Suala la Salim Kikeke kuhamia EFM na akili za watanzania

Kama ni hivyo basi ni jambo la heri.
 
Hapana watanzania siyo wa hovyo ila wameshangaa, Walitegemea kusikia amekuwa msemaji wa Serikali au msema wa Young Africa [emoji23][emoji23][emoji23], Ni sawa na Victor osimhen aondoke timu yake ya Napoli aje kuchezea Sigida big star.
 
Tz ina watu wenye mitazamo ya hovyo sana.
Hapana mkuu Tanzania tunampenda na tunapenda tuendelee kumuona kimataifa mfano alitakiwa aende CNN, Al-Jazeera, yani aendelee kucheza kwe ligi yake, Ndiyo maana Samata alivyoondoka Astoni villa watanzania tulikasirika tulitamani aendelee kuwepo Uingereza ili tuwe tunamuona kila wiki kwenye TV ndiyo maana alivyoondoka watanzania tukaanza kuihama timu kwa asila.
 
Umaarufu una gharama zake, na gharama zenyewe ni pamoja na hii kupangiwa uishi maisha gani na watu ambao hata huwajui....
Ni kweli umaarufu ni shida, Ray c alikuwa ana hojiwa akasema kuna kipindi alifuria mpaka akawa ana panda usafiri wa umma na kabla ya kupanda alikua ana jificha uso ili abiria wasimuone.
 
Sidhani kama ni sahihi
 
Amekaa sana BBC ni wakati wa kuwa na kitu chake mwenyewe sasa tusubiri ni suala la muda tu.Pia amekaa sana kwenye utangazaji habari Kuna haja ya kubadili upepo kidogo.
 
@Dr Rutegarwera
Naam namie nimeliona hili jambo nikaona nitie neno.

Bila shaka linaashiiria tabia za watanzania. Tupe picha tu mengine tulijijazia .

Lakini muhimu zaidi cha kujifunza ni kipi?



Jitihada za elimu hazijasaidia watanzania wengi ambao bado wapo kwenye giza tororo la ufahamu. Kwamaana hiyo uwezo wetu wa kuchakata mambo na msimamo wa maisha ni mepesi ajabu.

Mapungufu ya Radio zetu Tanzania ni makubwa kiasi kwamba ndugu yetu salim kutaka kujiunga baada ya kujijejngea brand kubwa kumewachanganya na kuwashangaza wadau wa habari

Bila shaka wanaosimamia maudhui TCRA wanafahamu hilo na ama wanapuuza au wnaaacha maudhui ya ohvyo yapite kwa kuwa hali hiyo inasaidia kulinda maslahi ya mabwana wakubwa-huwezi kuhoji utawala bora ikiwa kila kukicha redio na TV inajadili mahusiano na wanahabari ndio wanenguaji wakuu na machawa

Ripoti zetu nyingi bila shaka hazihaririwi ili kuhakiki. Michezo ndio kwenyewe ni simba na Yanga tuu

Ndugu yetu Salim ni brand kubwa kuliko karibia redio na TV zote ndani ya nchi -ni muda sasa wa vyombo vyetu hivi kujitafakari ama wabaki kama walivyo au wabadilike
 
Gharama za Maisha Ulaya ziko juu we fikiria Mpk kumiliki tv unalipia Kodi(nilimsikia Zuhura Yunus akisema)wakati huku kwetu ukiwa mjana utalipa inderect tax zile za lazima zingine zitakupita!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…