. Na sio Mkabaji.
Katika fani ya ushambuliaji huyu Mugalu ni Butu.
Hakuna cha kupepesa macho.
 
Siku akipoteza nafasi zaidi ya Tano kama zile alizopoteza wakati tunacheza na Merikh na As vita pale Taifa, kwenye Mechi muhimu ambazo tunahitaji ushindi Kisha tukafungwa na kutolewa ndo mtakuja kukubaliana na sisi humu.


Tena kwa hii hatua ya mtoano inayohitaji wingi wa magoli zaidi ya point 3 (robo na nusu fainali),eti ndo tumeenda ugenini tunapata nasafi za wazi zaidi ya Tano tunaziacha, kisa tuna "mshambukiaji mkabaji" tutakuja kupoteana humu. Ukweli usemwe Simba Sc kwasasa inahitaji mshambukiaji mahiri pale mbele, maana Si Mugalu wala Kagere wanaotosha wote ni viazi tu kwa Sasa ingawa nampa heshima yake Kagere kwa huduma yake tukufu pale Msimbazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nilidhani tunazungumzia CURRENT SITUATION, kwamba kwa washambuliaji waliopo sasa hivi ni kwanini Mugalu anaanza over hao wengine. Hoja zangu zilijikita hapa.

Ila kama mjadala ulihusu mambo ya baada ya msimu kuisha nani abaki nani atafutiwe mbadala, hapo naungama na wewe kwamba tunatakiwa kutafita better option kwenye eneo la ushambuliaji kuliko hawa tulionao.

NB: Nina uhakika hiki sicho tulichokua tunakijadili hapa.
 
Hii lugha ya Mugalu kuwazuia mabeki wa timu pinzani wasipande sijui imetokea wapi!!
Mechi ya As Vita Vs Simba kule Congo Mugalu alikuepo na wing backs wa As Vita walikua wakipanda kushambulia akiwepo na yule beki wao kile kiandunje Shabani.
hii ni capatin wa vital akimwongelea mugalu kuhusu mechi yao ya kwanza.
 

Hii inaitwa from a layman's eye.
Wana kamsemo kao kwamba ''mpira wote tunauona''
Ipo tofauti ya kuona na kutambua.
Kuna watu wanafanya kazi ili mambo yaonekane vile yanavyoonekana.
Wadau wanaamini Mugalu anapendelewa na zile nafasi zinazopatikana ni kwa sababu yeye ana bahati kuliko Kagere na ndio maana kwenye hoja zao wanasema ''Kama zile nafasi ambazo anapata Mugalu, angepata Kagere basi tungeshinda magoli....''

Wanasahau kwamba kuna utaratibu wa kuzitengeneza hizo nafasi. Jamani katika mpira wa miguu, scoring chances are created, sasa hawa ndugu wanadhani kwamba MNAZAWADIWA.
 
Hapa nime kopi na ku pest, hoja ya mtoa mada hii. Unaweza kuipitia hasa aya ya kwanza na ya tatu ya mtoa mada.

"Mimi ni shabiki wa mpira na mpira ninaujua kwa kuutazama na kuucheza uwanjani. Haiitaji elimu kubwa kugundua kuwa Chris Mugalu hafai na hastahili kuanza kikosi cha kwanza kulingana na kiwango chake hasa uwezo wake wa kufunga. Bahati nzuri kwake ni kuwa udhaifu wake unafichwa na ubora wa timu.

Na kwa bahati mbaya zaidi wachambuzi wengi wa soka hapa bongo wamekuwa na 'upofu' katika uchambuzi. Analysis zao nyingi zina base kwenye matokeo. Mfano, hata kama timu ikicheza ovyo kwa dk zote 89, ila ikapata goli na kushinda dakika ya 90..Basi tegemea analyis positive kutoka kwa wachambuzi wetu.. Vice versa is true.

Vivyo hivyo kwenye swala la Mugalu, wachambuzi wetu hawajui chochote kuhusu soka. Hata uchambuzi wao juu ya viwango vya wachezaji umemezwa na matokeo ya timu. Wengi utawasikia kuwa Mugalu ni striker mwenye uwezo wa kuhold mpira na kufungua nafasi kwa wengine. Hawazungumzii kabisa ubutu wake golini.

Na mbaya zaidi wachambuzi karibu wote wana copy na kupaste opinions zao zinafanana. Katika kipindi hiki, huwezi kuta wachambuzi wanajadili weaknesses za Mugalu, badala yake wanaelezea umuhimu wake na faida yake kule mbele.Najiuliza, Hivi kama hafungi, ana umuhimu gani sasa wa kuanza?, na je kama timu isingekuwa inapata matokeo na bado Mugalu angekuwa anapoteza zile nafasi, bado wasingemuelezea udhaifu wake?...Jibu ni rahisi tu, wana chambua kulingana na matokeo.

Mfano wa pili, ni Jonas Mkude. Kwa mtu anaejua mpira na aliyeangalia ile game, ilikuwa sio rahisi kuamini kama Mkude angerudi uwanjani second half..Alikuwa flopy sana siku ile.

Cha ajabu timu imepata matokeo kwenye comments unasikia uchambuzi kuwa Mkude alifanya majukumu yake vizuri na aliiunganisha vizuri sana safu ya ulinzi na ushambuliaji..Hivi ni mkude huyu huyu aliyekuwa na pass accuracy mbovu kuliko wachezaji wote wa simba siku hiyo? Ina maana wachambuzi hamuoni udhaifu wa wachezaji kisa tu timu imepata matokeo?

Basi kama ni hivyo, hakuna kazi rahisi kama kucwa mchambuzi wa soka bongo."
 
sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…