sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Sheria hii lengo lake ni kutoa kibali cha kuwakamata watu wa kuitwa "wachochezi" pindi mitandao kama Twitter inapokuwa haiingiliki kwa mitandao ya simu ndani ya nchi, hali hii ikitokea jua ya kwamba chochote utachoposti mtandao usioingilika ni ushahidi tosha umetumia VPN.
Ila kwa wengine vpn inatumika kivingine kabisa.
Elimu ya kisasa imerahisishwa sana kwa video tutorials, Kuna wanafunzi wanahitaji hizo tutorials ila hawana hela ya kununua bando la Mb 300 kila siku, hapo ndio wengi wanakimbilia VPN kama ha tunnel ila changamoto ni kupata settings, hapo hadi uwe na connection ya wasukaji wa settings za kupenya bure wakupe faili, kila nchi na mtandao una settings zake.
Kwa watu wazima waliomo ndani ya mahusiano, kuna mitandao hufunza mbinu za kuongeza utundu wa kuchangamsha penzi, vpn haikwepeki.
Kuna wifi si salama hasa hizi za bure zipo zinazoingizwa kinyemela virusi vya kuiba taarifa, kuiba mawasiliano, kuiba mafaili ya simu, n.k. mfano uwanja wa Mkapa tunasikia wameweka wifi ya bure, amini kwamba wapo wadukuzi wa mitandao "watajaribu kuidukua" wifi, Ukiingia wifi iliyofanikiwa kudukuliwa uchi bila vpn kuna "risk" ya taarifa kuvuja bila kujali mtumiaji ni Rais, waziri, igp, mkurugenzi wa Tra, mtumishi wa ikulu, n.k teknolojia haiangalii cheo!!, kuna watu tunaingia nao hapo ni raia wa nchi zenye wadukuzi sugu huwezi jua malengo yao.