Submeter Suluhisho la wamiliki na wapangaji Wa nyumba

Hapo kwenye kujua nani ana matumizi makubwa ni pazuri zaidi na nimepapenda.
Ila mtoa mada kasema suluhisho lipo
Hapa nilipopanga, umeme kwa mwezi nilikuwa nalipa 20,000. Ukiangalia matumizi yangu ni TV, Kuchemsha maji kwenye jagi, Sabufa, taa na kuchaji simu kibaya zaidi natoka saa 1 asubuhi na kurudi saa 12 jioni. Usiku mpk saa 5 nakuwa nimelala.
Kumbe kuna mpangaji hapa alikuwa anatumia friji lile la kizamani. Tangu nimefunga Sub meter siwazi tena masuala ya umeme.
 
Kila mtu atakula jsho lake. Ukifunga mbili mmoja asiponunua Atalala Giza wengine Mtaendelea kuinjoy Hii inakufanya Utumie kifaa chochote kwa maana ákimaliza umeme wako utabaki Giza. Submeter hizi pia zinauwezo Wa ku temper endapo kifaa chako kimepiga short Submeter itajizima na utapiga Simu kwetu tunakutumia Temper namba ukiweka itarudisha. umeme.
 
Kila mtu atakula jsho lake. Ukifunga mbili mmoja asiponunua Atalala Giza wengine Mtaendelea kuinjoy Hii inakufanya Utumie kifaa chochote kwa maana ákimaliza umeme wako utabaki Giza. Submeter hizi pia zinauwezo Wa ku temper endapo kifaa chako kimepiga short Submeter itajizima na utapiga Simu kwetu tunakutumia Temper namba ukiweka itarudisha. umeme.
 
Amina mkuu.
Maelezo yako yamenyooka sana.
Pasaka njema.
 
Nimejikuta nakupenda tu ghafla.
Sio kimapenzi, ni vile unavyotoa maelezo mazuri na yaliyonyooka.
You're a perfect gentleman....

Wifi yangu kapata mwanaume.
Unajua wanaume wengine wanajisikia sana, angejifanya hajaona post za watu za maswali hapa jukwaani.
Ila wewe umetujibu kiufasaha na kiuweledi kabisa.
Mungu akusimamie katika kazi zako.

Inshallah, tuombeane uzima, kama si mimi, nikiona mtu ana hitaji la mita za aina hiyo, nitakuunganisha nae.
Asante
 
Wapangaji wengine jau sana.
Ila hii separate meter ndo kiboko yao.
Friji za mtumba zile za zamani ni konyo.
Bora ulivyofanya uamuzi sahihi, japo najua lazima watakuwa wamekujadili.
Ila achana nao, pesa inauma sana
 
Basi haina msaada mkubwa
Nikajua ukikata kwako unabaki.
Kumbe nami nakaa giza kama wenzangu, tofauti tu ni kwamba wakichangishana wao, mie natulia tu.
Ila wote tunakaa giza hata siku 2...bado haisaidii 🤔
Hapo
Unatakiwa uwe na mbili au wao wabaki na sub mita wew ubaki na mita kuu yani wao ndio wa tumie iyo su
 
Hapo
Unatakiwa uwe na mbili au wao wabaki na sub mita wew ubaki na mita kuu yani wao ndio wa tumie iyo su
Asante mkuu.
Mtoa mada alitufafanulia vyema sana.
Mfano mwenye nyumba kakukataza kuifunga hio meter je?
 
Asante mkuu.
Mtoa mada alitufafanulia vyema sana.
Mfano mwenye nyumba kakukataza kuifunga hio meter je?
Huwez Sasa na swali LA muhimu kwann akataze??

, by the way akikataa huna namna ya kufanya mana hii sub
 
Hii inapunguza tu ila suluhisho ni kuweka mita yako.

Nyumba ninayokaa kila mpangaji anatumia hiyo ila ni lazima wote tuchangie umeme wa mita kubwa shida inakuja pale kuna watu hawataki kuchangia inakua mtihani.

Nashauri kama unataka suluhisho la kudumu heri mwenye nyumba akuwekee mita ya tanesco ya kwako.
 
Hata wakifunga wote bado itahitajika mita kubwa iwe na umeme unaojitegemea ili zenu zifanye kazi. Kumbuka ukiweka umeme na kujinunulia tayari unakua umehamisha zile unit kwenye mita kubwa kwenda kwenye mita yako. Ndo maana mfano mita kubwa ikiwa haina umeme na weww ukanunua umeme na kuweka mita kubwa ili uhamishie kwenye mita ndogo huo umeme hautaingia.
 
Hii ya kampuni gani na sh ngapi?
 

Kwamba hata unit zikiisha kwenye main meter ya Tanesco, mie kwenye submita yangu umeme utaendelea kuwaka as per my units? Hii sasa ndiyo watu wanataka... kila mpangaji atumie umeme wake binafsi, sio mambo ya sharing mita.

Japo nashindwa kuelewa, inawezekanaje submita iendelee kupokea umeme wakati Main Mita (Tanesco/supplier) inasoma 0 unit?!!!

au wewe Madame B umemuelewaje huyu ndugu Kulupango ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…