Sugu awatukana waandaaji wa fiesta kwenye facebook

Sugu awatukana waandaaji wa fiesta kwenye facebook

Msimamo wa Sugu kuhusu Fiesta ni Msimamo wa Chadema! Hata lugha ya Mr Sugu kuwa waandaaji wa Fiesta ni Wase.nge ni baraka za Kamati Kuu ya Chadema!
na wewe ni kati yao kama na wewe ni Clouse FM
 
Haya tutayaona pia kwenye majukwa ya siasa kutoka kwa sugu, subirini.
 
nyie ndo mnaosababisha wabunge waitwe waheshimiwa na waonekane km miungu watu kwenye jamii kwa sababu ya huu use..nge wa kuwa na nidhamu ya woga, acheni izo bwana, waoneni km watu wa kawaida ili wasipitishe misheria yao mibovu yakujilipa masurufu kibao.

Nani anawaogopa? Tungekua tunaogopa wabunge tusingekua tuna call out wabunge wakifanya makosa. Wenye nidhamu ya woga ni wewe na wenzako ambao mnaogopa kumsema "mheshimiwa" wenu sugu hata anapo kosea. Sasa kati ya mimi na wewe nani mwenye nidhamu ya woga? Yani unamuogopa SUgu mpaka akitukana unashindwa kusema kakosea? Duh....kweli unamuogopa.
 
Sijapata kuona wabunge wahuni kama Sugu na Lema! hata kama upatani na mtu uwezi kuandika matusi hivyo kama vile mvuta bangi, Sugu angekuwa sio mbunge wala hakuna angaelalamika, mbunge kutoa matusi ni ujinga wa hali ya juu

Mmh! Naona hapo nilipo- bold si kweli. Insult is an insult na uzito wake utategemea na tasfiri ya mlengwa/ mpokea ujumbe. I agree Sugu ametumia maneno makali sana kufikisha ujumbe wake. However, si kweli kwamba Sugu na Lema ndio wabunge pekee waliowahi kutumia strong language/insult kufikisha ujumbe. Kuna waliosemaga 1)....people should go to hell 2)... hata wakila majani ni sawa ndege ya raisi lazima inunuliwe 3).... waliopata ukimwi ni kiherehere chao etc etc. Hizi zote ni insult kubwa sana e.g. Kusema mtu mwenye ukimwi ni kiherehere chake ni tusi tena tusi zito mno. Binafsi nafikiri ukishakua kiongozi lazima uchague kwa umakini maneno yakutumia unapotaka kufikisha ujumbe. It is true that human beings go through certain challenges that ends up define them i.e. influence the way they act, talk etc. That is why the say "You can take a person from the hood but can't take the hood from a person" will always be true. However, when we hold certain positions in the society we should always remember: people put value on what we say and do. (Society defines us based on what we say and do). So it is our duty to ensure that what we say is exactly how we want people to portray us.
 
Juzi nilizungumzia ili swala na nikasema litawafikisha hawa watu mbali sana , utafikia wakati maneno na ubabe wa pesa/jeuri havitafanya kazi hapo ndipo bullet itakapohitajika kufanya kazi yake.
i wanna see bullets!
 
Hapa sasa ndio tunaona tofauti ya kila mgombea na hoja anazozitetea na ni kwa jinsi gani,
kama anachokitetea ni kwa manufaa ya watu wake au yeye binafsi,
Sugu kama ametumia neno hilo publically, ni shughuli,
Inawezekana ndio silaha aliyonayo kuhusiana na dhuluma wanazofanyiwa wasanii wenzake,
Malcom X namnukuu " By any means necesary!"
Pambana SUGU, kuwatetea wasanii wenzako
ukishindwa kurusha mawe watemee MATE!
 
Mtu gani mwenye akili timamu anayeweza tena kumchagua mtu anayemwaga mitusi mizito hivyo? Alikosa kabisa njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake kistaarabu?

wakati anachaguliwa kulikua na anti-virus inavuma mtaani,..
kama hauna nambie nikupe hakuna "mheshimiwa" kwenye antivirus ni zaidi ya ulichosoma facebook
 
Waandaaji wa fiesta wampeleke Sugu Mahakamani wadai fidia ya Bilioni moja kwa kutukana na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa ni *******!
 
Kupata attention ya rika mbalimbali? Ata pata attention ya watu kama wewe tu ila watu wazima watampotezea na hata vijana wenyewe uelewa watamuona hana maana.
lakini wewe upo kwenye mjadala!!ebu tujadili basi hoja yake mwelewa..we unaona sahihi UMAFIA unaofanywa na CLOUDS ENT??
 
magamba mna shida nyie! status ipi? Mr Sugu aligombea akiwa msanii na alipiga kampeni kisanii na wananchi wakamuelewa wakampa kura za kimbunga...tatizo lenu magamba ni unafiki...mnafikiri kufuga vitambi vikubwa na kusinzia bungeni kama wa..si...ra...na Kooomba...ndo uwakilishi???today nikiambiwa nichague kati ya mr Sugu na wa.si.ra kuwa wawakilishi wangu nitachagua mr sugu....by the way mbona mnataka kuaminisha watu kuwa fiesta ni ya ccm??? na kwa mtaji huo msiende arusha mtaabika kwa sana tu..
Sugu ni mbunge bwana wala sio magamba huwezi tetea matusi na uhuni anao fanya sugu! Tuache unazi wa vyama
 
lakini wewe upo kwenye mjadala!!ebu tujadili basi hoja yake mwelewa..we unaona sahihi UMAFIA unaofanywa na CLOUDS ENT??
Kama Sugu ana nia ya kweli ya kuwasaidia hawa wasanii anaodai wana dhulumiwa na Clouds FM kuna hatua anazo weza kuchukua ambazo zitawasaidia badala ya hii ya kutukana ambao haimsaidii yoyote. Kuna Baraza la Sanaa, kuna mamlaka inayo deal na media na pia kuna mahakama. Kama kweli anataka kuwa saidia basi awalete wasanii pamoja watafute mwanasheria waandae kesi ya kupeleke kwenye Baraza na mahakamani.

Njia nyingine anayo weza kusaidia wasanii yeye kama mbunge ni ku-author muswada na kuupeleka bungeni ili kubadilisha sheria zilizopo au kubuni sheria mpya ambazo zitalenga kuwalinda wasanii. Chadema ina wanasheria wengi tu anaweza akakaa nao na kuomba ushauri wa nini cha kuweka kwenye muswada. Pia anaweza kuita wasanii na kusikiliza kero zao na kujua ni mabadiliko gani wasanii wanataka.

Cha kushangaza it seems Sugu anaichukulia hili swala kuwa personal zaidi na wala si machungu na wasanii. Kwa nini yeye anapiga makelele kuliko hao wasanii wenyewe? Na kama hujui Sugu ana personal bifu na uongozi wa Clouds tokea zamani na ndiyo maana unamuona ana fura kwa kutukana. Sasa inamaana gani kuwa mbunge kama hatatumia resources za ubunge kuleta mabadiliko? Kama kutukana ndiyo jinsi ya kuleta mabadiliko basi ilikua hana haja ya yeye kuwa mbunge.

Ila kinacho shangaza zaiidi ni katika sakata lote hili sijasikia Sugu akikutana na wasanii na kuwauliza upande wao na pia sijasikia akiwauliza mashabiki wanataka nini kwa sababu matamasha kama FIesta yana jazwa na mashabiki. Sasa kukataza tamasha bila kuuliza wasanii wenyewe au mashabiki hapo inabidi ujiulize anamwakilisha nani sasa? Kama ana wakilisha wasanii je maoni yao hayajalishi?

Una lingine mkuu?
 
Hapa "Sugu" kakosea hata atetewe vipi. Hiyo lugha si tu ni mbaya kutamkwa na mbunge bali mtu yoyote yule hata kama ni msanii. Kama hizi ndiyo lugha za kisanii na bado ana taka kuzitumia arudi kwenye mzika. Kashaanza kuchemsha mapema ndiyo maana badala ya kupigia kelele vitu vya maana ana lalamikia Fiesta na ukichunguza ugomvi wake na Fiesta unatokana na bifu personal alilo nalo na watu wa clouds wala asijidai ni kujali wasanii. 2015 toeni huyu mtu.
kugushi nyaraka ni moja ya mambo CHADEMA wanayoyapigania.tujiulize kati ya sugu na hawa clauds nani wa kulaumiwa?tunamuonea huruma mwiz kwa kuwa anatoka damu,wakati hatutafakari madhara,adhaa na hasara na pengine hatar ya kuperuhiwa au kuuawa kwa aloibiwa.damu kwa mwizi isitumike kumuenz na kumuonea huruma mwizi,tukasahau kuwa aloibiwa alipata au alikuwa ktk madhara ya kupoteza uhai.CLOUDS ni mwiz wa SUGU,tusimuonee huruma kwa damu anayotoka muda huu.
 
Nilisoma maelezo ya Sugu jana. Kwa kadri nilivyoelewa ugomvi ni binafsi kati ya Sugu na Ruge kimaslahi. Mambo kama maslahi ya wasanii yanatumika kujaza watu tu. Matatizo ya wasanii yapo na Sugu anajua fika kuwa kama angedhamiria kuyatatua asingetumia njia anazotumia hata kama matatizo yote yangekuwa yanasababishwa na huyo hasimu wake kama anavyotaka tuamini.Tunahitaji hoja madhubuti kuhakikisha kuwa mgogoro huu unahusu maslahi ya umma, siyo maneno rahisi kama ufisadi, kuhodhi soko, chuki nk...

Umemaliza kila kitu mkuu. Hii ni personal issue kati ya Sugu na hao wenzie wa Clouds. Kama mbunge ana njia nyingi za kuaffect real change kwa maana kutukana hakusaidii wasanii. Na kama ana wajali sana hao wasanii mbona haja waita asikilize upande wao? Mbona yeye anajidai kuwa na machungu kuliko hao anaodai anawatetea?
 
kugushi nyaraka ni moja ya mambo CHADEMA wanayoyapigania.tujiulize kati ya sugu na hawa clauds nani wa kulaumiwa?tunamuonea huruma mwiz kwa kuwa anatoka damu,wakati hatutafakari madhara,adhaa na hasara na pengine hatar ya kuperuhiwa au kuuawa kwa aloibiwa.damu kwa mwizi isitumike kumuenz na kumuonea huruma mwizi,tukasahau kuwa aloibiwa alipata au alikuwa ktk madhara ya kupoteza uhai.CLOUDS ni mwiz wa SUGU,tusimuonee huruma kwa damu anayotoka muda huu.

Sawa Clouds ni wengi kama unavyodai. Sugu kama mbunge alipeleke hili swala Bungeni au akusanye wasanii watafute wakili wafungue mashtaka. Kutukana facebook ndiyo kutazuia wizi wa facebook? Kumbuka kinacho lalamikiwa hapa siyo the course Sugu aliyo amua kutake up bali ni njia anayo tumia. A the ends justify the means?
 
Shoga, mtoto si rizki, ****** n.k yote sawa tu mbona niliwahi kumsikia mbunge akiwa bungeni akisema mtoto si rizki na hakufanywa kitu.. Hayo ni maneno tu na kweli ni ******* kwani uongo!
 
Shoga, mtoto si rizki, ****** n.k yote sawa tu mbona niliwahi kumsikia mbunge akiwa bungeni akisema mtoto si rizki na hakufanywa kitu.. Hayo ni maneno tu na kweli ni ******* kwani uongo!

Hata huyo mbunge nae alitakiwa kukemewa. Mtu kutukana haijustify na mwingine kufanya hivyo. Au unataka kusema yeye ni bendera fuata upepo?
 
Na urudishe mapema hatutaki watu waogaoga katika mapambano haya!

Alichoandika mr 2 sugu kuhusu fiesta kwenye wall yake ya facebook



kama hii ndio chadema school of thought, muda si mrefu nitarudisha kadi niungane na mtikila.


Mods in jf tunasema "where we dare to talk openly"
so please if that is true then msiondoe hii thread.
 
Nilisoma maelezo ya Sugu jana hapa JF. Kwa kadri nilivyoelewa ugomvi ni binafsi kati ya Sugu na Ruge kimaslahi. Masuala kama "maslahi ya wasanii" yanatumika kujaza watu tu.



Hatukatai, matatizo ya wasanii yapo kama ilivyo kwa watz wengi wa kada mbalimbali na Sugu anajua fika kuwa kama angedhamiria kuyatatua asingetumia njia anazotumia hata kama matatizo yote yangekuwa yanasababishwa na huyo hasimu wake kwa asilimia mia moja kama anavyotaka tuamini.



Tunahitaji hoja madhubuti kujiridhisha kuwa mgogoro huu unahusu maslahi ya umma, siyo kutumia maneno rahisi kama umafia, ufisadi, kuhodhi soko, chuki ama matusi hatua aliyofikia...
 
Back
Top Bottom