Suala la VPN walengwa ni wapinzani, watumia VPN kuepuka gharama za mabando na kucheki mambo binafsi ondoeni hofu

Suala la VPN walengwa ni wapinzani, watumia VPN kuepuka gharama za mabando na kucheki mambo binafsi ondoeni hofu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Sheria hii lengo lake ni kutoa kibali cha kuwakamata watu wa kuitwa "wachochezi" pindi mitandao kama Twitter inapokuwa haiingiliki kwa mitandao ya simu ndani ya nchi, hali hii ikitokea jua ya kwamba chochote utachoposti mtandao usioingilika ni ushahidi tosha umetumia VPN.

Ila kwa wengine vpn inatumika kivingine kabisa.

Elimu ya kisasa imerahisishwa sana kwa video tutorials, Kuna wanafunzi wanahitaji hizo tutorials ila hawana hela ya kununua bando la Mb 300 kila siku, hapo ndio wengi wanakimbilia VPN kama ha tunnel ila changamoto ni kupata settings, hapo hadi uwe na connection ya wasukaji wa settings za kupenya bure wakupe faili, kila nchi na mtandao una settings zake.

Kwa watu wazima waliomo ndani ya mahusiano, kuna mitandao hufunza mbinu za kuongeza utundu wa kuchangamsha penzi, vpn haikwepeki.

Kuna wifi si salama hasa hizi za bure zipo zinazoingizwa kinyemela virusi vya kuiba taarifa, kuiba mawasiliano, kuiba mafaili ya simu, n.k. mfano uwanja wa Mkapa tunasikia wameweka wifi ya bure, amini kwamba wapo wadukuzi wa mitandao "watajaribu kuidukua" wifi, Ukiingia wifi iliyofanikiwa kudukuliwa uchi bila vpn kuna "risk" ya taarifa kuvuja bila kujali mtumiaji ni Rais, waziri, igp, mkurugenzi wa Tra, mtumishi wa ikulu, n.k teknolojia haiangalii cheo!!, kuna watu tunaingia nao hapo ni raia wa nchi zenye wadukuzi sugu huwezi jua malengo yao.
 
Kuna watu ndani ya hii nchi wanafikiri watatawala milele! Kisa tu ni ubinafsi wao, na tamaa iliyopitiliza ya madaraka.

Wamesahau kuna siku wao na watoto wao, marafiki zao, shemeji zao, vimada wao, wakwe zao, mwabwana zao, nk watakufa! Na nchi ndiyo itaendelea kubakia milele.
 
Ukitaka kuona uwezo wa viongozi wa Tanzania katika kufikiri. Angalia suala la utoaji wa vitambulisho vya Nida (vitambulisho vya taifa) ndiyo utajua akili za viongozi zilivyo.
Viongozi wa Tanzania badala wawaze maendeleo, wao wanawaza vyama tu.
Internet imekuwa anasa kwa Tanzania, kila siku vifurushi vinabadilika na kuwa ghari sana.
VPN haikwepeki
 
Inapiga ndo natumia😀😀
Ilishanishinda kutumia, natumia nyingine.
Hata VPN nao siku hizi wameanza kubana ilikuwa Droid wakaipiga pin ila sasa hivi nipo kwenye vpn matata japo spid siyo nzuri kivile naweza pakua hata 2GB.
WhatsApp, Telegram JF na kuperuzi website zingine siwazi.
Hata hii comment, nimetumia vpn
 
Vpn insaidia vipi kupunguza gharama ya kifurushi?
Mkuu Me sana kuna mtu alinielewesha aisee kumbekuna hizi Tunnel VPn mtu anatumia Mtandao bure kabisa na zote ziko playstore sikuwahi kuwaza Aisee 🤣🤣

Kuna Ha tunnel plus ,AM TUNNEL PLUS, AM TUNNEL PRO..AM nikambiwa kwa wateja wa Tigo..

Kumbe ni bora wazifungie Aisee zinaingiza hasara kubwa sana kwenye soko la internet kwa mitandao ya simu
Jana ishu ya vpn imenifunza mengi sana kumbe sio kilio cha vijana wa hovyo na wanasiasa pia ni kilio cha wale wasio kuwa na bando za kununua....
 
Ilishanishinda kutumia, natumia nyingine.
Hata VPN nao siku hizi wameanza kubana ilikuwa Droid wakaipiga pin ila sasa hivi nipo kwenye vpn matata japo spid siyo nzuri kivile naweza pakua hata 2GB.
WhatsApp, Telegram JF na kuperuzi website zingine siwazi.
Hata hii comment, nimetumia vpn
Dah Bora wazipige pin Aisee mkuu mnaharibu biahsra za mitaandao 😅😅
 
Mkuu Me sana kuna mtu alinielewesha aisee kumbekuna hizi Tunnel VPn mtu anatumia Mtandao bure kabisa na zote ziko playstore sikuwahi kuwaza Aisee 🤣🤣

Kuna Ha tunnel plus ,AM TUNNEL PLUS, AM TUNNEL PRO..AM nikambiwa kwa wateja wa Tigo..

Kumbe ni bora wazifungie Aisee zinaingiza hasara kubwa sana kwenye soko la internet kwa mitandao ya simu
Jana ishu ya vpn imenifunza mengi sana kumbe sio kilio cha vijana wa hovyo na wanasiasa pia ni kilio cha wale wasio kuwa na bando za kununua....
Tangu lini tapeli akapata hasara?
Hiyo mitandao ni matapeli na kila siku wanabadilisha vifurushi. Angalia uchumi wa wawatanzania wengi halafu kwa 1000 unapata mb 450 kweli?
Leo kupata 10gb lazima uwe na 20,000.
Umeweka hizo VPN kimakusudi sijui unamkomoa nani? Hizo vpn sijawahi kutumia, natumia zingine kabisa na ni mtelezo.
Mitandao ya simu imekuwa mitapeli sana acha nao watapeli.
Kipindi kile 1gb kwa buku, nani alikuwa anahangaika na VPN? Mimi mwenyewe nilikuwa sijui VPN ila nilipoona bando kila siku zinabadilika, nikaanza kwa Droid ila sasa situmii tena, nina chombo jipya. Siwazi bando.
Muvi ya 1.4Gb ununue bando la 3,000 mpk 4,000 ndiyo upakue? Hapana, wapate hasara tu, mimi sina msaada nao.
 
Back
Top Bottom