Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Oooh!!!
Naskia Sabaya kakamata watu juzi hapo maeneo ya stendi ya Boma waliokua wanauza sukari nje ya bei elekezi ya serikali..
 
Siawatetei wafanya biashara mdogo yaani wenye maduka,Ila ukweli wao wananunua kwa Bei ya juu ndani ya maduka ya jumla Sasa wafanyeje,
Akiuza sh 3000/ kwa kilo korona Cha kilo 25 atakua amerudisha hela aliyonunulia tu,sasa atapataje faida? Hata ungekuwa wewe ndugu msomaji,kwa hiyo lazima aongeze 500 hapo ili nae apate faida, hapo anapata 500 Mara 25 sawa na 12500.
Kwa hiyo wakulaumiwa ni wenye maduka ya jumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maduka ya reja reja yamegoma kununua sukari kwa sbb wanabanwa wao washushe bei wkt wanainunua kwa bei kubwa.Vivyo hivyo kwa maduka ya jumla
 
Sukari ipo ila wauzaji hawauzi wanaificha wanadai serikaliimetoa bei elekezi wakati wanakoinunua wao wanainunua ghali
 
Corona no production hasa huko nje tunakotegemea
 
Na wewe bado sijui upoje; juzi tumeambiwa sukari ipo ya kutosha nchini lakini saiv hamna madukani, hiyo bei elekezi inaleta uwiano wa bei maeneo yote bila ukandamizaji. Mnatakiwa mkubali bei elekez na muache kuficha sukar
Hayo maneno ya wanasiasa ndugu au umeshau kipindi kile walipopiga marufuku sukari toka nje ikapanda toka 1800 mpaka kufikia 3000 na zaidi wakasema wameweka bei elekezi na kuanza wakamata wafanya biashara sukari toka kipindi hicho haikuwahi kurudi 1800 nao wakalipotezea wakaanza kudai walipoingia madarakani sukari ilikuwa 5000 wameishusha mpaka 2400
 
Corona no production hasa huko nje tunakotegemea
Mkuu kwa tanzania viwanda uwa havizalishi sukari mwaka mzima ila kipindi cha kiangazi maana nicho kipindi ambapo mashamba ya miwa yanaweza pigwa moto na kuvuna miwa, hivyo sukari inayokuwepo uwa inakuwa ni stock
 
Tumieni asali

by ~Eng Stella Manyanya
 
Mkuu kwa tanzania viwanda uwa havizalishi sukari mwaka mzima ila kipindi cha kiangazi maana nicho kipindi ambapo mashamba ya miwa yanaweza pigwa moto na kuvuna miwa, hivyo sukari inayokuwepo uwa inakuwa ni stock
Probably but hata ikiwepo haiwezi kutosheleza maana production ya viwanda vyetu ni ndogo mno
 
Juzi nimemtuma dada wa kazi sukari kauziwa sh 5000 nikamwambia airudishe tu
 
Lakini haka si ka nchi ka viwanda tena dona kantre kanakosaje sukari
 
Haitoshelezi mahitaji ya ndani tunapaswa kuruhusu sukari kutoka Uganda, Zambia na Malawi ndiyo bei ya sukari itakaa sawa. Huu uhaba unaweza usababishe magendo mengi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ndicho kinachotakiwa kufanyika..mizigo iingie ya sukari. Serikali isichukulie hili jambo kisiasa wakati ni ishu siriazi na wanachi tunapata shida
 
Sugar is not good for you.

Adults should never be crying over sugar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…