Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
1. Wapi Yesu alihubiri miujiza ya pesa tu bila ya kuhubiri uponyaji au wokovu?Ukiona hivyo ujue kuwa huko kunakoitwa makanisa ya kweli wameshindwa kupata ufumbuzi wa shida zao
Wanaona tu kanisa kongwe ni sehemu tu ya kufunzwa Bible Study na kufunzwa doctrine tu za dini husika lakini solution za real problems za watu hawana!!
Ndio.maana watu wanakimbilia huko kwingine. Kungekuwa na solution walipo wasingehangaika kwenda kwa mitume na Manabii
Kanisa lijitazame ndani zaidi kuliko kulaumu huko wanakoenda na kuwaita hawajui neno nk
Mtu haendi kanisani kwenda tu.kukaririshwa mistari ya Biblia na doctorines za kanisa pekee!! Watu wana issues. Yesu na mitume walikuwa na majibu kwa real problems za watu hawakuishia tu kuwafundisha bible study na doctorines za kanisa
Acheni kutetea huu upumbavu maana BIBLIA inanena wazi
MATHAYO 5:9.
"Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu."
Je we hapo unapatanisha au unapotosha?
2. BIBLIA inadadavua tena waenende kwa SHERIA/AMRI 10 ZA MUNGU na SHUHUDA/MAHUBIRI NA MATENDO waliyofanya Manabii na Yesu.
Je hao Manabii wa kizazi hiki cha karne ya 21 wanafanya hivyo?
ISAYA 8:19-20.
"Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi."
3. Unaposema makanisa ya ukweli yameshindwa kupata ufumbuzi wa matatizo yao,
Una ushahidi gani?
Njia sahihi ni kuhalalisha hao Manabii wa uwongo?
Hawakutabiriwa na Mungu kuagiza Watu wajihadhari nao?
1 YOHANA 4:1-6.
MATHAYO 7:16-21.
MATHAYO 24.
2 WAKORINTHO 11:14-15.
4. ONYO:
UFUNUO 22:18-20.