mlingoti west
JF-Expert Member
- Mar 16, 2020
- 252
- 195
Hili soko huria wameona isiwe shida wamewachia RTC ,NMC na SUKITA wauze Bei elekezi
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Malimao bora kuliko sukari. Tafuta asali, itakuwa tamu zaidi.Wakuu Salaam;
Nimezunguka madukani kutafuta sukari ili nipate chai angalau nichangamke kipindi hiki cha mvua maana baridi ipo kweli huku duniani niliko, sasa kila duka naloingia naambiwa sukari hamna!
Nimejaribu kwenda hadi maeneo ya stendi lakini bado sukari najibiwa hamna.
Nimeamua ninywe chai na malimao tu maana yenyewe yataifanya hiyo chai hata iwe na ladha. Malimao yenyewe saivi kuyapata ni shughuli haswa mana watu wananunua wakachanganye kwenye mvukizo ili wajifukize.
Nimejaribu kuwauliza watu baadhi wanadai sukari hakuna kila sehemu na watu wameficha stock ila hawana uhakika kama kweli wameficha. Sasa tatizo ni nini wakati juzi limetoka tamko lenye bei elekezi ya sukari?
Kuna mmoja kanidokeza kua, wale waliokua na sukari kabla tamko la bei elekezi halijatoka, waliendelea kuuza kwa bei ile ile ya juu yani 3500. Sasa wakikutwa wanauza bei hiyo au mteja akisema kauziwa kwa bei hiyo, muuzaji anakamatwa.
Kwanini ifikie hali hii sukari iadimike ghafla? Au kweli sukari hamna?
Au wafanya biashara wanaficha sukari?
Kama vipi serikali ije na tathmini mpya juu ya hili swala.
Huko ulipo vipi sukari inapatikana kama kawaida au nako hamna kama maeneo ya huku?
Na vipi kuhusu bei ya sukari huko ulipo? Au unatumia malimao kama mimi?
Sukari ipo shida ni serikal kuigilia soko hulia. Wao walitakiwa kupunguza tax kwenye sukar ili bei ishuke. Yani yenyewe inachukua chake alafu bei ishuke?Hii nchi kila kitu ni cha kubahatisha.
Kwa nini kila mwaka hua inafikia sukari hakuna? Yaani hua wahusika wako wapi hadi inatokea sukari inakosa kabisa?
Wenye maduka wamegoma kuiuza....wameona ni hasara....unauziwa bei kubwa hlf serikali inaleta bei elekezi.....hlf kinachokera zaidi wateja wako wanakuchoma
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nchi kila kitu ni cha kubahatisha.
Kwa nini kila mwaka hua inafikia sukari hakuna? Yaani hua wahusika wako wapi hadi inatokea sukari inakosa kabisa?
sukari ipo ila wenye maduka wanaona kwa bei elekezi watakula hasara, na wateja wanawachoma... Mimi nilienda dukani nunua sukari mwenye duka akaniambia siuzi ila kwakuwa nakufahamu nitakuuzia wewe tu kwa bei isiyo elekezi maana nikiuza chini nitakula hasara .
Kibamba yote hakuna sukari aisee, mpk vile vya pakt robo plus hakuna
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunarudishwa kwenye zama za Mchonga meno za chai na uji bila sukariWauzaji wa rejareja wananunua mfuko wa sukari wa 50kg laki na nusu.. wakiuza kwa bei elekezi ya tsh. 2600 kwa dsm watapata sh. 130,000/= hivyo atakua na hasara ya elfu ishirini bado gharama alizozitumia kwenye usafiri. Hili limekaaje wadau coz wafanya biashara wengi wamegoma kuuza sukari kwa kuhofia faini ya laki tano endapo atakamatwa akiuza sukari tofauti na bei elekezi?
kuanzia kilo 50
Tuletee hapa Kawe, maana bado maduka ya Jumla wanauza bei ya Juu ( Tshs 145,000 to 150,000 /50Kg ). Ukipiga hesabu hapo hakuna faida kwa Sisi wauzaji wa rejareja.uko wapi nikuletee kwa bei elekezi 😎 😎