Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako alafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.
Stress za uchaguzi mbaya sana
 
Mkuu uko sehemu gani ya nchi!? Ambako wafiwa wanapika!?

Si vibaya nikifahamu la kabila lako.

Duh.. Hatari kweli.
 
Yaani utakuta mmeuguza ndugu yenu zaidi ya miezi 3 hospitali. Tena mmeuza kila kitu ili kuweza kugharamia gharama za matibabu na mwisho wa siku Mungu ana twaa kiumbe chake...
Leo hii uanzee kukopa ili uwalishe watu wanaokuja kuzika.
 
Kama hutaki kupika na michango usipokee
 
Siumeona hapo mablack ndio wamemkimbilia kwa kumfariji. Sio kwamba wamemkimbilia mikono mitupu wakisubiri msosi tu!
 
Hizi ni taratibu za kabila la wajaluo. Mfiwa unawaandalia chakula wageni na kuwakaribisha
 
Mkuu misiba ya kwetu waafrika inajiendesha yenyewe.
We ni kutangaza tu kwamba umefiwa.
Tatizo pale wewe usipohudhuria misiba ya wengine katika jamii.
 
Vipi kuhusu ndugu wanaokuja kukuhani halafu wanaomba nauli ya kurudi kwao na hela ya kurudisha deni la nauli ya kujia
 
Nilivyokua mdogo kuna ndugu yangu alifiwa na mtoto, Baada ya kuzika tu kesho yake akaitisha kikao kuwaambia wale ndugu kuwa
"Sasa msiba umeisha tawanyikeni hamna haja ya kuendelea kuwepo hapa"

Utoto wangu ulinifanya nimtafsiri alikua na roho mbaya ila Sasa nimekua na nimeelewa jamaa alikua sawa
 
Misiba mingi watu huwa wanachangia ama pesa au chakula kwa kiasi kikubwa, na ndio hutumika kulisha waliokuja msibani. Hujawahi kusikia mfiwa anakoshwa kwa mahanjumati na nguo. Na panapo msiba uwepo wa watu nao unasaidia kumpa mfiwa faraja sasa unataka watu waje wazike tu then waondoke basi hata wasiwape compay wafiwa. Ila pia kama familia ina uwezo sio mbaya kulisha watu wakiokuja msibani mana inakuwa ni sadaka pia ya marehemu
 
Yaani utakuta mmeuguza ndugu yenu zaidi ya miezi 3 hospitali. Tena mmeuza kila kitu ili kuweza kugharamia gharama za matibabu na mwisho wa siku Mungu ana twaa kiumbe chake...
Leo hii uanzee kukopa ili uwalishe watu wanaokuja kuzika.
Sikopi aisee, wachangishane wajipikie chakula
 
Mungu akusaidie yasikufike kwa Umri huo. Huwezi kuwa na familia uwaze kuhusu vyakula kuliko mpendwa wako ulopoteza.

Hujajua utu ni nini jifunze upendo na ukemee roho ya Uchoyo.
 
Kijjiiini kwetu huo utaratibu haupo. Mnazika mnapewa matangazo ya utaratibu wa kunawa maji Ni lini na kutandua matanga Ni lini..then mnasepa. Kula Ni lazima pale mtu/watu wanapokuja kuhani msiba(baada ya mazishi) na Mara nying wamama wanakujaga na vyakula kwenye mafurushi yao (raw food Kama unga, maharage etc) kwa ajili ya kulisha watu msibani na wababa Mara nyingi huacha rambi rambi kwnye sahani husika pale msibani.
 
Ni kweli kabisa msiba na Arobain kunakuwa na madeni mengi.

Nimewahi kuona kwenye shughuli kama hizo wahusika wananunua maji ya katoni mengi sana, wanakodi viti, tent, maturubai. Usipo changa kwenye hiyo shughuli kama mwana Family au ukoo Ni ugovi mkubwa.

Shughuli inaishi Kuna madeni makubwa
 
siku hizi kuna hadi vyama vya kuzikana huyu jamaa sijui anakwama wapi
 
Mungu akusaidie yasikufike kwa Umri huo. Huwezi kuwa na familia uwaze kuhusu vyakula kuliko mpendwa wako ulopoteza.

Hujajua utu ni nini jifunze upendo na ukemee roho ya Uchoyo.
Uaitafute justification mkuu.

Hili jambo hata watu wazima waliotuzidi umri mimi na wewe,tena wana familia nabwenye kutambua utu linawatesa hasa wale ambao katika jamii zao mtu akifiwa ndo huyo huyo anaachiwa majukumu yote ya kuandaa chakula na hharama mbali mbali.

Alafu mkuu inakuwaje mtu kafiwa asipopika chakula uanze kumlaumu mchoyo ?

Ina maana huoni kama kafikwa na jambo zito kiasi kwamba umpe udhuru kuwa ilikuwa haki asipike ?

Huoni kama huo ni ulafi kutaka msibani wafiwa wapike ili ule wewe ?
 
Vipi kuhusu ndugu wanaokuja kukuhani halafu wanaomba nauli ya kurudi kwao na hela ya kurudisha deni la nauli ya kujia
Hao ni watu wakuelimishwa kuwa kama hawakuwa na uwezo wa kuja haikuwa na ulazima wa wao kuja kwa sababu kuja kwao haina maana kuwa marehemu atafufuka.

Sasa kwa wao kuja na madeni wanaongeza msiba wa pili huo.

Kiubinadamu wafiwa wasibughudhiwe hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…