Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Tetesi: Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na Wanawake wa CHADEMA

Nawapongeza CDM kwa maamuzi hayo, hiyo ni kazi imepatikana haikuwa vizuri kuisusia, kuhusu uchaguzi wanaweza kuendelea na kesi zao huku jina lao likiwa kwenye chati, Cha msingi hizo pesa zitakazopatikana wajitahidi wafungue kampuni moja tu waajili vijana wengi wao msingi wao na maendeleo waache CCM watuletee Ila wao wasimamie swala moja tu la ajira kwa kufungua kampuni hata mbili.
 
Hizo propaganda za wapishi wa propaganda!

Ukweli hadi tunamaliza kupiga kura mambo yalikuwa shwari.

Kwa ujumla waangalizi wa uchaguzi wamethibitisha hilo.
Wagombea na viongozi wa upinzani walithibitisha hilo, rejea kukiri kwa Lissu na Zitto kwamba uchaguzi kiujumla umeendeshwa vizuri. Ila baada ya matokeo na kuona wameshindwa ndiyo wakaja na hadithi za alfu lela ulela!

Jiulize kwa nini wameshindwa kukusanya ushahidi unaoeleweka na wenye uzito na kuwasilisha mahakamani hata kwa chaguzi za wabunge na madiwani wakati chaguzi zilizopita walifanya hivyo? Au hata kuwasilisha kwa umma.

Achana na michezo ya kuigiza ya kuchapisha kura feki kisha ku stage kumkamata mtu na kura feki, alafu unazichoma mwenyewe hizo kura na kurusha vi clip!
Zamani walikuwa wakishindwa au kutoridhika wale mawakala wao walikuwa hawasign


This time kila wakala ka sign kuridhishwa na matokeo


Mara wameibiwa????
 
Hahaha hakuna wa kwenda bungeni, sharti lazima wathibitishwe kwa barua kutoka kwa katibu mkuu Chadema, kwenda NEC kisha wao waiwasilishe kwa spika.

Nje ya utaratibu huo hakuna wa kwenda kuapishwa.

Halafu kama hivi wameapishwa watu kama wewe bado mtamwona JPM mbaya, kumbe kuna mambo ya nyie kurekebisha kwanza
 
Hahaha hakuna wa kwenda bungeni, sharti lazima wathibitishwe kwa barua kutoka kwa katibu mkuu Chadema, kwenda NEC kisha wao waiwasilishe kwa spika.

Nje ya utaratibu huo hakuna wa kwenda kuapishwa.
Wameshaenda sasa. Hivyo tu!
 
Hii yaweza kuwa "watershed moment" kwa CDM kama ilivyokuwa wakati wa kumpokea Lowassa! Kwa wengi itabadili msimamo wa namna tunavyoichukulia CDM na upinzani kwa ujumla. Nasubiri maelezo ya Katibu mkuu juu ya hili.
 
Halafu kama hivi wameapishwa watu kama wewe bado mtamwona JPM mbaya, kumbe kuna mambo ya nyie kurekebisha kwanza
Watakuwa siyo wa chadema bali wa ccm.
Chadema haitambui matokeo ya uchaguzi wa October 28, 2020.

Huwezi kuwalazimisha kukubali matokeo.

Mkiona vipi mkifute chama, lakini kina haki kukataa.
 
😂😂😂😂😂😂😂
Tukubali au tukatae watanzania tunapendana. Nendeni bungeni tujenge nchi
Kwa upendo upi Mama? Wa lijambazi na aliekabwa na kuporwa vilivyo vyake? Yanatoka moyoni mwako kweli?
 
Tatizo kubwa hapo ni kwamba, kama wataenda bungeni kwa kupindishiwa sheria kwa amri ya Magufuli kama ilivyozoeleka wataishia tu kumtumikia Magufuli kama walivyo wabunge wengine wa ccm.

Na ndipo itakapodhihirika wazi kuwa wameenda kula pesa za ubunge na sio kupigania wapiga kura wao na muda wao ukiisha ndio hivyo tena watakuwa wamejiunga na ccm.
 
Pili, kaa ukijua CHADEMA lazima wapeleke Viti Maalum Bungeni hawawezi kuachia hiyo fursa ipite hivi hivi labda kama hicho chama hakiongozwi na wachaga.
Hoja nyingine bado ni za kitoto sana. Watia huruma kwa kufilisika cha kuchangia
 
Back
Top Bottom