Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Ngoja nicheke kwanza[emoji23][emoji23][emoji23]. Hao wenye magoli matatu mbele ya Mugalu, nina uhakika kama wangekuwa subjected kwenye nafasi za wazi kabisa alizopata Mugalu basi wangekuwa na magoli hata 6 au 7 kabisa, maana ukiangalia jamaa amekosa nafasi za wazi zaidi ya 11 emagine[emoji23][emoji23][emoji23].Ni kweli timu inahitaji magoli mengi katika hatua hii (na hatua nyingine yoyote ile ya mashindano). Hata Kama magoli Hayo atafunga Wawa na Kapombe, basi hewala. Sioni hoja ya msingi hapa kwamba ni nani afunge nani asifunge. Cha msingi ni magoli hata kama yote atafunga Miquissone sawa tu.
Mchezaji mwenye magoli mawili kwenye mashindano ambayo mwenye magoli mengi zaidi ana magoli matatu, anawezaje kuwa si mfungaji mzuri ?
Nielimishe hapa.
Hayo mambo ya kuimbwa na mashabiki au kuwapo kwenye kikosi bora cha wiki sidhani kama yana mashiko sana. Kikosi cha wiki kinachukua wachezaji wachache mmno kati ya kundi kubwa. Hoja yetu isijikite kwenye muktadha huu maana nitakuuliza kwamba Onyango hajawahi kuwa kwenye kikosi bora cha wiki, ina maana ni mchezaji wa hovyo ?
Pia naomba tuzungumzie current situation, hayo ya Simba inahitaji mshambuliaji mwingine sidhani Kama yana msaada wowote kwenye hoja iliyopo mezani. Maana hata iweje, Simba haiwezi kumpanga Prince Dube, Simon Msuva wala Erasmus wa Mamelodi kwenye mechi ijayo ya robo fainali. Ni ama Bocco, Kagere au Mugalu. Tujadili hili
Lakini pia tusisahau kuwa goli moja Kati ya hayo mawili ni la penalty, na hata hilo jingine halikuwa na skills zozote za maana.Hebu angalia magoli ya miquisone na Chama, unaona kabisa ni ya skills za kiwango cha juu,mpaka yanaingia katika kinyang'anyiro cha magoli bora ya mashindano. Ukweli usemwe Mugalu hana kiwango kinachotosha yeye kucheza Simba,ni vile tu kocha hana namna.
Alafu sikuelewi kabisa unaposema kuwa, eti swala la wachezaji kuingia kwenye vikosi vya wiki na kushindanishwa katika ubora wa magoli ni maswala ya kishabiki. Hebu niambie hapa ni wapi huko ambako ubora wa mchezaji hauhusianishiwi na takwimu na maoni mbalimbali ya mashabiki? Maana hata BaronDo(sijui inaamdikwaje),ni matokeo ya takwimu na maoni pamoja na kura za mashabiki, au wewe unataka Mugalu apimwe kwa Kipi? [emoji23][emoji23]
Ukweli usemwe, Mugalu ni mshambuliaji wa kiwango cha chini sana. Unasema hakuna striker mzuri afrika, hatukatai ila sio kwa kiwango hicho cha Mugalu Sasa, Hebu jaribu kulinganisha uwezo wa Makambo(aliyewahi kuwa striker wa yanga) au Dube na huyo Mugalu wako. Yani kama yule Makambo au huyu Dube, wangekuwa kwenye hiki kikosi kinachotengeneza nafasi nyingi hivi wasingekuwa kama huyu.
Sent using Jamii Forums mobile app