Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Ni kweli timu inahitaji magoli mengi katika hatua hii (na hatua nyingine yoyote ile ya mashindano). Hata Kama magoli Hayo atafunga Wawa na Kapombe, basi hewala. Sioni hoja ya msingi hapa kwamba ni nani afunge nani asifunge. Cha msingi ni magoli hata kama yote atafunga Miquissone sawa tu.

Mchezaji mwenye magoli mawili kwenye mashindano ambayo mwenye magoli mengi zaidi ana magoli matatu, anawezaje kuwa si mfungaji mzuri ?
Nielimishe hapa.

Hayo mambo ya kuimbwa na mashabiki au kuwapo kwenye kikosi bora cha wiki sidhani kama yana mashiko sana. Kikosi cha wiki kinachukua wachezaji wachache mmno kati ya kundi kubwa. Hoja yetu isijikite kwenye muktadha huu maana nitakuuliza kwamba Onyango hajawahi kuwa kwenye kikosi bora cha wiki, ina maana ni mchezaji wa hovyo ?

Pia naomba tuzungumzie current situation, hayo ya Simba inahitaji mshambuliaji mwingine sidhani Kama yana msaada wowote kwenye hoja iliyopo mezani. Maana hata iweje, Simba haiwezi kumpanga Prince Dube, Simon Msuva wala Erasmus wa Mamelodi kwenye mechi ijayo ya robo fainali. Ni ama Bocco, Kagere au Mugalu. Tujadili hili
Ngoja nicheke kwanza[emoji23][emoji23][emoji23]. Hao wenye magoli matatu mbele ya Mugalu, nina uhakika kama wangekuwa subjected kwenye nafasi za wazi kabisa alizopata Mugalu basi wangekuwa na magoli hata 6 au 7 kabisa, maana ukiangalia jamaa amekosa nafasi za wazi zaidi ya 11 emagine[emoji23][emoji23][emoji23].

Lakini pia tusisahau kuwa goli moja Kati ya hayo mawili ni la penalty, na hata hilo jingine halikuwa na skills zozote za maana.Hebu angalia magoli ya miquisone na Chama, unaona kabisa ni ya skills za kiwango cha juu,mpaka yanaingia katika kinyang'anyiro cha magoli bora ya mashindano. Ukweli usemwe Mugalu hana kiwango kinachotosha yeye kucheza Simba,ni vile tu kocha hana namna.

Alafu sikuelewi kabisa unaposema kuwa, eti swala la wachezaji kuingia kwenye vikosi vya wiki na kushindanishwa katika ubora wa magoli ni maswala ya kishabiki. Hebu niambie hapa ni wapi huko ambako ubora wa mchezaji hauhusianishiwi na takwimu na maoni mbalimbali ya mashabiki? Maana hata BaronDo(sijui inaamdikwaje),ni matokeo ya takwimu na maoni pamoja na kura za mashabiki, au wewe unataka Mugalu apimwe kwa Kipi? [emoji23][emoji23]

Ukweli usemwe, Mugalu ni mshambuliaji wa kiwango cha chini sana. Unasema hakuna striker mzuri afrika, hatukatai ila sio kwa kiwango hicho cha Mugalu Sasa, Hebu jaribu kulinganisha uwezo wa Makambo(aliyewahi kuwa striker wa yanga) au Dube na huyo Mugalu wako. Yani kama yule Makambo au huyu Dube, wangekuwa kwenye hiki kikosi kinachotengeneza nafasi nyingi hivi wasingekuwa kama huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefanya vema katika kutoa maoni kwa kuambatanisha marejeo.

Mi nauliza.
Hivi kwanini hapa watu wanakwepa kuzungumzia madhaifu ya Mugalu ?

Kweli anacheza vizuri, kweli Anasaidia timu.
Mbona akina Chama Bwalya huwa madhaifu yao yanajadiriwa hapa na yanapelekea hadi kujirekebisha na wanafanya vizuri sasa.

Huyu Mugalu yeye ni nani hadi ajadiriwe kwa mazuri yake tu.

Ukigusa udhaifu wake basi unashambuliwa kwamba hujui soka wewe.

Nini iko Shida ?

Mkuu, kwani wewe unaelewaje kuhusu kujadili mapungufu ya mchezaji ?
Maana watu kibao hapa wanamsema kwamba anatakiwa ajifue zaidi kwenye finishing yake ili uwezo wake wa kubadili nafasi kuwa goli (chance to goal) uongezeke kwa manufaa ya timu hasa kwenye hizi hatua.

Au huko sio kuongelea mapungufu yake ?

Concern ya watu ni pale ambapo wengine wanasema Mugalu hafasi kuanza (na hiki ndio kitu huu uzi unahusu) na achezeshwe Meddie.

Kinachojadiliwa hapa ni kwamba ukifanya cost-benefit analysis ya mfumo wa Simba, ni afadhali Mugalu aanze dhidi ya Meddie kuliko kinyume chake.
Sidhani kama kusema hivyo inamaanisha unafurahishwa na Mugalu kukosa magoli au ni kumfichia makosa mtu huyo.
 
Mchambuzi wa mpira ni poa akiwa mtu ambaye alishaucheza kama kina MICHAEL OWEN, IAN WRIGHT, RIO FERDINAND, ALLY MAYAI na wengine. Sio mtu hata danadana moja hawezi lakini anafosi kuwa pundit.
Waganga njaa tu hao,na hata humu nawaona.Ndo hao wanaotaka kutulazimisha et Mugalu ni striker bora kwenye ligi kuu Tanzania[emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagere ni mzuri kufunga kuliko Mugalu..na analingana kwa sifa zilizobaki na mugalu na kikubwa zaidi kagere ana kasi kuliko mugalu.

Anyway, mkuu ID yako na coment yako nimeisave. Muda ni mwamuzi mzuri namimi sitasita kukukumbusha.
Sikia ni hivi

Kagere hawezi cheza kama lone striker anafit kucheza na mshambuliaji nyuma yake

Kwa aina ya mfumo wa simba kagere ni ngumu kuanza kwa sababu hana uwezo wa ku link kwenye build up tofauti na mugalu na bocco

Kwani kagere kaanza kuwekwa nje leo? Si hata sven alimuweka nje bocco akawa anaanza

Mugalu na bocco ndio wana good linking play kwenye buuld up

Juzi tu hapa umeona game ya al ahly kagere akawa anazunguka tu hana uwezo wa kuhold mpira na kusubiri wachezaji wengine waje manake timu isogee kwake imkute na mpira ni tofauti kwa mugalu na bocco wao huo uwezo wanao

Kagere anaweza kucheza aina moja tu ya soka anaweza kucheza direct football tu na hawezi kucheza vzr kwenye timu inayofanya build up

Na saiv simba impunguze mmoja kati ya Bwalya miquissone au chama kwa ajili ya kagere tu? Hapana

Kagere ni mchezji bora sana ila kwa maslahi ya timu lazima asubirir
 
Mkuu, kwani wewe unaelewaje kuhusu kujadili mapungufu ya mchezaji ?
Maana watu kibao hapa wanamsema kwamba anatakiwa ajifue zaidi kwenye finishing yake ili uwezo wake wa kubadili nafasi kuwa goli (chance to goal) uongezeke kwa manufaa ya timu hasa kwenye hizi hatua.

Au huko sio kuongelea mapungufu yake ?

Concern ya watu ni pale ambapo wengine wanasema Mugalu hafasi kuanza (na hiki ndio kitu huu uzi unahusu) na achezeshwe Meddie.

Kinachojadiliwa hapa ni kwamba ukifanya cost-benefit analysis ya mfumo wa Simba, ni afadhali Mugalu aanze dhidi ya Meddie kuliko kinyume chake.
Sidhani kama kusema hivyo inamaanisha unafurahishwa na Mugalu kukosa magoli au ni kumfichia makosa mtu huyo.
Kwahiyo unakubali kwamba Mugalu ni striker butu,ila anacheza kwakua kocha hana namna?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi tufanye Mugalu is Excellent katika majukumu yake ya ushambuliaji.
Tuendelee kujadiri ubora wake katika timu ya Simba.
Mkuu kwani wewe unaamini katika individuality ?
''Nini kimefanyika'' huwa haikuhusu sana bali ''nani amefanya'' ndio muhimu zaidi ?

Idara ya ushambuliaji ya Simba akiwepo Mugalu inatengeneza nafasi nyingi za kufunga na hivyo inakua fanisi zaidi.

Idara ya ushambuliaji ya Simba ikiwa na Kagere, inatengeneza nafasi chache na hivyo inapunguza ufanisi.

Inaonekana wewe hujali kabisa kuhusu hayo mawili, kitu pekee unachojali ni kwamba Je, kati ya Kagere, Mugalu au Bocco, wakipata nafasi za kufunga zinazofanana ni nani (individual) atafunga zaidi.

Nitakua niko sawa kama nikidhani kwamba hivyo ndivyo unaamini (individual brilliance matters the most)
 
Hatua tuliyofika CCL kwa sasa (robo na nusu fainali),ni hatua inayohitaji wingi wa magoli zaidi ya point 3,Ili kijihakikishia nafasi ya kusonga mbele ila siyaoni hayo magoli kwa Mugalu. Ukweli ni kwamba kwa asilimia kubwa, Simba inashinda kwa skills na magoli ya midfielders na sio uwezo wa Mugalu kutulia na mpira akisubiri timu ipande, kama ni hivyo tungeona ana idadi kubwa ya assist lakini hana. Sasa kama hafungi, hana assist za kutosha anafaida gani mbele? Kama sifa yake kubwa ni kukaba, basi yule no beki na sio mshambuliaji kama yalivyo majukumu yake.

Kuna wengine hapa wanasema sijui mfumo sijui nini, angalieni hata mechi za Ligi kuu, Tangu Gomez awe mocha mkuu, na kumtumia Mugalu mtagundua kuwa kuwa Asilimia kubwa ushindi wa simba umekuwa ni wa Goli moja moja licha ya kutengeneza nafasi nyingi, ambazo mwisho wa siku Mugalu huzigeuza kuwa kosakosa langoni mwa wapinzani. Utakuta wafungaji ni akina Chama, Morrison, Miqiusone ambao wote hao ni mamidfilder. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa huyo anaesifiwa kuhold mipira kwenye 18,hahusiki sana kwenye hayo magoli ya hao mamidfilders[emoji23].

Ukweli usemwe bwana, Simba Sc inakosa mshambuliaji wa maana pale mbele. Kule kwenye page za Caf wanatamba Miqiusone Na Chama na hata kwenye kikosi cha wiki wanaingia hao , inamaana wao hawaoni uwezo wa Mugalu kukaba kama nyinyi mnavyopiga kelele humu,au wao hawajui hilo soka la kisasa,kwamba nyie ndo mnalijua sana [emoji1][emoji1][emoji1]? Na hata asilimia kubwa ya mashabiki wa Simba utawaona wanajivunia Chama,na Miqiusone na sio Mugalu. Leo hii watu wamemsahau Okwi na mkude kwasababu ya performance ya Miqiusone na Lwanga,ila bado wanamiss Fraga ambae ni majeruhi ,kwa sababu hilo garasa Mugalu Galina chochote cha ku-offer kwenye team.

Huyu Mugalu atakuwa kawaroga,sio bure.Ile mechi na As vita kwa mkapa,kama tungefungwa na kutolewa, kwa zile nafasi alizopoteza,sidhani kama mngekuja na huu utetezi wenu. Nilichogundua ushindi wa Simba sc ndio unaowapa upofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
umemaliza kila kitu..simba kuanza na Mugalu ni sawa na kuanza na wachezaji 10.5.....Muda ni mwamuzi mzuri sana, kuna siku watu watazikana hoja zao humu...ushindi wa simba ndio unawapa upofu
 
Ngoja nicheke kwanza[emoji23][emoji23][emoji23]. Hao wenye magoli matatu mbele ya Mugalu, nina uhakika kama wangekuwa subjected kwenye nafasi za wazi kabisa alizopata Mugalu basi wangekuwa na magoli hata 6 au 7 kabisa, maana ukiangalia jamaa amekosa nafasi za wazi zaidi ya 11 emagine[emoji23][emoji23][emoji23].

Lakini pia tusisahau kuwa goli moja Kati ya hayo mawili ni la penalty, na hata hilo jingine halikuwa na skills zozote za maana.Hebu angalia magoli ya miquisone na Chama, unaona kabisa ni ya skills za kiwango cha juu,mpaka yanaingia katika kinyang'anyiro cha magoli bora ya mashindano. Ukweli usemwe Mugalu hana kiwango kinachotosha yeye kucheza Simba,ni vile tu kocha hana namna.

Alafu sikuelewi kabisa unaposema kuwa, eti swala la wachezaji kuingia kwenye vikosi vya wiki na kushindanishwa katika ubora wa magoli ni maswala ya kishabiki. Hebu niambie hapa ni wapi huko ambako ubora wa mchezaji hauhusianishiwi na takwimu na maoni mbalimbali ya mashabiki? Maana hata BaronDo(sijui inaamdikwaje),ni matokeo ya takwimu na maoni pamoja na kura za mashabiki, au wewe unataka Mugalu apimwe kwa Kipi? [emoji23][emoji23]

Ukweli usemwe, Mugalu ni mshambuliaji wa kiwango cha chini sana. Unasema hakuna striker mzuri afrika, hatukatai ila sio kwa kiwango hicho cha Mugalu Sasa, Hebu jaribu kulinganisha uwezo wa Makambo(aliyewahi kuwa striker wa yanga) au Dube na huyo Mugalu wako. Yani kama yule Makambo au huyu Dube, wangekuwa kwenye hiki kikosi kinachotengeneza nafasi nyingi hivi wasingekuwa kama huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena Vema sana.

Tatizo Simba ya sasa haina mshambuliaji mwenye kiwango cha hao uliowataja.

Kwa kiwango cha Simba cha sasa ambacho Al-Ahally wakiwa nchini kwao na kwenye uwanja wao, inafikia mda wanalinda goli lao moja.
Na wanashambuliwa mda wote golini huku kocha wao hana amani.
Ni hatua nzuri sana waliyoifikia Simba.
Hiyo nafasi ya Mugalu hata kama angesimama Bonge Morringa, wacha huyo Makambo.
Saizi angekuwa na goli nyingi sana Club Bingwa na kwenye ligi.

Hii inatoka na uwezo wa Simba wa sasa ambao hao Al-Ahally wako nafasi ya pili.
Simba anaongoza sio kundi lake tu bali anaongoza katika pointi za juu timu zote zilizoingia robo fainali Afrika.
Angesimama mtu kama Makambo hapo mbele ingekuwa balaa kubwa zaidi.
Anyway kwa sasa tunaye Mugalu.
Hatuna namna nyingine.
 
Kwahiyo unakubali kwamba Mugalu ni striker butu,ila anacheza kwakua kocha hana namna?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo mkuu unataka nafasi ya Mugalu acheze Harry Kane ?
Maana nakwambia kwa washambuliaji waliopo Simba na mfumo unaotumika huyu mtu ndio sahihi zaidi.
Mimi binafsi siwezi kusema mshambuliaji huyo ni butu kwa sababu ana magoli mawili Champions league (mwenye mengi zaidi anayo matatu). Labda unaweza kunipa stastical definition ya mshambuliaji butu.

Ninachoweza kusema ni kwamba nakasirishwa na mshambuliaji kukosa magoli, japokua hakuna mshambuliaji asiyekosa magoli at all. Ingekua hivyo basi soka lingekua Kama basketball.

Kama kuna takwimu zinazoelezea ubutu wa mshambuliaji huyu naomba uziweke hapa.
 
umemaliza kila kitu..simba kuanza na Mugalu ni sawa na kuanza na wachezaji 10.5.....Muda ni mwamuzi mzuri sana, kuna siku watu watazikana hoja zao humu...ushindi wa simba ndio unawapa upofu
Mkuu unaposema ''Ushindi wa Simba ndio unawapa upofu'' wakati hiyo Simba iliyopata huo ushindi na Mugalu yumo humo humo uwanjani, Unamaanisha nini ?

Au nawewe ni wale ambao huwa wanasema ''Yaani Simba leo imshukuru Manula, vinginevyo ingefungwa''
Utafikiri huyo Manula ni mchezaji wa Mlandege ya Kijitoupele Zanzibar.
 
Naunga mkono hoja, wachambuzi wa bongo wengi ni bendera fuata upepo

Wanashindwa kujifunza hata vitu basic vya uchambuzi kutoka nje ya nchi (Ulaya)

Kitu nilichogundua Wachambuzi wengi wa bongo hawawezi kupiga mpira hata danadana 5 na wachambuzi wakubwa wa nchi za wenzetu wamecheza katika top top level, kama hawajacheza basi katika maisha yao yote wamejihusisha na soka kwa ukaribu sana
 
Mkuu kwani wewe unaamini katika individuality ?
''Nini kimefanyika'' huwa haikuhusu sana bali ''nani amefanya'' ndio muhimu zaidi ?

Idara ya ushambuliaji ya Simba akiwepo Mugalu inatengeneza nafasi nyingi za kufunga na hivyo inakua fanisi zaidi.

Idara ya ushambuliaji ya Simba ikiwa na Kagere, inatengeneza nafasi chache na hivyo inapunguza ufanisi.

Inaonekana wewe hujali kabisa kuhusu hayo mawili, kitu pekee unachojali ni kwamba Je, kati ya Kagere, Mugalu au Bocco, wakipata nafasi za kufunga zinazofanana ni nani (individual) atafunga zaidi.

Nitakua niko sawa kama nikidhani kwamba hivyo ndivyo unaamini (individual brilliance matters the most)
Katika mechi ya nyumbani na AS Vita, Mugalu alivyotolewa yakapatikana magoli mawili ya haraka haraka matokeo yakawa 4 : 1

Hiki ndicho tunachokiongela hapa.
Sio kweli Simba bila Mugalu inakosa Team building from behind to
foward.
Sub yake ilikuwa Supper Sub.
Mpira wa sasa hivi unahitaji Nguvu Kasi na akili.
Mugalu ana nguvu na kidogo kasi, ila kwenye kutumia akili kidogo ana mapungufu.
 
Umenena Vema sana.

Tatizo Simba ya sasa haina mshambuliaji mwenye kiwango cha hao uliowataja.

Kwa kiwango cha Simba cha sasa ambacho Al-Ahally wakiwa nchini kwao na kwenye uwanja wao, inafikia mda wanalinda goli lao moja.
Na wanashambuliwa mda wote golini huku kocha wao hana amani.
Ni hatua nzuri sana waliyoifikia Simba.
Hiyo nafasi ya Mugalu hata kama angesimama Bonge Morringa, wacha huyo Makambo.
Saizi angekuwa na goli nyingi sana Club Bingwa na kwenye ligi.

Hii inatoka na uwezo wa Simba wa sasa ambao hao Al-Ahally wako nafasi ya pili.
Simba anaongoza sio kundi lake tu bali anaongoza katika pointi za juu timu zote zilizoingia robo fainali Afrika.
Angesimama mtu kama Makambo hapo mbele ingekuwa balaa kubwa zaidi.
Anyway kwa sasa tunaye Mugalu.
Hatuna namna nyingine.
Lakini kuna watu wanasema, Eti Mugalu ni striker bora[emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na kocha wa simba nani anajua mpira?

Kama kocha wa simba anaona mugalu ndie best striker kuanza.. wewe nani umuone hafai..

Mpira wa ushindani mkali kama caf champions league usitegemee striker anaejua kufunga tu huku vingine hajui.. bali awe ana vya ziada vingii.. kama ball control, ball possession, na kusaidia kukaba na kuokoa kipindi ukiwa unashambuliwa... ni striker gani wa pale simba anamzidi mugalu kwa hizo factor zote...
Mugalu ni defensive striker

Naunga mkono hoja
 
Naunga mkono hoja, wachambuzi wa bongo wengi ni bendera fuata upepo

Wanashindwa kujifunza hata vitu basic vya uchambuzi kutoka nje ya nchi (Ulaya)

Kitu nilichogundua Wachambuzi wengi wa bongo hawawezi kupiga mpira hata danadana 5 na wachambuzi wakubwa wa nchi za wenzetu wamecheza katika top top level, kama hawajacheza basi katika maisha yao yote wamejihusisha na soka kwa ukaribu sana
Kuna kauli wanapenda kuitumia wachambuzi wa bongo, utasikia ENEO LA KIUNGO NDILO LITAAMUA MCHEZO, [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kagere ni mzuri kufunga kuliko Mugalu..na analingana kwa sifa zilizobaki na mugalu na kikubwa zaidi kagere ana kasi kuliko mugalu.

Anyway, mkuu ID yako na coment yako nimeisave. Muda ni mwamuzi mzuri namimi sitasita kukukumbusha.
Ukweli ni kwamba Mugalu anavumilika kwa sasa kwa sababu timu inapata matokeo

Time is a good teacher
 
Back
Top Bottom