Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Unaandika hivyo kwasababu haijawahi kukuta.

Kuna mambo yaache kama yalivyo.
Hapana ni suala la principles tuu hata mimi imeshawahi kunitokea na kwenye kikao cha familia nilipinga mwanzo mwisho habari za eti kununua ng'ombe, sijui kupika mawalii na mapilau, hakuna, chakula kilipikwa kidogo tuu kwa waliotoka mbali. Kila pesa au michango ilitunzwa na kutumika kwa umakini mpaka tukaondoa matanga na arobaini. Pesa ikabaki tukajengea kaburi na bado haikuisha tukampa mfiwa yote. Jamaa yangu mmoja eti wao wakakodi mpaka wapishi na kukawa na bufee kabisa. Mazishi kuisha ile siku wanafamilia wanakaa kikao wakakuta wana deni la milioni 3 na watu kuambiwa wachangie kila mtu anasema hali ngumu, ikabidi mfiwa akachukue mkopo Saccos sasa huo si ni ufala??
 
Kiuhalisia hili swala linakera.
Juzi nomepakiwa na bodaboda alikua analalamika jana yake wametoka kuzika na familia haikuwa na kitu...ikalazimika kukopa na kuandaa chakula kidogo nacho hakikutosha raia wakaanza kulalamika kuwa hawakushiba!
Unaona sasa?? Hii Mbaya sanaa
 
Kama familia ya mfiwa ndio inaandaa chakula, zile pesa tunazochangishagwa kwenye misiba ni za nini?
 
Sawa nitamuambia.

Nilichopinga mimi suala la wafiwa kugaramia chakula kwa ajili ya wazikaji,nadhani hukuelewa uzi.

Kwa ulivyosema wewe ndivyo inavyotakiwa iwe yani wanaokuja msibani ndo wachangie kama kupika papikwe wasaidiwe wafiwa.
Mkuu, hata kugharimia chakula bado ni suala la ujirani. Ndio maana huwa kuna michango au rambirambi. Na ukiwa na wasiwasi kwamba kutoa fedha itatiwa ndani basi nenda na mfuko wa sukati au mchele nk. Wafiwa wanaingia gharama nyingi sana, kwa hiyo mchango wako ni nafuu sana kwao.
 
sawa! watu wanakwepa aibu ndo maana wanapika..kumbuka kuwa si wote wanaokuwepo kwa msiba wapo kwa ajili hiyo, wengne wana yao apo ikiwemo udukuzi usio na tija ili siku moja mkikorofishana apate japo neno la kukuchamba!
 
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.
Ni suala muda tu. Itakwisha yenyewe. Sasa hivi watu wanajificha kwenye ratiba ya maziko kuwahi au wanaosafiri kuagia Muhimbili.
Yote kukwepa gharama
 
Mkuu chakula msibani ni mila ya kiafrika na ipo karne nyingi.
Kimsingi wafiwa wao hawapiki wao wenyewe kwa ajili ya msiba bali jamii inayo mzunguka mfiwa.
Nia ya mila hii ni kuwapunguzia wafiwa ukiwa na kuufanya msiba uwe wa jamii nzima.

Ukiitazama juujuu utafikiri msiba na kulisha waombolezaji ni jukumu la mfiwa, la hasha.
Tatizo linakuja pale mfiwa akiwa hana uhusiano mzuri na jamii inayomzunguka au hahudhurii misiba ya jamii yake.
Hapo mfiwa anaipata fresh.

Mila ya kuwapa waombolezaji chakula kabla ya mazishi ina ujumbe mzito zaidi. Kulisha watu ni kuwatakia heri ili maendeleo kimaisha yasikome, ni kama aliyefariki anawatakia heri wale waliobaki.

Huko Ulaya kuna jamaa yangu akiwa jirani na mzungu mmoja, apartment mlango huu unafuatana na mlango wake.

Kuna siku akapita jioni akitoka mishe zake akaona mlango wa jirani mzungu uko wazi na macho hayana pazia, kwenye kiti akamwona mke wa jirani yake kawasha mshumaa anaitazama picha ya mumewe huku machozi yakimtiririka.
Taratibu jamaa akaingia na kumuuliza mke wa jirani yake kulikoni?

Yule mama akamjibu kuwa mumewe amefariki mchana ule na hajui afanye nini maana amechanganyikiwa.
Huyu jamaa yangu akashituka, na akasikitika sana.
Lakini haraka akawaita waTanzania marafiki waliokuwa karibu.
Wakanunua vyakula na vinywaji na wakampa kampani yule mama hadi mazishi yalipofanyika.
Wazungu walioshiriki walikuwa wachache sana lakini waafrika walikuwa wengi.

Yule mama mfiwa kwa kweli alichangamka. Na baadaye alikiri kuwa waafrika wana moyo wa pekee duniani maana alikiri vile vile kuwa siku ile aliyomkuta akilia peke yake alikuwa akihisi kuchanganyikiwa na kutaka kujiua!
Alishukuru sana kwa kusaidia kubeba mzigo wa stress na kusema kuwepo kwao kulikuwa faraja kubwa.

Huu ni mfano ambao unaoonyesha jinsi sisi waafrika tumejaaliwa na Muumba namnaya kukabili misiba inayoleta matatizo makubwa kifikra kwa wafiwa.
Ni kweli mkuu umeongea jambo la kweli kabisa, na kwa mfano hai ulioutoa ndio itakiwavyo pale watu wanaposikia mwenzao kafa au kafiwa, ni jukumu la wajao msibani kuwafariji wafiwa na kuwapa matumaini badala ya kuwaongezea stress.
Tatizo ni hali iliyopo sasa hususan uswahilini sijui huko mitaa mikubwa, mtu kafiwa watu badala ya kuja kumfariji mfiwa wao ndio wa kwanza kumwongezea machungu, maiti bado iko hosp ina deni ikipatikana unatakiwa usafiri bado sanda bado kaburi heeee! bado maharage na uji au pilau tena wengine kwa nyodo anakwambia mi staki pilau nataka mweupe khaaa, mfiwa analia mno si kwa msiba pekee bali kwa yale yatokanayo na msiba.
 
Wewe endelea kujibana na hizo mali zako, siku ukifa tuko pale kupiga pilau na soda... dadadeeki!
 
Ila watu wa roho mbaya kwel.,chakula msibani it's is not a big deal...hizi ni chembechembe za roho mbaya...jaman...ebu mtoa mada fikiria vingine ila sio chakula msibani,...
 
Mkuu, hata kugharimia chakula bado ni suala la ujirani. Ndio maana huwa kuna michango au rambirambi. Na ukiwa na wasiwasi kwamba kutoa fedha itatiwa ndani basi nenda na mfuko wa sukati au mchele nk. Wafiwa wanaingia gharama nyingi sana, kwa hiyo mchango wako ni nafuu sana kwao.
Hata sikuelewi unasema nini ndugu.
 
Kama familia ya mfiwa ndio inaandaa chakula, zile pesa tunazochangishagwa kwenye misiba ni za nini?
Mchango umechangwa laki tatu

Gharama za chakula kwa wafiwa laki nne.

Ni sawa ndugu wa marehemu umewatia hasara ya laki moja nzima,bado ni gharama tu.

Ikiwa majirani watawachangia wafiwa haina shida.
 
Mimi huu utaratibu si uungi mkono kabisa! umeenea zaid mijini badala wafiwa wasaidiwe ndo kwanza wana didimizwa kwa kukomba hata kile kidogo kilicho bakia katika kumuuguza marehemu, Inapendeza msiba unapotokea inatakiwa majirani ndo wasaidie mahitaji muhimu ya msibani badala yake majirani ndo wanao tanguliza matumbo mbele huku wakiwa wamebeba pilipili na ndimu tayari kuupiga mpunga hii ni aibu !Na Haya mambo ya kutania misibani ni muda sasa yawe na kiwango maalumu yaani kama mtu akitania kuvuka mipaka hiyo ruksa kupasuka !
 
Huyu ni selfish individual tu..

Nafikiri ni mtoto pia.
Wanaolalamika nimeshawahi kuwaona watu wazima akiwemo babu yangu ambaye sasa hivi anakimbilia miaka 80 aliacha kufanya hayo mambo.Naye babu yangu pia pengine ni mtoto.
kwa ndugu tu mkuu wananchi wanatoa wanachoweza tumejiwekea standards ili kuepuka aibu kama zilizomkuta mtoa mada
 
Back
Top Bottom