Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Kama uongozi wa chama haujaridhia, wakienda Dodoma wafukuzwe uanachama.
Ndio dawa hiyo tunaomba muwaeleze na viongozi wao wakuu wa chama mwanachadema akienda kinyume na matakwa ya chama fukuza uanachama Mara moja
 
viongozi wa upinzani nadhani ni wanafiki, haiwezekani waseme hawatambui matokeo alafu tayari kuna wabunge wao wamekula kiapo na hawajawafukuza uanachama, hawa mabwana ni wabinafsi na wachumia tumbo bt time will tell.
 
Kama uongozi wa chama haujaridhia, wakienda Dodoma wafukuzwe uanachama.
du dada sky unaroho ngumu bado uko nao tu hao wahuni na saccos yao? haya mwenzenu kawakimbia alitaka muingie barabarani aone jinsi gani kmlivyowajinga mpigweeeee yeye alisema atakuwepo kwenye maandamano mbona hakutokea?zakuambiwa changanya na zako mngekoma
 
CDM hawaheshimu wanawake Wana kimfumo dume kweli hzo nafasi ziko kisheria kabisa, kumbe wanatetea matumbo yao wenyewe
Ishu hapa ni kwamba hata hao wanawake waliozushiwa wamesema hawawezi kwenda bungeni kwa ukatili waliofanyiwa kama wanawake ikiwemo majaraha mbalimbali kwenye miili yao,na wao wanaamini wangepewa fursa sawa kama wengine bila mabavu na dhuluma wangeshinda kihalali.
 
Ka

1-Kama unadhani spirit ya upinzani kwa wananchi ni wabunge tu utakuwa upo nyuma ya historia,upinzani ni imani na hakuna serikali inaweza kuua spirit ya upinzani.
2.Mwenyekiti alisema mpaka 2020 upinzani utakuwa umeshafutika,ni upinzani upi unaouzungumzia wewe?
3.Kama ni sheria;Je,mbona sheria zinafatwa tu kwenye viti maalumu na siyo kwenye mchakato mzima wa uchaguzi?
4.Kama mmetimia bungeni,mnahangaika na viti maalumu vya kazi gani?
Sasa hapo umesema nini? Kuna maneno unayotumia kwenye sentensi zako yanayoonyesha wewe ama mtu mwenye hasira sana au mtu asiyekuwa na busara katika mawasiliano bali mtoa lawama na confrotational. Route hiyo ni ngumua sana kutumia katika mawasaliano
 
Jibu hoja kwa hoja na siyo hoja kwa hisia-Act like a real man.Hakuna mahali nilipoandika nimekuzungumzia wewe personal bali nimezungumzia hoja zako;That's all.
 
Mpaka bunge la April 2021 Ndungai anaweza kuwa The Hague.
Ndugai kwa mujibu wa uspika wake, kama angethibitika kufanya uhalifu dhidi ya katiba au mwingine, angeshughulikiwa kisheria humu nchini.
Hata hivyo, wameona mbali wakamuwekea kinga.
Ukombozi wa uhakika wa wanadamu ni ule wa kutokea ndani, nje ni kuongezea nguvu tu.
 
Jibu hoja kwa hoja na siyo hoja kwa hisia-Act like a real man.Hakuna mahali nilipoandika nimekuzungumzia wewe personal bali nimezungumzia hoja zako;That's all.
Sikuona hoja ya kujibu kutoka kwako; nimeona snippets za hisia zako tu. Hoja yangu ilikuwa ni kwamba ni vizuri kwa CHADEAM kutoku-forfeit nafasi hizo za viti maalumu, lakini hukutoa hoja ya kwa nini ni vizuri kwa chadema kuendelea kuforfeit nafasi hizo. Halafu sasa eti unataka nikujibu kwa hoja ambayo hujaweka! Upuuzi mkubwa sana!!
 
Hivi kinachowafanya wanaume wawazuie hawa wanawake kwenda bungeni ni nini? Kwanza kwani ni wake zao???
Wamenisikitisha Sana Hawa wanaume kwa ubinafsi wao, mbona miaka yote hawatambui ushindi wa ccm, Ila walienda bungeni, Mimi namushauri Halima apeleke majina, maana ipo siku waweza shangaa tundu lisu kateuliwa na Raisi na kakubali, maana wanasiasa hawaamini Kama walivotuaminisha lowasa ni fisadi then wakaja kumpitisha Kama mgombea.
 
Ishu hapa ni kwamba hata hao wanawake waliozushiwa wamesema hawawezi kwenda bungeni kwa ukatili waliofanyiwa kama wanawake ikiwemo majaraha mbalimbali kwenye miili yao,na wao wanaamini wangepewa fursa sawa kama wengine bila mabavu na dhuluma wangeshinda kihalali.
Usiamini wanasiasa wewe dr slaa alifanywa mlemavu wa mkono lakini leo Yuko ccm
 
Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini linakula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAVICHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya viti maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa na ambao tulioshuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na kwenda bungeni ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa ua machaguo ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.
Ujinga tu na ubinafsi. Ingekua kwa mfano mbowe na labda lema sugu na wale walimbwende wa chadema mdee bulaya na matiko peke yao tu wameshinda ubunge chadema wasingesusia ubunge wangeingia na kundi lao la viti maalum. Kwa kua chadema ni kampuni ya mbowe na wengine wachache wenye hisa wameona kwa nini watu sio wamiliki wa chama wafaidike kwa mapato wakati wenyel kampuni hawapati kitu. Wangetamani hao kina mama maalum wawape masharti ya kusalimisha mapato yao bungeni kwao ila wanaogopa jamii itawazomea.
Badala ya kukubali wameshindwa vibaya uchaguzi kwa kua na sera mbovu za ubinafsi kwa kufuata mkakati wa uongo na uzushi na pia kumuweka mgombea urais kibaraka wa mabeberu wanasingizia kuibiwa kura bila kua na ushahidi wowote.
Badala ya sekretariat ya chama kuketi na kuwateua akina mama wenye kustahili kujaza nafadi za viti maalum kwa ubinafsi wameanguka kwenye mtego wa mabeberu wanaomlipa mwanasheria shoga amsterdam eti wasusie kwa kuibiwa kura.
Watanzania wameelimika sasa wanajitambua. Hivi kwa sera za ubinafsi na majimbo na mgombea anayetetea kwenye campaign zake ushoga wanafikiri watanzania ni wajinga kiasi gani wawachague?
Kabla ya uchaguzi wengi walitabiri kushidwa vibaya na uwezekano kufa chadema. Sasa utabiri umetimu nini cha ajabu?
 
Tatizo la siasa ni washabiki, washabiki wa siasa ndio watu wasiojielewa. Mara kadhaa mmekumbushwa kuwa wanasiasa wote wanajuana na hawapo serious na kitu kinaitwa kupigania sijui watu

Kuna watu walikufa 2010 wakimpigania Dr.Slaa, leo wakiamka ukawaambia Dr.Slaa yupo ccm wanaweza kufa tena.

Kuna watu walikufa 2015 wakimpigania Lowassa, leo wakiamka?

Kama katibu wa chama aliweza kuondoka, iweje ushangae leo hii kwa mdee na bulaya?? Mtajifunza lini nyie watu msiosikia? Au ndio mtaandika post kila muda kuwatukana?
🤣🤣
 
Kuna habari zina-trend mitandaoni kuwa kuna kuna kundi la wanawake wa CHADEMA lipo kwenye harakati za chini kwa chini linakula njama za kwenda Dodoma kula kiapo cha kuingia bungeni kwa viti maalum.

Kundi hilo linajumuisha wanawake wenye majina makubwa makubwa ndani ya chama hicho, waliojijengea heshima huko zamani kutokana na misimamo yao nje na ndani ya bunge.

Hata hivyo inasemwa kuna mkakati unaoratibiwa na katibu mkuu wa zamani "aliyeunga mkono juhudi" ambaye ndiye anayeongoza jitihada xa kuwashawishi na kuwaweka sawa ili wakubali kusaliti msimamo wa chama chao.

Mimi ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa BAVICHA Halima Mdee kuwa hili suala linakwenda kupasua taasisi ya akuna mama wa CHADEMA. Kwanza kitendo cha wanawake kadha wa kadha kujichagua wao wenyewe na bila ridhaa ya Chama kwenda bungeni ni kinyume cha sheria ya nchi juu ya utaratibu wa viti maalum.

Sheria inataka majina ya viti maalum yawasilishwe kwenye mamlaka husika na katibu mkuu wa chama na si mtu kujipeleka mwenyewe.

Pili kitendo cha mwanachama kujiteua mwenyewe na kwenda kula kiapo kinyume cha utaratibu wa chama ni kuvunja wazi katiba ya chama maana mwanachama anakuwa amejitwalia mamlaka ya vikao mbalimbali vya chama vyenye kuhusika na teuzi za viti maalum.

Iwapo akina mama wa CHADEMA watakwenda kuchukua nafasi hizi za viti maalum kinyume cha sheria itakuwa ni kuweka haramu nyingine ya kisheria juu ya haramu ya uchaguzi feki, na utakuwa ni uhuni mwingine wa Ndugai na serikali kama uhuni mwingine wowote tuliokwisha ushuhudia.

Kuna swali nataka Halima Mdee anijibu

1. Yeye kama Mwenyekiti wa BAWACHA na mwanachama mwandamizi wa CHADEMA amefanya nini kuisaidia CHADEMA ili utaratibu wote wa kuheshimu maamuzi ya Uongozi wa CHADEMA katika ishu hiyo ya viti maalum ufuatwe?

2. Yeye kama muathirika mkuu wa wizi wa kura wa waziwazi aliofanyiwa na ambao tulioshuhudia video zake, Je yuko tayari kwenda bungeni kinyume cha utaratibu wa Chama chake cha CHADEMA na kwenda bungeni ili kuhalalisha bunge ambalo limepatikana kwa dhulma kubwa ua machaguo ya wananchi?

Wito kwa Uongozi wa CHADEMA
Namshauri Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chadema, Iwapo Kuna kundi la wanachama wa CHADEMA watajitwalia mamlaka ya kwenda bungeni kuapa kuchukua viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama basi hao wamevunja katiba ya chama na watu hao washughulikiwe mara moja. Kwa sababu hata mkiwaacha watakuwa na Loyalty iliygawanyika, watajifanya kuwa upande wenu kujiegemeza kisiasa na kutafuta political standing mbele ya umma lakini watakuwa very Loyal kwa CCM na serikali yake kwa sababu ndo wanawapa kula.

Sasa ili kuondoa sintofahamu inayoweza kutokea huko mbele, Iwapo watajitokeza na kwenda kujiapisha bila ridhaa ya chama, basi Fukuza wote bila kujali jina la mtu.

Kama mkiwaacha, basi wapo wanawake mamilioni wa CHADEMA wanaofuatilia suala hili kwa nguvu zote na watakatishwa tamaa kwa chama kuwa selective kwenye kusimamia mambo ya msingi yenye manufaa kwa demokrasia ya Taifa.

Pili kwa kuwa CCM wamemessup kwa kuiba, kupora chaguzi na sasa wanatafuta legitimacy kwa kujaribu kuwanunua wapinzani kadhaa wa kuwaingiza bungeni, kitendo cha kuwatimua uanachama hawa kitawaondolea CCM ile legitimacy wanayoitaka ya uwepo wa wapinzani bungeni. Hapo mwanzo CCM waligeuza uwepo wa wapinzani bungeni kama rallying object ya kupeleka mashambulizi n. k, Sasa wamo mle peke yao, hawana excuse mbele ya wananchi ya kutodeliver. Sasa kukosekana kwa wapinzani wanajikuta wako peke yao, bunge limekuwa la chama kimoja, limekosa legitimacy, ndiyo maana wanahaha wapinzani wawemo!

Mwisho kabisa niwaombe akina mama wa CHADEMA wanaosumbuliwasumbuliwa na CCM ili wakahalalishe uharamu wa uchaguzi ule

1. Mkienda mle, mtahalalisha ile haramu, na itakuwa modus operandi ya CCM, yaani utskuwa ndo mchezo wao, kupora maamuzi ya wananchi kisha wawalambisha pipi wapinzani wachache mambo yao ya udhalimu yanaendelea. Je mko tayari kutusaidia sisi wananchi kwa kukataa michezo hii ya kihuni au mnataka kutuacha sisi wananchi kwenye mataa?

2. Je mko tayari kwa sababu ya vipande vya fedha kuwatupa na kuwasaliti viongozi wenu wa Chama na chama ambao kiukweli kabisa wanasimamia maslahi mapana ya wananchi na Chama kwa kukataa kulegitimize uharamu. Je nyie mnataka kukisaliti chama chenu kilichowatoa mbali?

3. Enyi wanamama wa CHADEMA hata mkiingia humo bungeni, hao CCM watawadharau, watawaona sellout.
Kikubwa zaidi sisi wananchi tutawadharau sana, maana mtakuwa hampo kwa ajili ya wananchi.
Si mngesubiri kidogo tu mpaka wafanye hiki wanachotuhumiwa kufanya?
Na kwa vile Mkurugenzi wa NEC amesema kuwa hawezi kutambua uteuzi wowote usio ambatana na barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama husika, tutajua kama wamefanya hivyo kwa ridhaa ya chama chao au utaratibu umepindishwa ili kuwanufaisha.

Wasiwasi wangu ni kuwa kutokana na umahiri walioonyesha wanawake wa Chadema hii ni mojawapo wa njama za kuleta mpasuko mkubwa ndani ya chama chao. Ni kweli uwezekano wa kuwa hili litatokea lipo hasa ukizingatia kuwa mmoja wa wanaotajwa kuwa ni wabunge wanaotarajiwa amefutiwa kesi fasta, kitu ambacho kinaweza kuwa ni mpango wa kumwezesha kuwahi kwenye uapisho. Hii ni moja ya changamoto ambazo wale wote wanaojihesabu kama wapinzani inabidi wazipitie.

Sidhani kama upinzani utakufa kama hawa wakina mama na pengine uongozi wa chama chao utachukua hatua hiyo. Tuvute subira kwanza maana hata ACT-WAZALENDO nao wanadaiwa kufikiria kujiunga na serikali ambayo sio tu wanaituhumu kuwa wamewaibia ushindi bali wamewapiga, kuwatesa na hata kuwaua baadhi ya viongozi na wafuasi wao.

Amandla...
 
BAWACHA jiongezeni, nendeni bungeni kwa zile nafasi 19

Mtakuja juta siku nyie mnakataa hizi nafasi halafu viongozi wenu wanakuja kuteuliwa na rais kwa kazi ndogo ndogo wanakubali

Za kuambiwa changanya na zako - Jakaya Kikwete

Msije kusema hatukuwashauri hili [emoji23][emoji23][emoji23]
huo sio ushauri
 
Devotha Minja
* Nusrat Hanje
*Agnesta Lambert
*Cecilia Pareso
*Asia Msangi
* Grace Tendega
*Nagenywa Kaboyoka

Inasemekana hawa wameshapangwa kuapishwa fasta kesho. Wabunge wa viti maalum wa chadema wanakwenda kujisajili kwa katibu wa bunge
👉Katibu wa bunge atachukua hiyo list ataipeleka kwa Dr Mahela kesho hiyo hiyo
👉The Mahera ataisha vyombo vya habari kupublish kwenye gazeti la serikali
 
Back
Top Bottom