Suala la Salim Kikeke kuhamia EFM na akili za watanzania

Suala la Salim Kikeke kuhamia EFM na akili za watanzania

Asiambiwe ukweli?
Ukweli upi acheni ulofa nyie watu...Mimi nimeona kule UK mtu alikua naibu waziri mkuu akaacha akawa mwandishi ni maisha tu...kwani shida iko wapi??? nyie majuha mnataka mpangie watu kazi una unataka awe omba omba muanzeel ooh Kikeke anapiga vibomu balaa...
Salim uza hata mihogo fanya kazi roho yako inapenda maisha sio rahisi hata Ulaya tena Ulaya pagumu sana sio mchezo..
 
Ameacha BBC kwa ajili ya kuingia EFM?!
Inaweza kuwa alikua analipwa pesa ndogo BBC na labda ndio sababu ya kuacha. Sio watangazaji wote wa BBC wanalipwa mishahara mikubwa, kuna mambo walio mle ndani ndio wanayajua.

Kuna hata mwingine alishakua head wa hiyo idhaa ya kiswahili lakini sasa anafanya Azam media. Hii inathibitisha kuwa hawalipwi mishahara mikubwa kama tunavyodhani
 
Nimeona jinsi watu wanavyomshambulia Kikeke kwenye akaunti zake za kijamii kwa uamuzi wake wa kujiunga na kituo cha matangazo cha E-fm.

Nimebaki kuajabia tabia ya watanzania. Maisha ni yake, uamuzi ni wake cha ajabu anatukanwa na kudhalilishwa na wachangiaji juu ya uamuzi wake huo.

Tanzania ni taifa la watu wa hovyo sijapata kuona.
Naunga mkono hoja.
Kuna wakati nilijitolea kusaidia jambo fulani East Africa Radio, angalia nilichoambiwa Pascal Mayalla kutoka kuwa Mwandishi Nguli hadi Mtangazaji wa kawaida East Africa Radio inamaanisha nini katika Tasnia?
P
 
Nimeona jinsi watu wanavyomshambulia Kikeke kwenye akaunti zake za kijamii kwa uamuzi wake wa kujiunga na kituo cha matangazo cha E-fm.

Nimebaki kuajabia tabia ya watanzania. Maisha ni yake, uamuzi ni wake cha ajabu anatukanwa na kudhalilishwa na wachangiaji juu ya uamuzi wake huo.

Tanzania ni taifa la watu wa hovyo sijapata kuona.
Most ya wanaomshambulia ni watu wasio na upeo
 
Usihukumu
Hauwezi kujua kilichomfanya aachane na BBC...Sio kila mtu anajielezea yanayomkuta
Ameachana au ameachwa?,
Hakuna mtu aache wali nyama akale dona na maharage tusilileteane utani
 
Sababu za kuacha bbc mkataba alikuwa hawezi Tena kurenew au walimwambia aache Kuna ukuu wawilaya
Ni hivi BBC Swahili wote wamehamia Kenya .Wanarusha matangazo yao kutoka Nairobi.Wafanyakazi walipewa uhuru,wale wanaokwenda Kenya sawa,wasiotaka kuhamia Kenya kazi yao iliishia hapo.
 
Watu huwa tunaajiriwa kwa ajili ya mambo matatu.
Kujikimu kimaisha, kuongeza ujuzi au maarifa ya kitu Fulani na kutafuta connection. Tatizo la watanzania tulio wengi tunaajiriwa kwa ajili ya kujikimu kimaisha hivyo hudhani kila aliyeajiriwa lengo lake ni hilo. Tukumbuke Salim kikeke ameishi kwenye hii tasnia kwa muda mrefu ila amehudumia media za kimataifa hivyo kama atahitaji kuwekeza kwenye media za nyumbani huwenda asiendane na soko letu. Hivyo kulazimika kufanya kazi katika media za nyumbani ili kujifunza ni namna gani media zetu zinavyoendeshwa. Au kuna mambo anahitaji kuyafanya hivyo kufanya kazi EFM ikawa ni moja ya njia anayotumia kufanikishia.
N.b Haya ni mawazo yangu tu
 
Back
Top Bottom