Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.

NB ; kwa zile ada ambazo wanaokuja kuzika ndo huwa wanakuja na chakula na pesa za michango pasi na kuwatia uzito wafiwa basi ada hii haihusiani na mada yangu na ndio inavyotakiwa.
 
Kwa sisi wanyakyusa msiba ni ibada ya shukrani. majilani na ndugu huja na vyakula vyao msibani na kuweka kambi hapo mpaka matanga ya ishe.
Kazi ya wafiwa ni kukalibisha wageni na kuwaonyesha jiko liko wapi ili wageni waandae vyakula.

Kwa mijini kila mtu yuko busy inawalazimu wafiwa kuandaaa vyakula ndio maana tunatoa michango na sio vyakula moja kwa moja
Swala la wafiwa kuandaa chakula sio baya bali tujitahidi kujua tumetoka wapi.
 
Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Mii nimependa huu ubeti... Kwa jinsi ulivyo jitoa, Ya kwamba nikifiwa! Na sio nikifa!
 
Kiuhalisia hili swala linakera.

Juzi nimepakiwa na bodaboda alikua analalamika jana yake wametoka kuzika na familia haikuwa na kitu...ikalazimika kukopa na kuandaa chakula kidogo nacho hakikutosha raia wakaanza kulalamika kuwa hawakushiba!
 
Kiuhalisia hili swala linakera.
Juzi nomepakiwa na bodaboda alikua analalamika jana yake wametoka kuzika na familia haikuwa na kitu...ikalazimika kukopa na kuandaa chakula kidogo nacho hakikutosha raia wakaanza kulalamika kuwa hawakushiba!
lazima chakula mkuu
 
Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Mii nimependa huu ubeti... Kwa jinsi ulivyo jitoa, Ya kwamba nikifiwa! Na sio nikifa!
😀😀😀
 
Mkuu chakula msibani ni mila ya kiafrika na ipo karne nyingi.

Kimsingi wafiwa wao hawapiki wao wenyewe kwa ajili ya msiba bali jamii inayo mzunguka mfiwa.

Nia ya mila hii ni kuwapunguzia wafiwa ukiwa na kuufanya msiba uwe wa jamii nzima.

Ukiitazama juujuu utafikiri msiba na kulisha waombolezaji ni jukumu la mfiwa, la hasha.

Tatizo linakuja pale mfiwa akiwa hana uhusiano mzuri na jamii inayomzunguka au hahudhurii misiba ya jamii yake.
Hapo mfiwa anaipata fresh.

Mila ya kuwapa waombolezaji chakula kabla ya mazishi ina ujumbe mzito zaidi. Kulisha watu ni kuwatakia heri ili maendeleo kimaisha yasikome, ni kama aliyefariki anawatakia heri wale waliobaki.

Huko Ulaya kuna jamaa yangu akiwa jirani na mzungu mmoja, apartment mlango huu unafuatana na mlango wake.

Kuna siku akapita jioni akitoka mishe zake akaona mlango wa jirani mzungu uko wazi na macho hayana pazia, kwenye kiti akamwona mke wa jirani yake kawasha mshumaa anaitazama picha ya mumewe huku machozi yakimtiririka.

Taratibu jamaa akaingia na kumuuliza mke wa jirani yake kulikoni?

Yule mama akamjibu kuwa mumewe amefariki mchana ule na hajui afanye nini maana amechanganyikiwa.

Huyu jamaa yangu akashituka, na akasikitika sana.

Lakini haraka akawaita waTanzania marafiki waliokuwa karibu.

Wakanunua vyakula na vinywaji na wakampa kampani yule mama hadi mazishi yalipofanyika.

Wazungu walioshiriki walikuwa wachache sana lakini waafrika walikuwa wengi.

Yule mama mfiwa kwa kweli alichangamka. Na baadaye alikiri kuwa waafrika wana moyo wa pekee duniani maana alikiri vile vile kuwa siku ile aliyomkuta akilia peke yake alikuwa akihisi kuchanganyikiwa na kutaka kujiua!

Alishukuru sana kwa kusaidia kubeba mzigo wa stress na kusema kuwepo kwao kulikuwa faraja kubwa.

Huu ni mfano ambao unaoonyesha jinsi sisi waafrika tumejaaliwa na Muumba namnaya kukabili misiba inayoleta matatizo makubwa kifikra kwa wafiwa.
 
mkuu msibani si kuna michango alafu mfiwa huusiki kupika kwa uzoefu wangu wamama ndio huwa busy kuchakata mambo ya chakula kupitia michango labda kama wewe huwa hushiriki misiba ya wenzako so wanakususia alafu kuna utaratibu familia hujiwekea kama sisi mchango minimum ni elfu 50 labda uwe na kipato cha chini sana na tunajua kweli huna
 
Huo mchango wa elfu 50 ni mwananzengo au ndugu?
 
mkuu msibani si kuna michango alafu mfiwa huusiki kupika kwa uzoefu wangu wamama ndio huwa busy kuchakata mambo ya chakula kupitia michango labda kama wewe huwa hushiriki misiba ya wenzako so wanakususia alafu kuna utaratibu familia hujiwekea kama sisi mchango minimum ni elfu 50 labda uwe na kipato cha chini sana na tunajua kweli huna
Huo ukoo upo serious sana
 
Kwanza chakula kinacholiwa na wanaokuja kuzika kinachanwa na hai wanaokuja kuzika
Kwani NI hella yako
 
Kwa sisi wanyakyusa msiba ni ibada ya shukrani. majilani na ndugu huja na vyakula vyao msibani na kuweka kambi hapo mpaka matanga ya ishe.
Kazi ya wafiwa ni kukalibisha wageni na kuwaonyesha jiko liko wapi ili wageni waandae vyakula.

Kwa mijini kila mtu yuko busy inawalazimu wafiwa kuandaaa vyakula ndio maana tunatoa michango na sio vyakula moja kwa moja
Swala la wafiwa kuandaa chakula sio baya bali tujitahidi kujua tumetoka wapi.
Mjinga NI mfuwa haandau chakula
Chakula Cha msibani kinatokana na pesa zinazochangwa pale msibani
 
Back
Top Bottom