Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

View attachment 1441333Hizi ndio bei elekezi kwa Mikoa yote,chunguzeni kwa makini bei za mkoa wa Dar es salaam mtapata majibu sahihi kwa nini sukari hamna madukani,maana haiwezekani kwa mtu wa dsm auze sukari kilo 50 na kupata faida ya tsh 3000,wakati mikoa mingine wanapata zaidi ya 13000.
Kweli kabisa mkuu. Hayo yote yanafanyika kumkandamiza mfanyabiashara. Huku serikali ikijitafutia umaarufu kwa wananchi
 
View attachment 1441333Hizi ndio bei elekezi kwa Mikoa yote,chunguzeni kwa makini bei za mkoa wa Dar es salaam mtapata majibu sahihi kwa nini sukari hamna madukani,maana haiwezekani kwa mtu wa dsm auze sukari kilo 50 na kupata faida ya tsh 3000,wakati mikoa mingine wanapata zaidi ya 13000.
Mmh Aisee!
Hili jambo liangaliwe upya la sivyo muhafaka haupatikani
 
Kwa utafiti mdogo nilioufanya morogoro kwa njia ya kuhoji maduka kwa sample ya maduka 5 kama naweza kupata sukari ni duka 1 pekee ndio kuna sukari tena kwa bei ya 3400 per 1kg
 
miwa yote hapo mtibwa bado wanakosa sukari
 
Kiukweli, sukari imekuwa tatizo. Kwetu Visiga, Kibaha pia tunaitafuta kwa tochi sukari. Soon Serikali itafanya jambo!
Sio visiga tu... mpk Picha ya Ndege... Maili Moja..... hakuna sukari... walisema tutumie asali...
 
Ni kweli hakuna sukari hatari sana! Nahisi Waziri Bashungwa amekalia kuti kavu....!
 
Hivi tatizo hili la sukari kuadimika chanzo ni nini?
Tatizo ni kuwa na viongozi ambao hawaangalii ya mbele(hawana mipango) kila kitu ni zima moto, miaka yote ina julikana kuanzia mwezi wa tatu, viwanda vya ndani huwa vinasimamisha uzalishaji kutokana na matengenezo, na inajulikana uzalishaji wa ndani huwa hautosherezi matumizi kwa upungufu wa zaidi ya metric tones, 100,000,sasa viwanda vina simamisha, uzalishaji, huku serikali haiagizi huo upungufu kwa muda muafaka, inategemea nini??? Uhaba unatokea, wanaanza kutumia vitisho, wakati wanajua tatizo ni wao, sheria ya uchumi lazima tu itafanya kazi, supply vs demand. Juzi waziri wa biashara anaanza kusingizia eti corona, ndio chanzo!!! Kifupi sukari iliyopo nchini hautosherezi mahitaji, lazima bei iwe juu tu, hata iweje, yale yale ya kipindi kile eti bei elekezi iwe 1800!!! Ndio wakawa wameharibu!!! Mtu anauziwa kilo moja na muuzaji wa jumla kwa 2900, yeye una mwambia akauze kwa 2600!!!!???eti bei elekezi!!
 
Back
Top Bottom