Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Labda hawaoni haki ikitendeka. Why Aida yupo Bungeni na Chama kimeshindwa kuchukua hatua stahiki? Double-standards!
Aida Ana kosa gani Hadi achukuliwe hatua? SEMA kosa la Aida acha Mambo ya wivu wa Mbowe.
 
Hiyo ni hofu ya mwenye njaa, kwanini ilwe nongwa kwa akina Mama wa Chadema kwenda mjengoni?, ingekuwa viti maalum ni wanaume simngeshaapishwa zaman. Acheni uzwazwa Wanaume tulieni dawa iwaingie

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Mwaka 2015 mliibiwa kura au hamkuibiwa. TOA jibu siyo ulete unyumbu hapa.
 
Kama kuna jambo ambalo silipendi ni tabia ya wafuasi wa Chadema kuwaita wale ambao wanatofautiana ndani ya chama wasiliti. Hivi kuna wangapi katika hao wanaowarushia madongo wakina Halima, Esther na wengine amechangia zaidi yao kihali na mali mapambano dhidi ya chama tawala. Hawa wamepigwa, wamenyanyaswa kijinsia, wamefukuzwa bungeni, biashara zao zimebanwa, wamekaa mahabusu mpaka kumekuwa kama kwao, wamefungwa, wamefunguliwa kesi lukuki n.k.

Wakati wote huo hawakutetereka katika msimamo wao. Leo mtu kasema kuwa inawezekana katika hili suala la wabunge wa viti maalum basi tumeona imetupa haki ya kuwaita wasaliti, wachumia tumbo na matusi mengine kama hayo. Sisi ambao hatuna ubavu wa kusimama hadharani, bila kuficha majina na sura zetu na kukemea serikali iliyopo kwenye madaraka! Sisi ambao ni wepesi wa kuwatukana lakini tunashindwa kuandamana nje ya mahabusu, jalat, na mahakama ambako vijana wetu wanasota kwa sababu tu walidiriki kuwa wapinzani. Sisi ambao tulishindwa kukataa katakata watu wetu kuondolewa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi, na kwa wale waliobaki kusimama na kupambana kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika vituo vya kupiga na kuhesabu kura. Sisi ambao tumeshindwa kusimama nao walipotuomba tuandamane kuonyesha kutoridhishwa kwetu na jinsi uchaguzi mzima ulivyoendeshwa. Wako vijana huko kusini ambao kweli walipambana lakini walishindwa kwa sababu walikuwa peke yao.

Ukweli ni kuwa si Halima, Lissu au Mbowe anayeweza kushinikiza serikali ifanye mabadiliko tunayosema tunayotaka. Hata wakina Armstrong na McAllister hawawezi kutuletea hayo mabadiliko. Wenye uwezo huo ni wananchi peke yao ambao kwa njia za amani, wakiungana na viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kuuonyesha utawala kuwa wanataka mabadiliko. Kukaa kimya kwao ni dalili tosha kuwa wanakubali kwa kiasi kikubwa na wanaunga mkono juhudi za serikali iliyopo madarakani.

Mimi siamini hata kama wakiingia bungeni wataunga juhudi kama wakina Lijualikali, Mollel, Silinde, Waitara na wengine kama hawa. Hawa wakina mama wametuonyesha kuwa ni wafia mabadiliko na wanastahili heshima yetu hata kama hatukubaliani na baadhi ya maamuzi yao.

Amandla...
 
Mpango wowote wa kupeleka wabunge viti maalum bungeni,utaiathiri pakubwa chama kikuu CHADEMA kwa kuwa watakua wamekubali kuwa Uchaguzi ulikua huru, Chama kikuu kineyakataa matokeo ya uchaguzi wote kitendo cha kukubali kupeleka wabunge viti maalum Bungeni ni kukubaliana na dhulma zilizofanyika katika uchaguzi.
Kwani lini chadema walikubaliana na matokeo ya uchaguzi?
2015 waliibiwa kura au hawakuibiwa? Najua walisema wameibiwa na hawaukubali uchaguzi na wakaenda bungeni.
 
Siamini kama hawa hawa CCM walipora kura nchi nzima leo hii wanawataka wanawake CDM wakachukue zile nafasi 19 za Ubunge... si bure kuna jambo hapo.
 
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
Ukisikia nyumbu ndo hao, kesho chadema wataenda bungeni chadema haohao watakuja hapa kushangilia wameshahau Jana walisema nini.
Hizo ndo akili zao nyumbu hovyo kabisa.
 
Mwaka gani CCM haikupora uchaguzi?
Wanawapora kila mwaka na mnaenda bungeni, kwanini mwaka huu mnaweweseka wakati kila mwaka CCM wanawapora uchaguzi na mlishazoea kuporwa?
Tatizo ni saccos na siyo chama.
 
A very logical question.
Nyumbu walishasahau kwamba miaka yote wanakataa matokeo, yangekuwa na kumbukumbu yangepata akili yakatafuta sababu za kuchezea kichapo Cha shoga mwizi lkila mwaka na hayabadiliki.
 
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
Mimi toka kina Sillinde wafanye mambo ya aibu simuamini mtu kabisa. najiamini mimi tu
 
Kubwa jinga wewe na matusi yako nakuweka ignore list,naona umevurugwa mfyuuu, go to hell [emoji48] and byee
Member mzee humu JF hujiheshimu
amevurugwa anaekunyunyizia
shwain wewe
 
Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini kula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya Bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya Viti Maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa wizi ambao tulishuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa dhidi ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.

Wizi wa kura kama huu hapa chini, utakubalije uchaguzi wa aina hii?

View attachment 1633707
Aksante kutujuza. Hii tayari imebuma. CCM wajaribu mbinu nyingine. Ninawaomba viongozi wa CDM wawafukuze uwanachama wasaliti wote. Heri kubaki na wanachama wachache walio "loyal" kuliko kuwa na kundi la wasaliti.
 
Kwanza chama kifanye uchunguzi kujua Ni akina Nani hao wanaotaka kusaliti. Baada ya hapo ndpo kifanye uteuzi wake wa kupeleka majina bungeni. Kiwateme hao vimbelembele.
 
Back
Top Bottom