Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Mimi ninaona huyu ndugu yetu @safuher alipaswa kusisitiza watu kutoa michango katika misiba kadri ya vipato vyao na sio kubagua utoaji wa huduma ya chakula.
Mkuu hapo sasa itabidi uanzishe mada wewe ya kusisitiza utoaji wa michango,lqkini kuona kuwa nilichoandika hakikutakiwa kiwe hiko sioni kama ni sahihi sana mkuuu
 
Mkuu, mimi binafsi ninadhani ulipaswa kuhimiza zaidi watu kuchangia fedha na chakula katika changamoto hii ya dharura ya msiba na sio kuweka msimamo mkali wa kugoma kuwapa chakula waombolezaji au kuwapa chakula kwa kuwabagua kuwa huyu ni wa mbali na yula ni wa karibu.

Ninadhani una jambo zuri sana la kuzungumza ila umeliongelea kwa namna ambayo sio sahihi.
Hayo yote nimeyazungumza kaka ila pengine hukuona umuhimu wa kusoma post yangu.

kuhusu kuhamasisha michango kama vile chakula si nimeshagusia hapa 👇👇👇kuwa wao ndo walete michango au chakula wakuletee mfiwa,sijui ulitaka nihamasishe vipi kaka.
Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.
Kama wameguswa na msiba wao ndo wakuletee vyakula...

Hii kauli inahamasisha watu wachangie chakula kwa wafiwa,kisha ndugu unataka nihamasishe vipi.

By the way mada yangu kuu ilikuwa ni kuwaambia majirani kuwa sio sahihi kula msibani kwa gharama walizoandaa wafiwa wenyewe,ni kukosa huruma.
 
Sawa ndugu yangu nimekuelewa vema
 
Mkuu hapo sasa itabidi uanzishe mada wewe ya kusisitiza utoaji wa michango,lqkini kuona kuwa nilichoandika hakikutakiwa kiwe hiko sioni kama ni sahihi sana mkuuu
Sawa ndugu yangu. Ninaomba radhi kama nimekukwaza
 
Yaan kabla sjajua Haya mambo,nilijua ukifiwa hupati gharama sana kama husafirishi maiti,Kumbe sku unapata msiba unaweza ulizwa unga uko wapi au kuni
 
Kumbe yamekukuta mkuu,watu wengine waanajali kula tu hawajui kama mtu kafiwa anahitaji achangiwe hata hiko chakula.
 
Hujui kwamba msiba ni sherehe ?
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.

NB ; kwa zile ada ambazo wanaokuja kuzika ndo huwa wanakuja na chakula na pesa za michango pasi na kuwatia uzito wafiwa basi ada hii haihusiani na mada yangu na ndio inavyotakiwa.
 
Je, mchungaji aliyekuja kuzika anapochukua sadaka yake kwani ni yeye kafiwa? Yaache yakae yalivyo watu siku hizi hawafikiri zaidi ya pua yao.

Wasabato niliwai udhuria msiba mchungaji alivyomaliza alikabidhi ile sadaka nishangazwa sana
 
Hayo mambo ya daslaam ya Dar.

Kijijini kwetu ukifiwa kila kitu kinaletwa na wageni kuanzia mbuzi n'gombe mahindi Michele..na wanapika wao wenyewe.

Daslaam hawawezi kukuelewa utapewa kila Aina ya jina hasa uswahilini na kuimbwa utaimbwa.
 
Kijijini kwetu ukifiwa kila kitu kinaletwa na wageni kuanzia mbuzi n'gombe mahindi Michele..na wanapika wao wenyewe.
Sasa huu ndio ubinadamu na ustaarabu wa kweli usiokuwa na utata
 
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.

NB ; kwa zile ada ambazo wanaokuja kuzika ndo huwa wanakuja na chakula na pesa za michango pasi na kuwatia uzito wafiwa basi ada hii haihusiani na mada yangu na ndio inavyotakiwa.
Inaelekea wewe sio mhudhuriaji wa misiba, na unamgonjwa ndani kila ukimwangaliiiia unaona kabisa hapa shughuli imefika ukingoni, Sasa huna kitu ndani na huna Cha kupika Wala wachangaji huna.
 
Ok boss,mm sitii neno hapoo ila
 
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.

NB ; kwa zile ada ambazo wanaokuja kuzika ndo huwa wanakuja na chakula na pesa za michango pasi na kuwatia uzito wafiwa basi ada hii haihusiani na mada yangu na ndio inavyotakiwa.
Kwa hili nakuunga mkono kabisa, kama wanavyofanya waislam wa Answaar sunni a.k.a suruali fupi.

Wapo sahihi.
 
Wao hupeleka chakula kwa marehemu na michango mingine au huenda na kurudi mikono mitupu tu ?
 
Wao wanapeleka chakula na vinywaji kwa mwenye msiba. Tena wanasema wafiwa wasiwashe moto kabisa kuandaa chakula.

Utaratibu mzuri kabisa.
 
Back
Top Bottom