Suala la timu ya USM Alger kuja na Maji na vyakula linafikirisha sana

Suala la timu ya USM Alger kuja na Maji na vyakula linafikirisha sana

Juzi tumeona kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha timu ya USM Alger ikiwasili JK Nyerere International Airport ikiwa na shehena ya Maji ya kunywa na pia inasemekana walibeba na vyakula vyao.

Huenda wakawa na nia njema ya kuhakikisha usalama wao na kuepuka hujuma za kimichezo lakini pia kwa upande mwingine wanaweza kutumia fursa hiyo kuingiza vimiminika kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa wachezaji wao ambapo unaweza kukuta mchezaji mwanzo mwisho yupo na energy ile ile au mara dufu.

Inavyoonekana vinywaji hivyo wameingia navyo siku hiyohiyo ambapo ukifuatilia sidhani kama mamlaka husika kama TFDA, TBS nk zilikuwa na muda wa kufanya ukaguzi wa kina.

Nadhani mambo kama haya vyombo vyetu vya Usalama including SSIT kwenda mbali zaidi.
Ukiona hivyo ujue hao waarabu wameishangia mchecheto. Na leo wanakufa kwa mkapa na kwao watakufa tena.

Na nyie Makolo leo mje kwa Mkapa ili muone jinsi tunavyompelekea moto mwarabu
 
Naona hao USM Alger wamecomplicate tu hiyo issue, dunia imebadilika, hakuna sababu ya kuja na vyakula wala maji, vyakula na maji vilivyopo hapa Tz ni sawa tu na huko kwao na huenda vya hapa kwetu vikawa na ubora kwa kuwa vitakuwa more fresh.

Wajikite kucheza mpira na sio hivyo vitu vidogo.
 
Pia mleta mada umecomplicate mambo, huhitaji kuja na vitu vya kuongeza nguvu kutoka huko nje wakati vinywaji vya namna hiyo vimejaa mtaani.
 
Mimi nilitegemea waje na mitungi yao ya gesi (ili kukwepa kuvuta hii hewa yetu na kule vyumbani) kuliko kuja na maji, vinywaji na vyakula.
 
Pia mleta mada umecomplicate mambo, huhitaji kuja na vitu vya kuongeza nguvu kutoka huko nje wakati vinywaji vya namna hiyo vimejaa mtaani.
Sikuwa na maana ya vinywaji halali bali nilimaanisha vile visivyoruhusia kabisa ambavyo hata madukani havipo
 
Utakuwa mgeni kwenye mpira, Timu kibao zinafanya hivyo ikiwamo Brazil
Tatizo waswahili hadi mfafanuliwe kila kitu ndipo mtaelewa hoja imebeba nini, wazito sana kuelewa Concept. Ila wapo ambao wamenielewa humu
 
Haya mambo ya watu kuja na vyakula vyao hayajaanza leo kwani mwaka 1974 wakati Mehallah El Khubra ya Misri walipokuja kucheza nusu fainali klabu bingwa Afrika dhidi ya Simba walikuja na vyakula vyao hadi na maji yao.

Mwaka uliofuata 1975 Enugu Rangers ya Nigeria walipokuja kucheza na Yanga nao walikuja na maji yao ya kunywa.

Hata miaka mingine kama 1976 klabu ya Ibadan Shooting Stars ya Nigeria nao walikuja na maji yao hata Racca Rovers pia ya Nigeria mwaka 1977 nao walikuja na maji yao ya kunywa. Kwa hiyo haya ni mambo ya kawaida na hayajaanza leo na pia haitakuwa mwisho.
 
Cha msingi yanga wajipange maana nasubiri wakifungwa kesho mapemaa nipo redioni kuskiliza wachambuzi wa mchongo nibaki ancheka. Ila wawafunge waarabu ili wajute kuna na maji yao na vyakula
 
𝙺𝚊𝚖𝚊 𝙺𝚞𝚔𝚊𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚊𝚔𝚊𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚝𝚞, 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚗𝚊𝚖𝚗𝚊
 
Back
Top Bottom