Sugu: TRA siyo CHADEMA, acheni janja janja lipeni kodi

Sugu: TRA siyo CHADEMA, acheni janja janja lipeni kodi

Sugu kawaita Watanzania Niggaz.

Hakuna anayeona hilo kama tatizo?
Mweusi kumuita mweusi mwenzie hamuonekani kama ni tatizo.

Inataka kufanana na polisi mweusi akimuua raia mweusi kwa risasi na polisi mweupe akimpiga mtu mweusi kwa risasi
 
Usichepushe mada. Hakuna issue hapo!
Nchi inapokosa nidhamu kwenye mambo yanayoonekana madogo, kukosa nidhamu huko hujidhihirisha katika mambo ambayo yanaonekana makubwa.

Tatizo lile lile la kukosa kuheshimiana, linalomfanya mtu ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani na aliyekuwa mbunge kama Sugu kuwaita Watanzania "Niggaz", ndiyo lile lile linaloweza kusababisha TRA wajione wana haki ya kumuonea raia, au kumfanya raia ajione ana haki ya kutolipa kodi.

Watu hawaheshimiani, hawaheshimu mifumo, hawaheshimu sheria, mifumo nayo haiheshimu watu, taasisi za serikali haziheshimu watu.

Na usipoona hili kutoka muktadha huo mkubwa, utajikuta unachagua team tu, team Diamond, team TRA, team Sugu. Team CHADEMA. Team CCM.

Lakini huoni tatizo la msingi la nchi yenye watu wanaowindana na kudharauliana kila kona.
 
Jiwe alikua hazuii transaction alikua anachukua chote alichotaka kwenye akaunti yako yaani kwa mfano wamekuta milioni 100 wanakueleza wanachukua 50 wanakuachia 50 ndio ilikua biashara hiyo
Saizi hawachukui Bali wanafunga account ili ujitokeze kwenye mahojiamo yaani wakujulishe kosa
 
Kudos wanajamvi.

Legendary wa mziki na Mbunge wa Zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" amewataka watu maarufu na Wananchi kwa ujumla kulipa Kodi.

Sugu amenukukiwa akisema watu waache janja janja kwaninTRA sio Chadema na kwamba kulipa Kodi Ni Uzalendo.

Asante Sana Sugu kwa kuonesha uzalendo,Sasa umekomaa kisiasa na unatambua kwamba Nchi Ni muhimu kuliko Vyama.[emoji106][emoji106]

Kudos bwana Sugu kwa huu ujumbe wa kizalendo[emoji116]
View attachment 2464348
Huyu kila kitu anaingiza siasa. Wakati mwingine anadhani anajenga kumbe anabomoa. Jinga kweli hili.
 
Huyu kila kitu anaingiza siasa. Wakati mwingine anadhani anajenga kumbe anabomoa. Jinga kweli hili.
Kwa taarifa yako Asake wa Tandale ndiyo kaingiza siasa kwa kusema kuwa anadhani kuwa kuna mtumishi wa TRA ni mpinzani ndiyomaana anaikomesha Wasafi
 
Back
Top Bottom