safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.
Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.
Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.
Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.
Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.
Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.
Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula
Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.
NB ; kwa zile ada ambazo wanaokuja kuzika ndo huwa wanakuja na chakula na pesa za michango pasi na kuwatia uzito wafiwa basi ada hii haihusiani na mada yangu na ndio inavyotakiwa.