Tangu lini tapeli akapata hasara?
Hiyo mitandao ni matapeli na kila siku wanabadilisha vifurushi. Angalia uchumi wa wawatanzania wengi halafu kwa 1000 unapata mb 450 kweli?
Leo kupata 10gb lazima uwe na 20,000.
Umeweka hizo VPN kimakusudi sijui unamkomoa nani? Hizo vpn sijawahi kutumia, natumia zingine kabisa na ni mtelezo.
Mitandao ya simu imekuwa mitapeli sana acha nao watapeli.
Kipindi kile 1gb kwa buku, nani alikuwa anahangaika na VPN? Mimi mwenyewe nilikuwa sijui VPN ila nilipoona bando kila siku zinabadilika, nikaanza kwa Droid ila sasa situmii tena, nina chombo jipya. Siwazi bando.
Muvi ya 1.4Gb ununue bando la 3,000 mpk 4,000 ndiyo upakue? Hapana, wapate hasara tu, mimi sina msaada nao.