Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Labda hawaoni haki ikitendeka. Why Aida yupo Bungeni na Chama kimeshindwa kuchukua hatua stahiki? Double-standards!
Aida Ana kosa gani Hadi achukuliwe hatua? SEMA kosa la Aida acha Mambo ya wivu wa Mbowe.
 
Hiyo ni hofu ya mwenye njaa, kwanini ilwe nongwa kwa akina Mama wa Chadema kwenda mjengoni?, ingekuwa viti maalum ni wanaume simngeshaapishwa zaman. Acheni uzwazwa Wanaume tulieni dawa iwaingie

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Wakienda bungeni ndio watapoteza heshima yote waliyonayo kwenye jamii, watajitia doa ambalo halitafutika.

Watanzania wa sasa wanaelewa kila kitu, ole wao hao wanawake.
Mwaka 2015 mliibiwa kura au hamkuibiwa. TOA jibu siyo ulete unyumbu hapa.
 
Kama kuna jambo ambalo silipendi ni tabia ya wafuasi wa Chadema kuwaita wale ambao wanatofautiana ndani ya chama wasiliti. Hivi kuna wangapi katika hao wanaowarushia madongo wakina Halima, Esther na wengine amechangia zaidi yao kihali na mali mapambano dhidi ya chama tawala. Hawa wamepigwa, wamenyanyaswa kijinsia, wamefukuzwa bungeni, biashara zao zimebanwa, wamekaa mahabusu mpaka kumekuwa kama kwao, wamefungwa, wamefunguliwa kesi lukuki n.k.

Wakati wote huo hawakutetereka katika msimamo wao. Leo mtu kasema kuwa inawezekana katika hili suala la wabunge wa viti maalum basi tumeona imetupa haki ya kuwaita wasaliti, wachumia tumbo na matusi mengine kama hayo. Sisi ambao hatuna ubavu wa kusimama hadharani, bila kuficha majina na sura zetu na kukemea serikali iliyopo kwenye madaraka! Sisi ambao ni wepesi wa kuwatukana lakini tunashindwa kuandamana nje ya mahabusu, jalat, na mahakama ambako vijana wetu wanasota kwa sababu tu walidiriki kuwa wapinzani. Sisi ambao tulishindwa kukataa katakata watu wetu kuondolewa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi, na kwa wale waliobaki kusimama na kupambana kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika vituo vya kupiga na kuhesabu kura. Sisi ambao tumeshindwa kusimama nao walipotuomba tuandamane kuonyesha kutoridhishwa kwetu na jinsi uchaguzi mzima ulivyoendeshwa. Wako vijana huko kusini ambao kweli walipambana lakini walishindwa kwa sababu walikuwa peke yao.

Ukweli ni kuwa si Halima, Lissu au Mbowe anayeweza kushinikiza serikali ifanye mabadiliko tunayosema tunayotaka. Hata wakina Armstrong na McAllister hawawezi kutuletea hayo mabadiliko. Wenye uwezo huo ni wananchi peke yao ambao kwa njia za amani, wakiungana na viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kuuonyesha utawala kuwa wanataka mabadiliko. Kukaa kimya kwao ni dalili tosha kuwa wanakubali kwa kiasi kikubwa na wanaunga mkono juhudi za serikali iliyopo madarakani.

Mimi siamini hata kama wakiingia bungeni wataunga juhudi kama wakina Lijualikali, Mollel, Silinde, Waitara na wengine kama hawa. Hawa wakina mama wametuonyesha kuwa ni wafia mabadiliko na wanastahili heshima yetu hata kama hatukubaliani na baadhi ya maamuzi yao.

Amandla...
 
Kwani lini chadema walikubaliana na matokeo ya uchaguzi?
2015 waliibiwa kura au hawakuibiwa? Najua walisema wameibiwa na hawaukubali uchaguzi na wakaenda bungeni.
 
Siamini kama hawa hawa CCM walipora kura nchi nzima leo hii wanawataka wanawake CDM wakachukue zile nafasi 19 za Ubunge... si bure kuna jambo hapo.
 
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
Ukisikia nyumbu ndo hao, kesho chadema wataenda bungeni chadema haohao watakuja hapa kushangilia wameshahau Jana walisema nini.
Hizo ndo akili zao nyumbu hovyo kabisa.
 
Mwaka gani CCM haikupora uchaguzi?
Wanawapora kila mwaka na mnaenda bungeni, kwanini mwaka huu mnaweweseka wakati kila mwaka CCM wanawapora uchaguzi na mlishazoea kuporwa?
Tatizo ni saccos na siyo chama.
 
A very logical question.
Nyumbu walishasahau kwamba miaka yote wanakataa matokeo, yangekuwa na kumbukumbu yangepata akili yakatafuta sababu za kuchezea kichapo Cha shoga mwizi lkila mwaka na hayabadiliki.
 
Ulitaka akubali kisha uanze kumtukana?
Kataa uamini siku ikifika hamtakuja na kuuliza tena humu mtakuja na hija nani achaguliwe ili aende bungeni, au nani kaachwa wakati alistahili.
Mimi toka kina Sillinde wafanye mambo ya aibu simuamini mtu kabisa. najiamini mimi tu
 
Kubwa jinga wewe na matusi yako nakuweka ignore list,naona umevurugwa mfyuuu, go to hell [emoji48] and byee
Member mzee humu JF hujiheshimu
amevurugwa anaekunyunyizia
shwain wewe
 
Aksante kutujuza. Hii tayari imebuma. CCM wajaribu mbinu nyingine. Ninawaomba viongozi wa CDM wawafukuze uwanachama wasaliti wote. Heri kubaki na wanachama wachache walio "loyal" kuliko kuwa na kundi la wasaliti.
 
Kwanza chama kifanye uchunguzi kujua Ni akina Nani hao wanaotaka kusaliti. Baada ya hapo ndpo kifanye uteuzi wake wa kupeleka majina bungeni. Kiwateme hao vimbelembele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…