Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Ni takribani wiki sasa tangu bei elekezi ya sukari kuwekwa hadharani na serikali kupitia waziri mwenye dhamana.

Mimi nimemuuliza leo wife kwa Dada Rose(Mchaga) sukari kanunua kwa bei elekezi ya 2600 TSH, kasema hapana.
Je, huko mliko bei elekezi inazingatiwa?

Kama haizingatiwi je, serikali imeshindwa kusimamia hili?

Au serikali ilitoa bei elekezi bila kuzingatia mambo muhimu kama upatikanaji na uzalishaji?
Ni ngumu na haitekelezeki kwa kuwa wauzaji wa Jumla wanauza zaidi ya bei elekezi ya serikali, sasa mfanyabiashara gani kichaa anunue sukari ambayo atakuja kuiuza kwa bei ya hasara, walichofanya wafanyabiashara ni kuacha kununua mzigo mpya na wale wachache walio nao bado wanauza kwa bei ambayo itawapa faida ambayo ni tofauti na ile bei elekezi ya Serikali
 
Nashukuru nilikuwa na msafiri kutoka Zenji ameniletea mfuko wa kilo 5 ambo alininunulia kwa 9000.

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Ni takribani wiki sasa tangu bei elekezi ya sukari kuwekwa hadharani na serikali kupitia waziri mwenye dhamana.

Mimi nimemuuliza leo wife kwa Dada Rose (Mchaga) sukari kanunua kwa bei elekezi ya 2600 TSH, kasema hapana.
Je, huko mliko bei elekezi inazingatiwa?

Kama haizingatiwi je, serikali imeshindwa kusimamia hili?

Au serikali ilitoa bei elekezi bila kuzingatia mambo muhimu kama upatikanaji na uzalishaji?
Huku kwetu, walipotangaza tu bei elekezi, wauzaji wakashusha bei ghafla. Agizo linatekeleza bila shuruti
 
Hai baada ya doria ya mkuu wa wilaya sasa sukari imepotea kabisa na ukiuziwa ni mpk mtu awe anakujua kama hakujui sukari ni hakuna.
Source Fb page ya redio Bomang'ombe
 
Back
Top Bottom