BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,869
- 13,137
Kama ni hivyo basi ni jambo la heri.Watu huwa tunaajiriwa kwa ajili ya mambo matatu.
Kujikimu kimaisha, kuongeza ujuzi au maarifa ya kitu Fulani na kutafuta connection. Tatizo la watanzania tulio wengi tunaajiriwa kwa ajili ya kujikimu kimaisha hivyo hudhani kila aliyeajiriwa lengo lake ni hilo. Tukumbuke Salim kikeke ameishi kwenye hii tasnia kwa muda mrefu ila amehudumia media za kimataifa hivyo kama atahitaji kuwekeza kwenye media za nyumbani huwenda asiendane na soko letu. Hivyo kulazimika kufanya kazi katika media za nyumbani ili kujifunza ni namna gani media zetu zinavyoendeshwa. Au kuna mambo anahitaji kuyafanya hivyo kufanya kazi EFM ikawa ni moja ya njia anayotumia kufanikishia.
N.b Haya ni mawazo yangu tu